Kila Nikiwatajia Kabila Wananikimbia

Hata mimi nitakupa mchango mkuu.
Nikiangalia avatar yako,uwa nacheka sana.
Kwa kuniongezea uhai,unastahili mchango wangu.

Asante mkuu Nzi, mpango mzima bado ukikamilika nitawataarifu wadau!
 
Du jamaa yangu mm nina mama mmoja anatafuta mchumba yoyote toka kule radi inapoanguka hata mchana kiangazi, kesho nitamweleza muwasiliane na picha yake nitaituma humuhumu JF

Mmmmh!!
 
aah mbona rahisi tu kama wewe ni wa huko...chagua umpendaye then rudi waambie wazee wako..yani utamkuta nakusubiri home!

Mmh! MJ umenichekesha..

@Katavi, usijali mkuu utapata mwenza kwa atakayekupenda kwa kabila kalo. Kwani kuna wafipa wangapi wameoa au kuolewa?!! usikate tamaa..
 
Nenda pale katumba,utachagua tena original from Burundi.Hawakatai wale
 
Naombeni ushauri kutokana na tatizo linalonikumba ktk haya mambo ya kimahusiano. Ni muda mrefu nimekuwa nikikimbiwa na wapenzi, na hii hutokea kila ninapowatajia KABILA langu. Mpenzi wangu wa mwisho niliamua kumueleza nia yangu ya kwenda kujitambulisha kwao, lakini alikataa kwa sababu kuwa hawezi kuolewa na mimi, hata kwao watamshangaa kuolewa na mtu kutoka kabila linalosifika kwa uchawi(sina uhakika na hili) na uhusiano uliishia hapo. Kutokana na umri kuanza kunitupa mkono, nimekuja kwa staili ya kuoa na nimepata binti mmoja ambae bado hajapata details zangu. Kutokana na experience niliyopata kutoka kwa wapenzi wa zamani, nafikiria kumdanganya kuhusu kabila langu ili naye asije akanibwaga.
Naombeni ushauri nikaoe kijijini mtu wa kabila langu au niendelee na mpango wa kumdanganya huyu kuhusu kabila langu!
Aaah mdanganye tuu,ameshazoea huyo hata hapo umeshamdanganya kuwa unampenda kaamini,sasa ataacha kuamini hilo kabila lako la uongo,ataamini kuwa humpendi mara tuu utakapo mtosa,hivi hivi hawazi kushtukia!!
 
Aaah mdanganye tuu,ameshazoea huyo hata hapo umeshamdanganya kuwa unampenda kaamini,sasa ataacha kuamini hilo kabila lako la uongo,ataamini kuwa humpendi mara tuu utakapo mtosa,hivi hivi hawazi kushtukia!!

Tehe tehe tehe!
 
jamani bahati kama hizi watu wanakimbia.kabila kitu gan kwan...dah ukiona wanazidi kukuzingua njoo kwangu...
 
Back
Top Bottom