Izack Mwanahapa
JF-Expert Member
- Apr 21, 2011
- 497
- 236
Ndugu wadau dalili zinaonyesha kuwa CCM wanajipanga kumuongezea Rais Kikwete muda wa miaka miwili kwa kisingizio cha kuandaa mazingira mazuri kwaajili ya katiba mpya. Moja ya wabunge wa CCM aliyeshangiliwa sana leo Bungeni wakati wa kuchangia mjadala wa mabadiliko ya katiba ni Livingston Joseph Lusinde (Mtera).
Ambaye amesema kuwa serikali inakabiliwa na matumizi makubwa ya fedha katika kipindi hiki yakiwemo yale ya chaguzi za serikali za Mitaa hivyo amependekeza Rais aongezewe miaka miwili ili katiba nzuri iandaliwe lakini pia akibeza baraza la katiba na wanaharakati akisema ni vibaraka wa wafadhili.
Wabunge wa ccm wameonyesha kufurahishwa sana na hoja hii maana ameshangiliwa kupita kiasi, si ajabu amepangwa.