Kikwete tumia helcopta kwenda Chalinze kutupunguzia adha za msongamano kila mara!

petu hapa,

Kama ww ni kiongozi, unatakiwa uwe na imani na msimamo. iwapo unaamini kununua chopper ni suluhisho la kupunguza foleni/gharama then simamia hilo suala unaloliamini kama kiongozi na kuwa tayari kuwa criticised na kujitetea kwa nini huo uamuzi ni mzuri. Lkn leo hii hawa viongozi wetu (wa kupeana) ukiwapinga hoja, utaambiwa unataka kumng'oa madarakani na ushuzi mwiiiiingi usiokuwa na maana!

you are right practice without logic is a killer.
 
Mambo mengine ni kweli yanakera sana, kwanza kutusababishia kuchelewa tunakoenda kwa foleni, pili msafara anaoambatana nao na gharama zake. Issue nyingine ni hii ya kusindikizwa na kupokelewa Airport na makamu wa Rais, Waziri Mkuu,na utitiri wa viongozi wengine hata kama ameondoka kwa masaa mawili. Mkuu wa nchi anahitaji kusindikizwa na kupokelewa,lakini sidhani kama ni busara kwa viongozi wote kujaa airport!!

true ish.... inakera sana tena sana !saa nyingine huwa nadhani hawa viongozi walio chini ya "serikali kuu" kazi yao ni kuabudu viongozi walio juu yao. WIZI MTUPU !
 
Inauma sana unajua! inakwera sana unajua! Eti mtu! raisi wako yupo, lakini hakujali, wala hakupendi, hana taimu na wewe!... wimbo wa q chilla - "ulinizaa wewe ukinikataa"
 
wewe umenikuna!! it is rather ridiculous!!kila baada ya siku sita lazima aende kwao huyu ana ikulu ana nyumba nyingine mjini hivi kama Mwl.Nyerere au Mkapa wageamua kwenda kwao kila weekend ingekuwaje safari za mara kwa mara zinathibitisha ubathirifu wa Kikwete!!kutohurumia hela ya wa Tanzania yaani ni rais wa kutumbua hela kwa jinsi anavyotaka yeye inashangaza sana ukiona ati wazee wakisema watu wasichukue form kuchallange mtu ambaye yuko so unconscious na matumizi ya fedha za umma hivi kama anapeleka salamu kwa ndugu kwanini asimtumie huyo mtu gari akabebwa na kuletwa ikulu!! kama ni shirikina anafuata kwanini huyo mgaga asiletwe kwake!! lakini kwa sababu ni fisada kama wenzie hana uchungu na hela ya watanzania na bado watu wanataka tuendelee na huu uozo!!I am sure 101% that kikwete hajui gharama za safari zake lakini laiti kma alijua alafu akawa rational!!huu upuuzi wa kwenda kila weekend kwao ungekoma given ans akili ya kutosha!!
 
Na angekuwa anatumia helikopta mungeuita ufisadi ,yaani sehemu ya kuendeka kwa gari anatumia helikoputa ,yaani mungekandamiza tu ,tunahitaji dikiteta ili apambane na mafisadi na wananchi sugu.
 
Raisi ni taasisi tena yenye maadili na maslahi kwa anaowatumikia,Naungana kabisa na Mkuu Kiroroma kwa hoja nzito aliyoitoa ,Ni hoja maridhawa kwa wakati muafaka inapaswa kupigiwa chepuo la nguvu hadi hapo Mkuu huyu wa nchi itakapopanda akilini mwake.Anaposema atumie helcopta hana maana ikanunuliwe kama za kina Obama La hasha!! amezungumza categorically kuwa zilizopo za jeshi la polisi na JWTZ zaweza kutumika kwa wakati rais anaenda umbali ambao unasababisha kero zisizokuwa za lazima kwa wanachi.
Aende Bagamoyo Chalize , au akitoka uwanja wa ndege alimradi anatumia miundo mbinu yetu finyu basi atumie usafiri wa helcopter,Kwanza kwa usalama wake pili bughudha anazowapa wapiga kura wake.Hili lilipaswa kutambuliwa na wote wale wanaomzunguka.

Lakini lipo lingine lililotajwa na wachangiaji;Kwamba pia anataka kuuza sura kwa wananchi pembezoni mwa barabara.Hili nasema aitishe mikutano mingi mingi ya hadhara kuwasalimia wanachi kila pembe ya nchi.Kwani kama amedumaza uchumi kwa kuzingatia mambo yaso muhimu kwa taifa, basi aendekeze ulimbwende ambao nadhani huko amekubuhu zaidi.
 
Inakera,inasumbua,tena inaudhi sana pale Rais Kikwete anapoenda kwao Chalinze mara kwa mara siku za mwisho wa juma kama leo asubuhi kwa msafara mkubwa wa magari,Acha kuwa ni gharama kubwa kwa Taifa ,muda ,na ujumbe anaoenda nao lipo hili jambo la kutusumbua sana sisi watumiaji wa barabara ya Morogoro.Kwanza ,magari yale yanaenda kwa kasi kubwa hatari hata kwa waenda kwa miguu.Pili,Traffic jams,magari kuwekwa pembeni na wakati mwingine watoto wadogo wanaokatiza barabara.Huu ni usumbufu usiohitajika kusababishwa na kiongozi wa juu kama Kikwete ,kwani ni gharama nafuu kuchukua helkopta ya jeshi au hata polisi kwenda mahali kama Chalinze.Sina maana ya gharama kifedha tuu bali hata usumbufu anaowapa watu wengine kama wananchi waishio kando kando mwa barabara ,askari polisi ,askari wa usalama barabarani,UWT nk nk.Si jambo geni kwa rais kutumia helkopta hata kule Marekani hutumika kumbeba rais badala ya kusumbua wananchi
,

Mkuu Kiroroma hapo umenena,Chukua tano kwa manufaa ya Taifa!!!!!!
 
,

Mkuu Kiroroma hapo umenena,Chukua tano kwa manufaa ya Taifa!!!!!!

.....Timor Nauliza vp YOYO au masanilo wamekuwahi? kama bado nakufungulia lango, binti karibu nyumbani au mpaka nipropose kwa luninga???

Kuhusu msafara wa Muungwana mie natoa hoja kwamba washauri wake wooote pale Ikulu wafutwe kazi kwani mie nijuavyo Rais hupangiwa na hajipangii mtoko. yeye anapropose kisha wataalm wanakaa chini kuangalia afanyacho kina tija gani kwa nchi kisha huandaa schedule. Hii ni aina nyingine ya uozo na ufisadi.
Nalishukuru sana Bunge letu kwa kulala usingizi wa pono mpaka mkoromo wake tunausikia... teh teh
 
Yap!!,

Hoja zote mbili zina walakini wa kuwa fisadi, nafikiri kinachohitajika ni mkakati wa kuziboresha barabara zetu ili kusiwe na unnecessary traffic jam.

Rgds
 
Mzizi wa tatizo ni rahisi sana. Watu tunaujua huo mzizi wa tatizo ila hatuutilii maanani na badala yake tunaishia kulaumu tu bila kupata ufumbuzi.

Mzizi wa tatizo tutaujua iwapo tutajibu maswali yafuatayo kwa usahihi:

1. Sifa za Rais bora ni zipi? Na tunaweka kigezo gani kumjua na kumchagua?
2. Zipi ni kazi za Rais? Nani anayempangia kazi Rais?
3. Nani anayehakikisha kuwa rahisi anatimiza kazi zake? Na kama hatimizi majukumu yake, ni chombo kipi kinastahili kumwajibisha?

Haya maswali ni very tricky na mzizi wa matatizo mengi sana yanaweza kuwa traced chanzo chake.
 
Hii ni hoja ya msingi,Wadau iangalieni mushauri Mkuu wa nchi acheni kung'ata meno tuu wakati wote!

Hakika mambo mazuri hayana budi kuigwa,Hatuwezi kuboresha miundo mbinu overnight,wakati mikakati inafanywa ni vema wewe akili zao za kuwashauri vinara hawa wa siasa kutumia mbinu mbadala kuliko kusubiri kuzitumia wakati wa kusaka kura tuu.Hizo hizo choper zinatumiwa na wao wakati wa kuwaendea wapiga kura.Sasa iweje wakati huu wa kuwapa kero za vingora barabarani wasifikirie kutumia hizo hizo zilizopo?
 
Raisi ni taasisi tena yenye maadili na maslahi kwa anaowatumikia,Naungana kabisa na Mkuu Kiroroma kwa hoja nzito aliyoitoa ,Ni hoja maridhawa kwa wakati muafaka inapaswa kupigiwa chepuo la nguvu hadi hapo Mkuu huyu wa nchi itakapopanda akilini mwake.Anaposema atumie helcopta hana maana ikanunuliwe kama za kina Obama La hasha!! amezungumza categorically kuwa zilizopo za jeshi la polisi na JWTZ zaweza kutumika kwa wakati rais anaenda umbali ambao unasababisha kero zisizokuwa za lazima kwa wanachi.
Aende Bagamoyo Chalize , au akitoka uwanja wa ndege alimradi anatumia miundo mbinu yetu finyu basi atumie usafiri wa helcopter,Kwanza kwa usalama wake pili bughudha anazowapa wapiga kura wake.Hili lilipaswa kutambuliwa na wote wale wanaomzunguka.

Lakini lipo lingine lililotajwa na wachangiaji;Kwamba pia anataka kuuza sura kwa wananchi pembezoni mwa barabara.Hili nasema aitishe mikutano mingi mingi ya hadhara kuwasalimia wanachi kila pembe ya nchi.Kwani kama amedumaza uchumi kwa kuzingatia mambo yaso muhimu kwa taifa, basi aendekeze ulimbwende ambao nadhani huko amekubuhu zaidi.

Nyinyi mnataka kummaliza ,hizi helikopta ikiwa mapailoti wanazikwepa kuranda nazo mnataka akapande raisi ,hapandi mtu wala Kikwete usiwasikilize kabisa hawa wanaokutafutia mauti kwa helikopta za kubebea mikungu ya ndizi ,huu si ushauri bali ni uuwaji ,kabisa ,kuna nchi matajiri na hawatumii helikopta kumpandisha raisi wao ,jamani wacheni kulinganisha AirForce One kile chombo kingine kabisa ,msione vinaelea jamani vimeundwa ,nyinyi hapa Bongo angalau gari zinatakiwa zikae pembeni kuna nchi njia zinafungwa kabisa tena kwa masaa ,ndio maana yake Raisi anapita au atapita ,sasa mnataka mpishane kwa miendo ya kasi ,eti mnashindana na raisi halafu ukajisifu ,kuwa umempita ,wacheni hizo tafuteni jingine ,hapa simtetei Kikwete ,isije ikaeleweka kuwa namtetea hapana wandugu hapa namtetea Raisi wa Tanzania au kwa namna nyingine natetea njia ya usafiri kwa kutumia Raisi wa Tanzania (Kwa yeyote atakaekikwaa).
Tunaposema Kikwete asitumie Cheo cha Uraisi au Mkapa alitumia cheo vibaya hakuna maana ya kumlinda yeyote yule ,ila tunakizungumzia cheo ,hivyo ni vizuri kutumia Cheo kuliko kumuelekeza kidole mtu ,hiki cheo si urithi wa Kikwete wala yeyote yule ,ni mali ya WaTanzania wote hivyo kinahitaji heshima na kuheshimiwa na kila mtu ,unaposema Raisi atumie helikopta jua kuwa wewe humtakii awaye yeyote Raisi usalama ,kwa ufupi unahatarisha usalama wa Raisi kwa kumtaka apande helikopta ,vyombo ambayo matengenezo yake hayataki ubabaishaji ,na ikiwa kwa kutumiwa na Raisi ni kitu ambacho kinatakiwa kiwe uptodate uwezo wa kuviweka vyombo hivyo uptodate hatuna ,kila kitu ni spana mkononi na mapailot wenyewe wanalielewa hilo.
 
Hakika mambo mazuri hayana budi kuigwa,Hatuwezi kuboresha miundo mbinu overnight,wakati mikakati inafanywa ni vema wewe akili zao za kuwashauri vinara hawa wa siasa kutumia mbinu mbadala kuliko kusubiri kuzitumia wakati wa kusaka kura tuu.Hizo hizo choper zinatumiwa na wao wakati wa kuwaendea wapiga kura.Sasa iweje wakati huu wa kuwapa kero za vingora barabarani wasifikirie kutumia hizo hizo zilizopo?

ni kweli hatuwezi kuboresha miundo mbinu overnight, YAANI HIYO SIPINGI HATA KIDOGO... lkn kama ulivyosema hapo kwamba ndo wapo ktk mikakati ya kuboresha miundombinu, unajua ni vizazi vingapi vimesikia that same sh*t over and over ? bado tu tuendelee kusubiri, hapana bana NOT THIS TIME. Ni dhahiri kwamba hawa jamaa wameshindwa kazi, na hawana sifa za uongozi!
 
Nyinyi mnataka kummaliza ,hizi helikopta ikiwa mapailoti wanazikwepa kuranda nazo mnataka akapande raisi ,hapandi mtu wala Kikwete usiwasikilize kabisa hawa wanaokutafutia mauti kwa helikopta za kubebea mikungu ya ndizi ,huu si ushauri bali ni uuwaji ,kabisa ,kuna nchi matajiri na hawatumii helikopta kumpandisha raisi wao ,jamani wacheni kulinganisha AirForce One kile chombo kingine kabisa ,msione vinaelea jamani vimeundwa ,nyinyi hapa Bongo angalau gari zinatakiwa zikae pembeni kuna nchi njia zinafungwa kabisa tena kwa masaa ,ndio maana yake Raisi anapita au atapita ,sasa mnataka mpishane kwa miendo ya kasi ,eti mnashindana na raisi halafu ukajisifu ,kuwa umempita ,wacheni hizo tafuteni jingine ,hapa simtetei Kikwete ,isije ikaeleweka kuwa namtetea hapana wandugu hapa namtetea Raisi wa Tanzania au kwa namna nyingine natetea njia ya usafiri kwa kutumia Raisi wa Tanzania (Kwa yeyote atakaekikwaa).
Tunaposema Kikwete asitumie Cheo cha Uraisi au Mkapa alitumia cheo vibaya hakuna maana ya kumlinda yeyote yule ,ila tunakizungumzia cheo ,hivyo ni vizuri kutumia Cheo kuliko kumuelekeza kidole mtu ,hiki cheo si urithi wa Kikwete wala yeyote yule ,ni mali ya WaTanzania wote hivyo kinahitaji heshima na kuheshimiwa na kila mtu ,unaposema Raisi atumie helikopta jua kuwa wewe humtakii awaye yeyote Raisi usalama ,kwa ufupi unahatarisha usalama wa Raisi kwa kumtaka apande helikopta ,vyombo ambayo matengenezo yake hayataki ubabaishaji ,na ikiwa kwa kutumiwa na Raisi ni kitu ambacho kinatakiwa kiwe uptodate uwezo wa kuviweka vyombo hivyo uptodate hatuna ,kila kitu ni spana mkononi na mapailot wenyewe wanalielewa hilo.

kwa hiyo mwiba,
unasema kwamba huna imani na hao marubani wa chopper au chopper zenyewe ? je unadhani chopper ndo suluhisho au nazo zitaleta mabalaa mengine kama gharama kuwa kubwa nk. iwapo rais atahitaji kutumia chopper every once in a while, then why worry kuhusu mechanical problems ? na nina imani kwamba tukiamua kuwa na mainjinia wa hizo chopper, tunaweza kuwa nao bila ya kuhitaji injinia toka nje ! chochote tukiamua tunaweza kuwa nacho ktk taifa hili !
 
Tukiamua lini ? Usifikiri wanaota kama uyoga ? Nilichokusudia ni hizo Chopper na sio marubani ,hatuna uwezo wa kumiliki chopper kwa kiwango cha kusafiria raisi na si mtu wa kawaida ambae roho yake ni moja tu ,ila Raisi anabeba watu wengi nyuma yake ,hivyo ndio ukaona msusuru wake unakuwa si mdogo au convoy lake sio dogo ,halafu mnataka kumpandisha katika chopa zinazobeba mikungu ya ndizi ,wacheni utani.
 
Mimi nina pendekezo rahisi!

Kwanini asisafiri Usiku wa manane na msafara wake huo... ? Kwa mfano akiondoka katikati ya Jiji mida ya saa sita za usiku na kutumia njia mbadala hadi maeneo ya ubungo na kutoka hapo kuchanga mbuga na msafara wake? si lazima aende Chalinze mchana au wakati kuna msongamano..
 
Mtamwita mchawi au mwanga ,hilo mnaliweza tena litakuwa habari kubwa na kwa nini asafiri usiku wa manane ,Raisi ndani ya nchi anayoiongoza ,tatizo ni nyinyi mshakuwa wazee na mshaona misafara mingi ya Raisi tokea zamani mkiwa wadogo ,lakini kwa wanafunzi na watoto wadogo masikini za Mungu wanafurahi kiasi wanaona msafara wa raisi na kuupungia mikono ila mizere na mijitu mizima inaona adha kubwa nasema hili ni tatizo linalosababishwa na umri na si vinginevyo.Mnaona mnacheleweshwa.

Tena namshahuri Raisi Kikwete awe ana tabia ya kuwarushia watoto fedha japo noti za mia mia anapokatiza katika mitaa ,ambayo atakumbana au anajua kuna watoto wanakuwepo karibu ya bara bara itapendeza sana.
 
Back
Top Bottom