Kila Kukicha, Tanzania ya Leo..Bora hata Tanzania ya Jana.....masikini Tanzania!!

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
Nikiamka asubuhi , napiga miayo na kujivuta vuta kupunguza uchovu wa kulala hoi usiku wa kuamkia leo. Naanza mishe za Mjini, namuita Brother abdallah dereva wa Taxi, Leo ananiambia bei imepanda...mh, Mchana naenda kwa mama niwekee ati naye kapunguza kipimo kwa kuwa 'vitu ni ghali'. Bosi ananituma nimnunulie dola Bureau de Change , leo Dola moja ni tshs 1800 wiki ijayo itakuwa alfu 2, jana ilikuwa 1750...Mmh. Nacheki Habari Arusha Kumechafuka. Salary Sleep imekatwa kodi kuubwa japo mgao wa umeme najua uliondoka kwa ajili ya mtoto wa Mfalme . Mchumba ananicall ati Vibaka wamechana wavu wa dirisha wameiba vijiko ati leo inabidi warudie zama za kula kwa Mikono. Mmh napita Kariakoo nanunua kijiko naweka Mfukoni kushuka kwenye daladala kimepinda hakitamaniki...kumbe feki bwana. Najaribu kumpigia simu mama kijijini kuuliza kama wamepata mvua japo kupanda viazi.... ati hakuna mvua wala mtoto wake manyunyu, baada ya nusu dakika Tigo wanasema salio halitoshi, jana nimeweka buku nikatuma mesaji kama tano hivi.....

Mmh Hii Ndo Tanzania! Kila Kukicha Bora ya Jana. Bora enzi za Utumwa , mababu WALIJUA kabisa ni Utumwa kuliko Utumwa tulio nao halafu hatujui kuwa ni Utumwa! Maisha Magumu...Kila Siku yanazidi Kuwa Magumu. Najiuliza Tunaishi ili kusubiri siku ya Kufa hapa kwetu japo wenzetu ulaya wanaishi kwa kusogeza mbele siku za kufa. Laiti kama tungekuwa na Uraia wa nchi mbili..labda ningechukua wa nchi nyingine nikajifiche huko .Ukweli uko pale pale naipenda Tanzania..ila.... Mambo yaendavyo yanaiosha nia ya kuwa Mtanzania!
Kadri siku zinavyoenda ,masikitiko ya kuwa 'mtanzania' yanaongezeka! Mungu nisaidie nisije kupoteza moyo wa Kuwa mtanzania!
 
Atakuja hapa Faiza Foxy atakwamba walitembea uchi enzi za Nyerere. Walijipanga mstari kununua sabuni. Sasa hivi mna barabara nzuri.
 
Atakuja hapa Faiza Foxy atakwamba walitembea uchi enzi za Nyerere. Walijipanga mstari kununua sabuni. Sasa hivi mna barabara nzuri.

Hao ni baadhi ya Watu ambao pengine Ubongo Unapoteza Function kwa umri wao mkubwa! Muhimu ni Kwamba kama wao waliishi hivyo ilikuwa enzi hizo. Maisha yangu ya sasa siyo atakayoyaishi Mwanangu!
 
Back
Top Bottom