Ndugu wana MMU poleni kwa majukumu. Mimi ni mwanaume mwenye umri wa kutosha kuwa na familia. Shida inakuja pale ambapo kila mchumba ninaemuona ananifaa kuoa na anaendana na sera zangu ananizidi kwa elimu. Nikimpata mwenye sera kama za kwangu aniuliza nina elimu ya kiwango gani?nikimwambia elimu yangu ananiambia kaka elimu yako haiendani na yangu. Na kwa bahati mbaya wanawake wote ambao nimekutana nao wamenizidi kwa elimu. Kama mnavyojua wanawake wenye elimu huwa wanapenda wanaume waliowazidi kwa elimu angalau kidogo. Mimi nina elimu ya form4 ila nimebahatika kuwa na kazi ambayo kipato chake kinanitosha kuendesha maisha yangu na pia mimi ni mjasiriamali. Nasema inanitosha kwani imenijengea nyumba ambayo ndo naishi kwa sasa na inaniwezesha kula vizur kila cku. Naombeni ushauri, nifanyaje nimpate wangu anaendana na elimu yangu?ukizingatia umri ndo huo miaka30.