Kila Shetani na Mbuyu Wake!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
IPTL Saga, Benjamin Mkapa

Richmond/Dowans saga, Jakaya Kikwete!

Ukirudi kumsoma Brian Cooksey, na varangati zima la IPTL, unabakia kushangaa na kuduwaa.

Nimeisoma ripoti ya Cooksey tena leo ikiwa ni mara ya 20 tangu ripoti hiyo itoke na kila siku inakuwa kama kuna kitu kipya kinafunuka!

Ni jinamizi gani lililowashika Viongozi na Watendaji wa Tanzania?

Ukijumuisha gharama halisi za tangu mwaka 1994 mpaka leo hii za mambo ya umeme, hii ikiwa ni mikataba na makampuni yote ya umeme (IPTL, Songas, Dowans, Artumas nk., halafu gharama za nchi kukosa Umeme tangu 1994 mppaka leo hii, utagundua kuwa Tanzania tumeshatumia karibu Dola Bilioni 2 za Kimarekani kuzungushana kuhusu suala la Umeme tangu 1994.

Fedha hizo zingetosha sana kutujengea Steiglers Gorge, kununua mitambo mikubwa na ya kuaminika na mengine mengi ambayo yasingetuleta hapa.

Sasa kila Shetani na Mbuyu wake, je tunakokwenda ni Ushetani gani na Mbuyu gani utatokea?
 
As long as ufisadi unaruhusiwa kuendelea kushamiri kama a way of life tutaendelea kushuhudia haya tunayoyashuhudia sasa na mengine mengi.
 
Yap ndo Bongo yetu hiyo mkuu wangu... Mbowe alisema afadhali ya mkoloni wakasema hajui anachokizungumza..
 
Ndo hapo sasa, maana pamoja na kasoro zote za mambo yanavyo kwenda tunaendelea kujidaganya kwamba mambo bado ni safi.
 
Mkandara,

Utani tuweke pembeni, nafikiri tumekwenda Mlingotini tukajiroga kuwa wajinga!

Cooksey anasema Mkapa alishinikizwa na Mahathir, pia kina Rugemalira nao walipiga domo la Uzalendo kudai Motoo Konishi na wenzake ni wakoloni.

Lakini najiuliza, hizi pesa za Capacity charges zinatoka wapi?
 
Mimi toka niliposikia kuwa asilimia 51 ya watanzania akili zao
zimedumaa.......kidogo nimeanza kuelewa

sishangazwi na lolote tena.
 
iptl saga, benjamin mkapa

richmond/dowans saga, jakaya kikwete!

Ukirudi kumsoma brian cooksey, na varangati zima la iptl, unabakia kushangaa na kuduwaa.

Nimeisoma ripoti ya cooksey tena leo ikiwa ni mara ya 20 tangu ripoti hiyo itoke na kila siku inakuwa kama kuna kitu kipya kinafunuka!

Ni jinamizi gani lililowashika viongozi na watendaji wa tanzania?

Ukijumuisha gharama halisi za tangu mwaka 1994 mpaka leo hii za mambo ya umeme, hii ikiwa ni mikataba na makampuni yote ya umeme (iptl, songas, dowans, artumas nk., halafu gharama za nchi kukosa umeme tangu 1994 mppaka leo hii, utagundua kuwa tanzania tumeshatumia karibu dola bilioni 2 za kimarekani kuzungushana kuhusu suala la umeme tangu 1994.

Fedha hizo zingetosha sana kutujengea steiglers gorge, kununua mitambo mikubwa na ya kuaminika na mengine mengi ambayo yasingetuleta hapa.

Sasa kila shetani na mbuyu wake, je tunakokwenda ni ushetani gani na mbuyu gani utatokea?


mkuu nimekusoma lakini hiyo fedha yote kuipata kwa mara moja sio kitu chepesi tatizo letu hatuna mipango ya mda mrefu, ndio maana kikwete kakurupuka iwashwe mitambo ya iptl,..hakujua hili tatizo au alikuwa wapi..mambo ya zima moto bwana..
 
Mimi toka niliposikia kuwa asilimia 51 ya watanzania akili zao
zimedumaa.......kidogo nimeanza kuelewa

sishangazwi na lolote tena.

ohhh my God.Pity! whats the reason behind? We must do something especially for the sake of the next generation!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom