Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

asisingizie washauri yeye mwenyewe hakumbuki alituambiaga akili za kupewa changanya na zako, au na hiyo alikaririshwa na washauri wake
 
Pengine tumeamua kujenga uchumi kwa kutumia michezo maana kwa kutumia njia zingine mambo yamekuwa magumu.
 
Waje tu kutuburudisha,maana tunahitaji burudani sasa kwa kazi kubwa ya kuijenga nchi yetu,mpaka tumeendelea kiasi hiki cha kwenda huku na kule kuomba hela za kusapoti bajeti yetu,watuletee na chandarua basi,angalau kila mchezaje alete moja tu!!
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado Serikali ina dhamira ya kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania, 'La Liga' kuja Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa Hispania nchini kusaidia kufanikisha mpango huo.

Aidha, Kikwete ameipongeza Hispania kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita nchini Poland na Ukraine. Rais Kiwete alisema hayo jana Ikulu, jijini Dar es Salaam katika hafla ya utambulisho wa balozi mpya wa Hispania nchini, Luis Manuel Cuesta Civis.

Kikwete alisema: “Wananchi wa Tanzania, ambako timu za Hispania, zina washabiki na wafuasi wengi, bado wanasubiri kwa hamu ziara ya moja ya timu kubwa za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania. Tunataka ije hapa, icheze mechi moja ama mbili na itembelee mbuga zetu maarufu za wanyama.”

Aliongeza:“Kama utakavyokuja kuthibitisha mwenyewe, Watanzania ni watu wanaopenda michezo na hasa soka na ni wafuatiliaji wakubwa wa Ligi Kuu ya Hispania ambako timu zenye mvuto zaidi ni Real Madrid na Barcelona.”

“Tunawapongeza sana kwa kuweka historia. Kwanza mlishinda Kombe la Mataifa ya Ulaya, kisha mkashinda Kombe la Dunia. Sasa mmeweza kutetea Kombe la Ulaya. Hili halijapata kutokea kwa nchi moja kushikilia vikombe vyote viwili vikubwa vya soka duniani kwa wakati mmoja ama nchi kutetea Kombe la Ulaya.”

Wakati huohuo, serikali imesema imeridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wanamichezo walioshiriki michezo ya Olimpiki iliyomalizika Jumapili iliyopita, London, England.

Pamoja na wanamichezo hao kurudi bila medali, lakini serikali imesema wanastahili pongezi kwa vile walijitahidi kushindana kadri walivyoweza. Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa wanamichezo iliyofanyika muda mfupi baada ya kuwasili.

"Mmetujengea heshima kubwa Olimpiki, miaka ya nyuma wanamichezo wetu waliokuwa wakituwakilisha baada ya mashindano wanazamia uko, lakini nyinyi hakufanya hivyo" alisema Thadeo.

Mbali na kuwapongeza wanamichezo hao, pia Thadeo aliwakabidhi vyeti na medali za ushiriki kwenye michezo ya Olimpiki. Katika michezo hiyo, Tanzania iliwakilishwa na wanamichezo wa masumbwi, riadha na kuogelea, ambapo waliishia hatua ya makundi.

Yaan hii ndo mipango aliyonayo kwa nchi kama hii??nina wasiwasi na hizi safari zake za kila siku!!anaenda kuramba cone 2!!
 
Awachukue under 20 awapeleke huko for at least a year wakajifunze soka will be much help than this. Sie mbona tunaenjoy runingani tu.
 
Mmetujengea heshima kubwa Olimpiki, miaka ya nyuma wanamichezo wetu waliokuwa wakituwakilisha ,baada ya mashindano wanazamia uko lakini nyinyi hakufanya hivyo" alisema Thadeo.

Kweli kuna wachovu wa fikra nchi hii.
 
Hongera sana mheshimiwa Raisi , kwa kuwaleta Baca ama madrid ni njia mojawapo ya kutangaza utalii wetu
 
Acha fkra magamba ziara hzo ztakua na faida gan kwa mtanzania wa kawaida ambae hata kununua betr ya kuweka kwnye radio n shida kutokana na hali mbaya ya uchumi wa taifa le2 uliosababishwa na serikali ya CCM.Sekta ya michezo yenyewe inakufa kutokana na uwajibikaj mbovu wa viongoz,ni aibu 2meenda olimpiki hata medali moja hatujapata na bdo rais anawaza ku2letea timu za Real na Barca bila mikakat ya kuinua viwango vya wanamichezo we2.CCM IMECHOKA HAIPASWI KUAMINIWA TENA NA WATANZANIA M4C DAIMA
Kimaadili, kiuungwana, kiustaarabu na kidemokrasia, mimi ninaheshimu mawazo yako.
 
Mkuu Phillemon Mikael,
Wewe ni kiongozi halafu ni mkongwe humu JF tumia lugha ya tafsida kwenye kujenga hoja zako, sio vizuri mtu kama wewe kutamka Rais ni mjinga hata kama unapingana naye.

pumbaf kabisa. Hayo madili wanayotaka kula kodi zetu yafie mbali. Wanaacha kuanza kuandaa wachezaji wa michezo mingine mingi tu tunaiacha wanafikiria kuweka kambi za kina kaseja,ngasa, nk! Hivi hata kurusha mikuki, tripple jump, long jump hatuwezi kutrain watu wakafanikiwa? Huo ujinga wa kuleta sijui brazil, madrid, unatusaidia nini? Au ni kutafuta chance ya kupiga picha na kina ronaldo na messi? Hata huyo balozi nahisi alibaki mdomo wazi kuona state leader anaongea upuuzi ambao kwao unaoongelewa na mameneja wa timu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Phillemon Mikael,
Wewe ni kiongozi halafu ni mkongwe humu JF tumia lugha ya tafsida kwenye kujenga hoja zako, sio vizuri mtu kama wewe kutamka Rais ni mjinga hata kama unapingana naye.

pumbaf kabisa. Hayo madili wanayotaka kula kodi zetu yafie mbali. Wanaacha kuanza kuandaa wachezaji wa michezo mingine mingi tu tunaiacha wanafikiria kuweka kambi za kina kaseja,ngasa, nk! Hivi hata kurusha mikuki, tripple jump, long jump hatuwezi kutrain watu wakafanikiwa? Huo ujinga wa kuleta sijui brazil, madrid, unatusaidia nini? Au ni kutafuta chance ya kupiga picha na kina ronaldo na messi? Hata huyo balozi nahisi alibaki mdomo wazi kuona state leader anaongea upuuzi ambao kwao unaoongelewa na mameneja wa timu.
 
Last edited by a moderator:
mimi huyu raisi nimeshamchoka, kabisa awe anatumia akili zake au anashauriwa mimi kwa kweli nimemchokaa hafai kuendelea kutuongoza
 
kwa sababu watanzania ni wapenda michezo anafikiri anaweza kuwateka kwa kuleta hizo timu tunachotaka walimu na madokta waqlipwe vizuri hivyo ndio vipaumbele vyetu wala hizo timu haziwezi kutatua matatizo tuliyonayo
 
Hapa bora kusoma comments za wadau tu maana mnh.......... umebaki muda mfupi tusije tukaharibu funga za watu siku za mwisho.
 
Back
Top Bottom