Ni lini Tanzania nayo itashiriki kombe la dunia la wanawake na mpira wa pete(Netball)? Michezo ni sekta muhimu kiuchumi kwa taifa

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Leo hii timu ya mpira wa miguu ya Hispania imeshinda kombe la dunia la wanawake mjini Sidney nchini Australia baada ya kuifunga timu ya Uingereza goli 1-0.

Goli la Hispania lilifungwa na Olga Carmona baada ya kupewa pasi maridhawa na Mariona Caldentey. Hispania wamecheza mchezo kabambe khasa wa mpira huku wakimiliki sehemu kubwa ya mpira na kutoa pasi za uhakika na kama si uhodari wa golikipa wa Uingereza Mary Earps, Hispania ingekuwa imeshinda kwa magoli mengi likiwemo goli alozuia kipa huyo kwa njia ya penalty.

Hizi zilikuwa ni fainali za kombe la dunia la wanawake ambapo timu ya wanawake ya Hispania imekuwa nchi ya pili duniani kwa timu zake mbili za wanaume na wanawake kushinda kombe la dunia nyuma ya Brazil ambayo timu yake ya wanaume ilishinda makombe matatu yote ya dunia kwa vijana wa umri chini ya miaka 17 na 21 na wakubwa kati ya mwaka 2003 na 2005.

Katika mashindano ya mwaka huu bara la Afrika liliwakilishwa na nchi nne za Morocco, Zambia, Nigeria na Afrika Kusini na ni Zambia pekee ambao hawakuweza kuvuka hatua ya mechi la makundi ya timu 16.

Pia kwa mara ya kwanza kama ilivyokuwa katika kombe la Dunia la wanaume nchi za Afrika za Morocco, Nigeria na Afrika Kusini zlivuka hatua ya mchujo wa mtoano wa timu 16 kwenda kucheza hatua ya robo fainali.

Pia kwa mara ya saba kulifanyika mashindano ya kombe la dunia la mpira wa pete (Netball) mashindano yalofanyika nchini Afrika Kusini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa mjini Cape Town. Nchi 16 zilishiriki mashindano hayo na Australia ikawa bingwa kwa kuifunga Uingereza kwa vikapu 61-45 huku Jamaika ikiwa ya tatu na Afrika Kusini nchi mwenyeji kuambulia nafasi ya sita.

Fainali za kombe la dunia la wanawake zimefanyika katika uwanja wa Australia au Stadium Australia ambao una uwezo wa kujaza watu zaidi ya 75,000 na upo katika jimbo la New South Wales ambako ndiko ulipo mji wa Sidney. Mji huo ulitanganzwa kuwa mshindi wa utafutaji nchi mwenyeji mwaka 2021. Pia kwa upande wa Netball Afrika Kusini walitangazwa kuwa wenyeji mwaka 2019 huku serikali na jimbo la Cape wakiwa nyuma ya jitihada hizo kuhakikisha mji wa Cape Town unakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Safari hii bara la Afrika likapoteza tena nafasi ya kujaribu kucheza hatua ya nusu fainali baada ya Nigeria kutolewa kwenye mashindano hayo kwa penalties na Uingereza.

Timu zote za Afrika zimecheza uzuri sana na zimeonyesha kuwa na nguvu na stamina lakini zikasindwa kuhimili ufundi na mbinu za timu khasa za Ulaya ambazo zina kila aina ya uwekezaji wa kutosha kuanzia katika vitalu vya watoto wadogo hadi wakubwa.

Suali langu kwa waziri wa michezo wa Tanzania ni kwamba:

Lini Tanzania itafanya juhudi kuhakikisha nchi yetu yashiriki katika michezo mikubwa kama fainali hizi za kombe la dunia katika maeneo ya mpira wa miguu kwa wanawake, mpira wa pete na mashindano mengine ambayo ni muhimu katika kukuza taswira ya nchi yetu kimichezo?

Pili, je serikali ina mipango gani kuhakikisha sekta ya michezo yaandaliwa kuwa sekta rasmi yenye kuweza hata kutoa ajira kwa wananchi wengine ambao watakuwa wakiajiriwa katika michezo hii?

Tukumbuke michezo hutoa ajira, hukuza utalii kwa nchi kuwa mwenyeji, hukuza mahusiano ya kibiashara, hukuza utamaduni kati ya nchi washiriki na masuala mengine mengi tu.

Lingekuwa ni jambo la mbolea sana kama Tanzania tungeanza na mshindano ya kombe la taifa kwa ngazi zote ukiwa ni mkakati wa kukuza morari wa michezo nchini na kisha kuandaa mashidano ya kikanda kwa Afrika Mashariki.

Michezo ni moja ya sekta muhimu sana kwa nchi khasa katika kukuza uchumi ambao utaongeza tija na kuifanya serikali ipate mapato yake yanotokana na shughuli za michezo pekee, hivyo kuondokana na fikra za kutengeneza tozo zisizo na idadi.
 
Hoja nzuri naomba nikujibu kwa kifupi sio rahisi Tanzania kufika huko kwani hakuna misingi ya michezo
Pita katika shule 10 unazozijua Kisha piga picha viwanja vya michezo katika shule hizo ukipata kiwanja Cha mchezo wa netball njoo unipe hiyo picha ukipata kiwanja kizuri Cha football njoo unipe hiyo picha
Unapozungumzia netball Australia wanaishi huo mchezo na nadhani ndio waasisi
Mwisho nadhani michezo sio sera ya michezo kwa nchi yetu ndio maana hata mashuleni hakuna vifaa Wala mafunzo kwa waalimu wa michezo
 
Tungeweza kuomba ushauri elekezi kutoka Morocco ambao timu zao za wanaume na wanawake woe wamefika fainali za kombe la dunia.

Si waliahidi kutujengea uwanja Dodoma?

Au tayari pesa imepigwa?
 
Viwanja vyote vya michezo kuanzia mashuleni mpaka open space zote zimeuzwa wakiona michezo haina faida na sisi na mwisho wake bila kuwaza mbali watoto wameamua kuwa panya road
Sasa sijui tuwe na mashindano ya wizi maana nchi nzima kila sekta ni wizi kuanzia wakubwa mpaka wadogo
 
Waliingiza Ndondo Cup naona ni ulaji wa watu.
 
Tungeweza kuomba ushauri elekezi kutoka Morocco ambao timu zao za wanaume na wanawake woe wamefika fainali za kombe la dunia.

Si waliahidi kutujengea uwanja Dodoma?

Au tayari pesa imepigwa?
Dunia ya Leo Wala sio ya kuomba ushauri mbinu maarifa na Kila kitu kipo kiganjani na kwenye vitabu suala ni maamuzi
Hatuhitaji ushauri kujenga viwanja vya netball mashuleni ambapo kiwanja kimoja ni kama 6ml tena unaweza kukitumia na basketball pamoja
Hatuhitaji ushauri kupeleka walimu course za michezo hapo ni maamuzi ambayo ndio hatuko tayari
 
Viwanja vyote vya michezo kuanzia mashuleni mpaka open space zote zimeuzwa wakiona michezo haina faida na sisi na mwisho wake bila kuwaza mbali watoto wameamua kuwa panya road
Sasa sijui tuwe na mashindano ya wizi maana nchi nzima kila sekta ni wizi kuanzia wakubwa mpaka wadogo
Viwanja hakuna watu wameanza kufanya mazoezi barabarani viwanja vidogo vilivyopo ni mnagombea karibu team nne kwa siku moja imefika hatua wengine wanacheza saa Sita mchana
 
Back
Top Bottom