Kikwete kuzileta Barcelona na Real Madrid kuwaburudisha Walalahoi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,800
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado Serikali ina dhamira ya kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania, 'La Liga' kuja Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa Hispania nchini kusaidia kufanikisha mpango huo.

Aidha, Kikwete ameipongeza Hispania kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita nchini Poland na Ukraine. Rais Kiwete alisema hayo jana Ikulu, jijini Dar es Salaam katika hafla ya utambulisho wa balozi mpya wa Hispania nchini, Luis Manuel Cuesta Civis.

Kikwete alisema: "Wananchi wa Tanzania, ambako timu za Hispania, zina washabiki na wafuasi wengi, bado wanasubiri kwa hamu ziara ya moja ya timu kubwa za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania. Tunataka ije hapa, icheze mechi moja ama mbili na itembelee mbuga zetu maarufu za wanyama."

Aliongeza:"Kama utakavyokuja kuthibitisha mwenyewe, Watanzania ni watu wanaopenda michezo na hasa soka na ni wafuatiliaji wakubwa wa Ligi Kuu ya Hispania ambako timu zenye mvuto zaidi ni Real Madrid na Barcelona."

"Tunawapongeza sana kwa kuweka historia. Kwanza mlishinda Kombe la Mataifa ya Ulaya, kisha mkashinda Kombe la Dunia. Sasa mmeweza kutetea Kombe la Ulaya. Hili halijapata kutokea kwa nchi moja kushikilia vikombe vyote viwili vikubwa vya soka duniani kwa wakati mmoja ama nchi kutetea Kombe la Ulaya."

Wakati huohuo, serikali imesema imeridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wanamichezo walioshiriki michezo ya Olimpiki iliyomalizika Jumapili iliyopita, London, England.

Pamoja na wanamichezo hao kurudi bila medali, lakini serikali imesema wanastahili pongezi kwa vile walijitahidi kushindana kadri walivyoweza. Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa wanamichezo iliyofanyika muda mfupi baada ya kuwasili.

"Mmetujengea heshima kubwa Olimpiki, miaka ya nyuma wanamichezo wetu waliokuwa wakituwakilisha baada ya mashindano wanazamia uko, lakini nyinyi hakufanya hivyo" alisema Thadeo.

Mbali na kuwapongeza wanamichezo hao, pia Thadeo aliwakabidhi vyeti na medali za ushiriki kwenye michezo ya Olimpiki. Katika michezo hiyo, Tanzania iliwakilishwa na wanamichezo wa masumbwi, riadha na kuogelea, ambapo waliishia hatua ya makundi.
 
Ndo vipaumbele vya watanzania, bado kwenda tena kubembea Jamaica kwa akina usain bolt
 
Ombi zuri lakini kwa mwaka huu haiwezekani tena kwani msimu wa La Liga ambao unaanza kesho tarehe 18/8 hadi tarehe 01/06/2013.

Ikumbukwe kuwa muda pekee timu za ligi ya Spain na Ulaya kwa jumla zinakuwa na ratiba iliyobanana sana wakati msimu unaanza kwani mbali na mechi za ndani, kunakuwa na mashindano ya Ulaya. Wakati pekee timu zinapokuwa huru kidogo ni pale wanapomaliza msimu.

Mhe. Raisi afuatilie ili ikiwezekana ziara hizo ziweze kufanyika baada ya msimu huu kumalizika.
 
Huyu Rais ni Mjinga Kabisa ...aliwaleta Brazil hapa kwa Gharama kubwa..walisaidia nini???....Kama hata kwenye viwango hatumo.....Olimpiki hatumo....timu wachezaji Saba ..wasindikizaji 10 na waziri ndie aliyewasindikiza eti Hadi London ila akawahii kurudi bungeni...
 
Kweli jamaa ni Janga la Taifa!! Hizo fedha si wangeongeza mosquito nets,mashuka na vitanda kwenye hospital zetu? Kama lengo ni utalii kwani TTB wanafanya kazi gani?
 
Huyu Rais ni Mjinga Kabisa ...aliwaleta Brazil hapa kwa Gharama kubwa..walisaidia nini???....Kama hata kwenye viwango hatumo.....Olimpiki hatumo....timu wachezaji Saba ..wasindikizaji 10 na waziri ndie aliyewasindikiza eti Hadi London ila akawahii kurudi bungeni...

Mkuu Phillemon Mikael,
Wewe ni kiongozi halafu ni mkongwe humu JF tumia lugha ya tafsida kwenye kujenga hoja zako, sio vizuri mtu kama wewe kutamka Rais ni mjinga hata kama unapingana naye.
 
Last edited by a moderator:
Kichwa ya huyu jamaa ni maalum kwa kufugia haflo, anayesema rais anadanganywa na washauri wake afikiri tena.
 
Hivi bado kuna watu wanamshangaa huyu JK, uwezo wake wa kuongoza umefikia hapo, mnategemea afanye nini cha ziada. Nadhani hajapiga picha na Messi, kwa hiyo anatafuta opportunity.

Eti anawapongeza wanariadha kwa kurudi hata kama hawajaleta medali, pongezi za nini, ni heri wasingerudi, nchi nyingine hawa wangekaa jela kwanza kwa kupoteza pesa zetu kila mwaka.
 
Ritz utaraumu watu bure. mambo ya huyu jamaa yanatia hasira, jambo la muhimu msiposit ishu zake za kijinga.
 
Tukisema madaraka ya Rais ni makubwa sana apunguziwe tunaambiwa sisi tuna nongwa, angalia sasa Rais anaamua kutumia pesa nyingi za watanzania bila hata ridhaa yao kwa jambo lisilo na mashiko.
Chonde chonde watanzania wenzangu tuna sababu za kuhoji kwanini hizo pesa zisitumike kwenye mambo ya msingi kama kuongeza walimu kwenye shule za kata,kuweka vitanda kwenye hospitali zetu au ni kwa vile wao na familia zao hawatibiwi huko? Mh. Rais Kikwete chonde chonde usitufikishe mahali tukaanza kujiuliza kama wewe kweli ni mwenzetu katika shida tulizonazo. Kama una nia hiyo basi weka wazi faida na hasara ya mpango wako huo na kwamba fedha utapata wapi, nyakati za kuwa na usiri kwenye fedha za umma umepitwa na wakati.
Kama mpango wako wa kuwaleta barca au real madrid ni kuwasahaulisha watanzania na madhambi yaliyofanywa na serikali yako unakosea, sula la kumtesa Dr.Ulimboka bado ni tete, fedha za uswisi ni tete,chenji ya rada ni tete nk nk.Acha kabisa mpango huo utatuongezea hasira juu yako na serikali yako.
 
Ombi zuri lakini kwa mwaka huu haiwezekani tena kwani msimu wa La Liga ambao unaanza kesho tarehe 18/8 hadi tarehe 01/06/2013.

Ikumbukwe kuwa muda pekee timu za ligi ya Spain na Ulaya kwa jumla zinakuwa na ratiba iliyobanana sana wakati msimu unaanza kwani mbali na mechi za ndani, kunakuwa na mashindano ya Ulaya. Wakati pekee timu zinapokuwa huru kidogo ni pale wanapomaliza msimu.

Mhe. Raisi afuatilie ili ikiwezekana ziara hizo ziweze kufanyika baada ya msimu huu kumalizika.
Acha fkra magamba ziara hzo ztakua na faida gan kwa mtanzania wa kawaida ambae hata kununua betr ya kuweka kwnye radio n shida kutokana na hali mbaya ya uchumi wa taifa le2 uliosababishwa na serikali ya CCM.Sekta ya michezo yenyewe inakufa kutokana na uwajibikaj mbovu wa viongoz,ni aibu 2meenda olimpiki hata medali moja hatujapata na bdo rais anawaza ku2letea timu za Real na Barca bila mikakat ya kuinua viwango vya wanamichezo we2.CCM IMECHOKA HAIPASWI KUAMINIWA TENA NA WATANZANIA M4C DAIMA
 
Back
Top Bottom