Kikwete On TBC1: Aongea na wazee wa mkoa wa Dar

Nitafurahi amalizapo kuongea aruhusu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wanahabari
 
maneno yote aliyokua akiyasema bibi kiroboto bungeni leo ndo anayarudia yaelekea waliongea sana na bibi kiroboto kablaa hajaingia bungeni iweje wote wanaongea jambo moja tena kwa lugha ilele ( staili na maneno pamoja na mpangilio ni ulele wa maneno) hapa najiuliza nani anamnukuu mwenzake?


ndio maana mimi nimesema huyu alimtia maneno mdomoni yule bibi kiroboto
 
Tatizo CDM wamewapotosha sana wananchi...ameamua mwenyewe atoe ufafanuzi!

Hapana siyo hekima. namsikia anafikia kusema kuwa Spika amekataa kuruhusu mswada kusomwa kwa mara ya kwanza. Hii kwa watu wa kawaida wanaweza kutafsiri kuwa spika amekataa kwa maelekezo ya Rais.

Ni vizuri rais kuwa na hekima. Tena anasema anashukuru Bunge limepitisha. Kama wewe ni mshauri wa rais basi mwambie rais awe na busara.

Anatamba hadharani kuwa bado siku 12 tu uanze kutumika. Kwamba, hapo siku za katikati atautia saini. This is very bad!

Sijui wewe unaliangalia kwa mtazamo gani?
 
hao ni wazee wa mji anaoishi-ingekuwa anaishi dodoma angezungumza na wazee wa dodoma
Sawa nini umuhimu wake toka Nyerere hadi JK kuzungumza na wazee wa Dar? mbona hamnipi elimu jamani?.. kwa nini wakutane na wazee wa Dar na kuwa hotuba ya Kitaifa hali wakienda Dodoma, Moshi, Mwanza hawafanyi hivyo..think about it.. kuna umuhimu gani wa rais kuzungumza na wazee wa Dar!
 
safi sana Rais wetu kikwete waambie hao wajinga wachache, wanaompinga ni wachache ambao hawana hoja wanasukumwa na UDINI.
 
Nitafurahi amalizapo kuongea aruhusu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wanahabari


walio wengi mle ndani hawawezi kumuuliza mwaswali ya kumchalenji..hata hivyo jk ni muonga wa maswali sidhni kama ataota nafasi hiyo
 
JK ana weledi wa kuongoza, jinsi anavyochambua mambo, anastahili kuitwa Dr. Kikwete. December 1, 2011, ni kuitia saini tu. WATZ tuwe pamoja na serikali yetu katika kipindi cha furaha na huzuni. JK anataka kuacha madaraka kukiwa na KATIBA MPYA
 
Back
Top Bottom