Kikwete na utitiri wa miradi Bagamoyo (Pwani)

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,219
79,498
Ifuatayo ni miradi inayoendelea au ipo njiani kuanzisha wilayani Bagamoyo au Mbegani au Mkoa wa Pwani kiujumla

(i) EPZ zone mbali ya kuwa kuna Kamal EPZ
(ii) Turkish University in Tanzania
(ii) World Tourism University for Africa
(iii) Muhimbili University campus Mloganzila
(iv) Uongozi Institute
(v) Bandari Mbegani
(vi) Uwanja wa ndege wa kimataifa
(vii) Kamal steel factory
(viii) Bagamoyo University
(ix) shule ya Wachina Bagamoyo
(x) IFM Msata
(xi) Global Industrial Park Mkuranga Pwani
(xii) Mount Ukombozi Health Sciences University Pwani

Naomba tuendeleze list hii na tuangalie kama viongozi waliopita wangefanya hivyo tungekuwa wapi leo? Je wenzetu wa Lindi, Mtwara, Shinyanga, Singida, Manyara na Tabora vp wao? hawahitaji huduma hizi sio?
 
Angepeleka New Kigamboni city Bagamoyo ingekuwa bora manake foleni Dar mjini ingekuwa historia
 
Angepeleka New Kigamboni city Bagamoyo ingekuwa bora manake foleni Dar mjini ingekuwa historia
Kwani nani kwakuambia hapo itakapokuwa haitapunguza msongamano? kinachotakiwa ni miundo mbinu daraja na kuwe na makazi pia huko
 
Ifuatayo ni miradi inayoendelea au ipo njiani kuanzisha wilayani Bagamoyo au Mbegani au Mkoa wa Pwani kiujumla

(i) EPZ zone mbali ya kuwa kuna Kamal EPZ
(ii) Turkish University in Tanzania
(ii) World Tourism University for Africa
(iii)Muhimbili University campus Mloganzila
(iv) Uongozi Institute
(v)Bandari Mbegani
(vi) Uwanja wa ndege wa kimataifa
(vii) Kamal steel factory

Naomba tuendeleze list hii na tuangalie kama viongozi waliopita wangefanya hivyo tungekuwa wapi leo

Mkuu Mloganzila ipo kibamba na sio bagamoyo
 
Mkuu maeneo kama bagamoyo na mkoa wa pwani yalisahaulika sana acha yaboreshwe!sasa wewe ulitaka hii miradi iende wapi?
 
Hujui kuwa sasa taasisi ya urais ni mradi wa familia, na familia ni pamoja na ndugu jamaa na marafiki.? Huko Bagamaoyo ndiko kuna ndugu wengi wa rais wetu wa sasa. Ole wao akina Nyerere, Mwinyi na Mkapa (kidogo tu) ambao hawakugundua kuwa uraisi ni mradi mzuri wa familia zao.
 
Ifuatayo ni miradi inayoendelea au ipo njiani kuanzisha wilayani Bagamoyo au Mbegani au Mkoa wa Pwani kiujumla

(i) EPZ zone mbali ya kuwa kuna Kamal EPZ
(ii) Turkish University in Tanzania
(ii) World Tourism University for Africa
(iii)Muhimbili University campus Mloganzila
(iv) Uongozi Institute
(v)Bandari Mbegani
(vi) Uwanja wa ndege wa kimataifa
(vii) Kamal steel factory

Naomba tuendeleze list hii na tuangalie kama viongozi waliopita wangefanya hivyo tungekuwa wapi leo
Ulitaka hii miradi iende posta au upanga.
 
Hayo mengine mimi sina shida nayo, shida yangu kubwa ni hiyo bandari, kwa nini fedha inayotumika kujenga hiyo bandari isitumike kuimarisha na kupanua bandari za Tanga na Mtwara na kuboresha hii ya Dar es Salaam?
 
Ifuatayo ni miradi inayoendelea au ipo njiani kuanzisha wilayani Bagamoyo au Mbegani au Mkoa wa Pwani kiujumla(i) EPZ zone mbali ya kuwa kuna Kamal EPZ(ii) Turkish University in Tanzania(ii) World Tourism University for Africa(iii)Muhimbili University campus Mloganzila(iv) Uongozi Institute(v)Bandari Mbegani(vi) Uwanja wa ndege wa kimataifa(vii) Kamal steel factoryNaomba tuendeleze list hii na tuangalie kama viongozi waliopita wangefanya hivyo tungekuwa wapi leo
Hao wakwere hata wapewe nini hawataweza, hawawezi kujikwamua kabisa. Angepeleka studio ya kurekodi nyimbo asilia na ngoma!
 
Angalia hata mgao wa fedha mbalimbali za maendeleo na capitation uliofanyika jana na wizara ya fedha Bagamoyo wamepewa fedha nyingi sana
 
Naomba nirudie nilichoandika kwenye thread nyingine siku chache zilizopita: Kikwete kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaonekana (kwa vitendo) kuwa na vision ya Pwani hasa Bagamoyo, na sio ya nchi nzima!
 
Umesahau Bagamoyo University ambapo mmoja wa chancellor ni Dr. Mvungi,****** ahamishie hata ikulu huko haitawasaidia wacheza ngoma wenzake
 
Kwani Kikwete ndio anaamua miradi iende wapi?

Miundombinu ya Bagamoyo ni mizuri kunafikika kwa bahari, umeme upo na maji yapo on top ipo karibu na Dar Es Salaam.

Hushangai kwanini kila kitu Dar?
 
Back
Top Bottom