Kikwete: Sijui kwa nini nchi yangu ni maskini

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Jamani rais wetu siyo dhaifu Mnyika anamwonea tu. Rais wetu mnamwonea bure tu kwani hata sababu ya nchi yake kuwa maskini hajui. Sasa atawezaje kupanga bajeti nzuri. Tumwache rais wetu aishi kwa amani. Chode chonde tusimdhalilishe jamani.
 
Ni kweli kabisa. Tusimwonee rais innocent asiyejua hata kwa nini watu wake ni maskini. Sijui huo ni udhaifu au ujinga!
 
Ni kweli kabisa. Tusimwonee rais innocent asiyejua hata kwa nini watu wake ni maskini. Sijui huo ni udhaifu au ujinga!

Aisee, yaani kila nikifikiria kauli hii najuta hata kwanini sikupata usingizi mrefu tangu 2005 na nije kuzinduka 2015, nisikione kabisa kipindi cha uongozi wa JK....ni zaidi ya neno DHAIFU!
Lakini nikaja gundua kuwa mawazo yangu yalikuwa dhaifu zaidi kuliko hata utawala wa JK ambao ki ukweli UMEOZA! Raia dhaifu husimika kiongozi dhaifu, tulishamgundua udhaifu wake mapema kabisa 2007, wengine tangu akiwa waziri, lakini udhaifu wetu umepelekea TUMKENULIE MENO hadi leo, wengine tukisingizia ameiba kura, kwani ni nani aliyepaswa kuzilinda kama sio sisi, kutokea kwa wizi sio ujinga na uzembe ama unafiki na usaliti wa walinzi! Kabla hatujamtukana tujitukane wenyewe kwanza! Udhaifu wetu umeleta raisi dhaifu vile sijapata kuona! Hakustahili kuvumiliwa hata kidogo! Lakin huyooooo, anaelekea kumaliza kipndi chake kwa heshima!
Watu wanacheza na mahesabu, wanawaingizia galasa madarakani, linawanyong'onyesha wenyewe mkijipa moyo "ATATOKA TU BAADA MIAKA 10" miaka inakatika anaacha mashimo aridhini, anakuja mwingine yale yale, kumbe tunaumiza watoto wetu wenyewe baada ya vifo vyetu vya kizembe! UOZO WOWOTE KATIKA TAIFA NI ZAO LA MFUMO MBOVU WA SIASA, YOTE TUYAONAYO NI ZAO LA DEMOKRASIA. Ubunifu haujawai kufika mwisho.
Mungu wetu anaita!
 
Mtasema mchana na usiku mtalala. Kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kupandisha pango. Bora maisha kwa kila mtanzania. Raisi huchaguliwa na watu, ikiwa rais aliyechaguliwa na watu anagundulika kuwa dhaifu basi hao waliomchagua ndio dhaifu zaidi, afadhali ya huyo. Nyani halioni nanihii lake, humcheka mwenziwe wakati huenda la kwake ni kubwa zaidi.
 
Kama mtakumbuka kauli hii aliitoa mapema tu katika awamu yake ya kipindi cha mwanzo,sijajua kama jibu lilishapatikana au la mpaka hivi leo.

Hivi sasa tunashuhudia ni kwa jinsi gani dhana ya kupanga ni kuchagua inavyofanya kazi kwa vitendo. Badala ya kutumia fedha nyingi katika mambo yasiyo na msingi tumeona ni jinsi gani tuyakavyoweza kupiga hatua kimaendeleo.
 
Bado haelewi kwa nini sisi ni masikini kwa sababu alikuwa busy na safari za nje kwenda kuomba misaada
 
Mm ningeomba kuwepo kipindi cha watumishi wa umma cha kuhoji Mali walizonazo watoa wapi? Na amelitumikia hili taifa kwa kipindi gani mpaka anakuwa tajiri kupita kiasi.
Na tuanze na riz1 maana huyu mtoto ni tajiri kuzidi watumishi waliolitumikia taifa hili zaidi ya miaka ya uhuru.
 
Back
Top Bottom