Kikwete na utitiri wa miradi Bagamoyo (Pwani)

Kati ya hiyo miradi uliyoitaja kuna ile ambayo ni yenye umiliki binafsi wa wawekezaji ambao huwezi kuwapangai wakawekeze wapi maana wao wana priorities zao na wamefanya market na resources survey kabla hawajaamua kuwekeza. Kuna miradi mingine ilikuwa conceived kabla hata Kikwete hajaingia madarakani na inatekelezwa sasa kutokana na mpango kazi uliokuwepo wakati huo. Halafu madai mengine hayaingii akilini kwa sababu Bagamoyo ilikuwa nyuma na inahitaji na yenyewe kuonja maendeleo ambayo wananchi wake watajivunia na kujikwamua kutoka katika umaskini uliokithiri. Halafu utasema nini kuhusu Mkapa pale chini ya utawala wake ilipobuniwa Mtwara Corridor?

Kuhusu Bandari ya Mtwara, hiyo iko katika mpango wa Mtwara Corridor ambayo inahusisha pia utengenezaji wa barabara ya kuelekea Songea, Mbinga na Mbamba bay hadi Malawi na hivyo hivyo kuelekea Mozambique. Bandari ya Tanga iko kwenye plan ya kuunganisha reli hadi Musoma na baadae kuelekea Kampala. Mpango huu utahusisha ukarabati na upanuzi mkubwa wa bandari ya Tanga. Malalamiko mengine ni vizuri yakafanyiwa utafiti kabla hayajatolewa maana inaonekana yanatolewa bila tafakuri ya kina.
Huoni amelalamika tumipata majibu mengi hata sikuwahi kuya sikia....hata hivyo asante kwa majibu yako lakini hii itatekelezwa lini...
 
Mwache tu aipeleke, jinsi kutakavyo kuwa jiji ndivyo wakwere watakapokuwa wakimbizi, maana hawatabaki maeneo hayo.
 
Ifuatayo ni miradi inayoendelea au ipo njiani kuanzisha wilayani Bagamoyo au Mbegani au Mkoa wa Pwani kiujumla

(i) EPZ zone mbali ya kuwa kuna Kamal EPZ
(ii) Turkish University in Tanzania
(ii) World Tourism University for Africa
(iii)Muhimbili University campus Mloganzila
(iv) Uongozi Institute
(v)Bandari Mbegani
(vi) Uwanja wa ndege wa kimataifa
(vii) Kamal steel factory

Naomba tuendeleze list hii na tuangalie kama viongozi waliopita wangefanya hivyo tungekuwa wapi leo

Hata akihamishia Kariakoo Bwagamoyo watu wa kule hawabebeki labda afungue kumbi ya ngoma za asili
 
Hayo mengine mimi sina shida nayo, shida yangu kubwa ni hiyo bandari, kwa nini fedha inayotumika kujenga hiyo bandari isitumike kuimarisha na kupanua bandari za Tanga na Mtwara na kuboresha hii ya Dar es Salaam?

Na pia huo uwanja wa ndege wa kimataifa Bagamoyo iliyopo kilometer 25 kuktoka Dar kwa nini fedha zisitumike kuboresha jk Nyerere airport unaotuaibisha hivyo!? Ahh kweli tuna kazi!
 
Mwalimu Nyerere alipokuwa Rais,wapo watu wa Mara walisikika kusema kwamba,''Nyerere ni hoperess[yaani,hopeless]. Yeye ni Rais lakini hafanyi lolote kuuendeleza mkoa wa Mara.

Mtu mtakatifu ni mtakatifu tu mtu mkweli na asiye na tamaa ya mali. Nyerere angeweza kufanya lolote atakalo tena kwa Tz ya wakati ule wa miaka ya "kumi na tisa kweusi" watu walikuwa wajinga kwelikweli lakini cha ajabu ni kwamba hakufanya hivyo na watoto wake tunafanya nao kazi za kawaida tu hapa nanii.... Mtakatifu Nyerere pray for us!
 
Utawala wa majimbo utakomesha upendeleo wa Sehemu zembe kusubiri mgao wa hisani badala ya kufanya kazi kwa bidiii.Ndo maana jamaa wa CCM pwani walisema Kaskazini wasahau Urais ili wampe wa pwani mwingine waboreshe zaidi pwani ililnganelingane na kaskazini!!Mshindwe na kuzimia 2015 na mzinduke 2016 wakati Rais wa Wananchi atakapokuwa ameapishwa

Hakuna watu wanaoogopwa nchi hii kama watu wa Kilimanjaro! Kisa wale jamaa ni wachapa kazi kinoma na hawana utani na masuala ya maendeleo. Leo hii Kilimanjaro ni moja ya mikoa inayoongoza kwa maendeleo na vyou vikuu vingi na mashule ya sekondari ndio inaongoza kwa mbali (zaidi ya sekondari 350 wakari Dar secondary 150 bado). Lakini hizi hazitokani na kazi ya serikali ni nguvu za wananchi la sivyo Kilimanjaro ingekuwa maskini wa kutupa! Heko nyie akina mangi!
 
sio mbaya, ngoja apeleke huko, tutafika hata huko na wakwere watatuuzia viwanja watahamia mbali zaidi, huwa wana kwaida yakukimbia maendeleo, chukulieni mfano wa wazaramo, mbona wamehama mji?

sure umenikumbusha ngoja nikatie nanga huko watahama tu alafu nitachukua nchi pale yap!!
 
ahakikishe anatafuta pesa za miradi hiyo kabla ya miaka mitano,vinginevyo atakayekuaja anaweza akaipeleka miradi yaiana hiyo kwao manake yeye kaanzisha
 
Kama sisi ni wazalendo kweli tuache ushabiki wa kisiasa.Binafsi sina pingamizi endapo miradi hii itakuwa imeangalia context. Mfano, EPZ unataka kupark na kusafirisha nini huko Bagamoyo? I mean ni kitu gani kinachozalishwa Bagamoyo ambacho kilihitaji EPZ? Uwanja wa ndege kulikuwepo tetesi za kuwa utajengwa wilayani Mkuranga.....sasa kama ni Bmoyo naona kuna mashaka pia. Kwa hiyo Mkuu Priory of Zion suala si kupeleka wapi, suala ni maamuzi haya yamekuwa backed-up na socio-economic, environmental & context? Ukisema kisiasa inawezekana.
Kwa hiyo unataka maradi wa bandari uende Karatu au Hai?
 
Hulka ya watu wa huko sanasana wamezoea sherehe/mazishi na ngoma za asili!
 
Kati ya hiyo miradi uliyoitaja kuna ile ambayo ni yenye umiliki binafsi wa wawekezaji ambao huwezi kuwapangai wakawekeze wapi maana wao wana priorities zao na wamefanya market na resources survey kabla hawajaamua kuwekeza. Kuna miradi mingine ilikuwa conceived kabla hata Kikwete hajaingia madarakani na inatekelezwa sasa kutokana na mpango kazi uliokuwepo wakati huo. Halafu madai mengine hayaingii akilini kwa sababu Bagamoyo ilikuwa nyuma na inahitaji na yenyewe kuonja maendeleo ambayo wananchi wake watajivunia na kujikwamua kutoka katika umaskini uliokithiri. Halafu utasema nini kuhusu Mkapa pale chini ya utawala wake ilipobuniwa Mtwara Corridor?

Kuhusu Bandari ya Mtwara, hiyo iko katika mpango wa Mtwara Corridor ambayo inahusisha pia utengenezaji wa barabara ya kuelekea Songea, Mbinga na Mbamba bay hadi Malawi na hivyo hivyo kuelekea Mozambique. Bandari ya Tanga iko kwenye plan ya kuunganisha reli hadi Musoma na baadae kuelekea Kampala. Mpango huu utahusisha ukarabati na upanuzi mkubwa wa bandari ya Tanga. Malalamiko mengine ni vizuri yakafanyiwa utafiti kabla hayajatolewa maana inaonekana yanatolewa bila tafakuri ya kina.
hatuhitaji Bandari au Airport Bagamoyo (30 km from Dar) ni utumiaji mbaya wa rasiliamli akajenge lake Tanganyika (bandari) na Mwanza (airport) potentials ni kubwa zaidi ukiangalia nchi ya DRC na Mwanza na uchimbaji wa madini na rasilimali nyinginezo
 
Hapa jamaa anataka ajue miradi hii ikiwemo lukuki ya barabara imeenda huko kwa amri ya nani? Nani amepigwa memo? Issue si kusahaulika. Lindi, Singida, nk. Huyu jamaa kajipendelea ata kama unatokea huko. Must be an equal distribution of public income across all regions. Mkoa wake unazalisha kidogo ukilinganisha na miradi iliyofunguliwa kwa muda mfupi.
bandari ya dar au tuseme jiji la dar limezidiwa sasa unataka upanuzi wa dar uende singida na kuiacha bagamoyo?
 
Mwache tu aipeleke, jinsi kutakavyo kuwa jiji ndivyo wakwere watakapokuwa wakimbizi, maana hawatabaki maeneo hayo.
sasa kinacholalamikiwa ni kipi?huoni anawajengea nyinyi wa kilimanjaro, tanga na mbeya?
 
Back
Top Bottom