Kumbukumbu ya Mapinduzi na Muungano: Sanduku la Kura Linapogeuka Kuwa Jinamizi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,261
KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI NA MUUNGANO: SANDUKU LA KURA LINAPOGEUKA KUWA JINAMIZI

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinakusudia kupeleka hoja ya mabadiliko ya 13 ya Katiba ya Zanzibar ili kuwezesha kuongezewa muda wa muhula wa uongozi Dk. Hussein Ali Mwinyi ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

“Tunaanza rasmi kuipeleka hoja hii mbele ya Sekretarieti ya CCM Zanzibar tarehe 10 Januari, 2014 ili utaratibu uanze.

Wala hatukushauri tumeamua sisi kwa sababu ilani ya CCM ya miaka mitano umeshaitekelza kwa miaka mitatu tu ya uongozi wako,” anasema Dk. Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar katika maelezo yake leo tarehe 6 Januari, 2024 mbele ya Rais Mwinyi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la kisasa Mwanakwerekwe, Zanzibar

Kwa mujibu wa maelezo ya awali ya viongozi wa CCM waliohudhuria hafla hiyo, inakusudiwa kuwa badala ya muhula wa uongozi wake kutimia 2025, Dk. Mwinyi amalize muhula wa kwanza mwaka 2027, miwili zaidi ya mitano inayoelekezwa na Katiba.

Rais Mwinyi aliingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa 2020, na Katiba inamruhusu kumaliza muhula mmoja mwaka 2025 na kama atagombea tena na kuchaguliwa, akamilishe mitano ya pili mwaka 2030 ambako atastaafu uongozi.


View: https://youtu.be/353oaRvPb2k?si=YmDuMmn73i2QpRsN
 
Back
Top Bottom