Kikwete in Dubai: On Transit.. kukutana na Al-Adawi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
Rais Kikwete na ujumbe wake wako Dubai wakiwa njiani kurudi nyumbani kutoka mkutano wake na Waziri Mkuu wa Uingereza huko London siku chache tu zilizopita. Vyanzo vyetu vya uhakika vinadokeza kuwa akiwa Dubai kuna uwezekano mkubwa Rais Kikwete kukutana Bw. Al-Adawi mmmiliki wa Dowans mwekezaji ambaye yeye alimualika kupitia Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz.

Hata hivyo, haijajulikana hadi hivi sasa kama Rais Kikwete au uongozi wa serikali unatambua kuwa kampuni ya Dowans Tanzania Limited ilianzishwa kwa kutumia false pretense pale iliposema kuwa mmoja wa wanahisa wake wakubwa ni kampuni ya Portek Systems and Equipment LTD. Hiini kwa mujibu wa nyaraka za kampuni hiyo zilizoko BRELA.

Uchunguzi wa kijarida cha leo cha Cheche unaonesha pasipo shaka kuwa kampuni ya Portek yenye makao makuu huko Indonesia haina hisa yoyote kwenye DTL kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa mara kwa mara na baadhi ya vyombo vyetu vya habari. LIcha ya hayo uchunguzi umeonesha kuwa kampuni ya Portek haijihusishi na biashara ya kufua umeme kama ambavyo iliandikwa na mojawapo ya magazeti ya Habari Corporation karibu miaka miwili iliyopita.

Chanzo chetu kinadokeza kuwa mojawapo ya maamuzi ambayo yanatarajiwa kuchukuliwa ni kuona jinsi gani serikali itaweza kuyanunua majenereta hayo licha ya upinzani mkali kwani ahadi iliyotolewa kwa mmiliki wa kampuni hiyo kuwa baadaya mkataba serikali itanunua majenereta hayo imeanza kuwa deni baada ya kuonekana ni vigumu kutekeleza ahadi hiyo katika mazingira ya sasa ya kisiasa nchini.

Hata hivyo, njia nyingine ambayo inatajwa tajwa kama desperation move ni kutokuweka timu nzito ya kuitetea TANESCO kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Mapatanisho ya Kibiashara (IAC) huko Paris, Ufaransa. Endapo TANESCO itashindwa kesi hiyo kampuni ya Dowans italipwa zaidi ya dola milioni 100 na kuzidi kwa kiasi thamani ya majenereta yenyewe.

Suala la kutaifisha mitambo hiyo haliangaliwi kwa ukaribu kama inavyodekezwa na wapasha habari wetu. "Kutaifisha wanaogopa kwani wanaona itatuma ujumbe mbaya kwa wawekezaji kuwa Tanzania inataka kurudi kuwa nchi ya kijamaa" amesema mdokezaji wetu.

Mwekezaji huyo wa Oman pamoja na washirika wake wa kibiashara bado hawajakubali kushindwa na wanatumia "ushawishi" wao wote kuhakikisha kuwa suala la Dowans linapotea katika vichwa vya magazeti ili hatimaye uamuzi wa kununua uje kutangazwa tu baadaye kuwa "ilikuwa ni lazima, tusingeweza kuacha nchi iingie gizani" tumetonywa.
 
kaka tunashukuru kwa kutuhabarisha kweli tumewabana nazani mpaka tulipofikia ingawa mafanikio ni madogo ila tunaweza kusema tulipinga japo kwa kuongea au kwa kupeperusha ujumbe kwa watanzania wengi kwa jinsi tuwezavyo.
mimi ningeshauri kila mtu afanye ambalo analiweza sio kila mtu anaweza kutuletea habari kama MM ila kwa sisi wengine tujaribu kuzisambaza hizi habari kwa kila mtu ambaye una contact naye. wengi wetu tunaogopa kufanya hivyo tunazani tutajulikana ila kuna njia nyingi sana za kufanya usijulikane. nazani invisible anaweza kutusaidi zaidi.
 
Mimi siku hizi ninashangaa sana ninaposikia watu wengi wakimuorodhesha Muungwana kama mpambanaji dhidi ya mafisadi!! Jakaya ni fisadi nambari wani kwahiyo kwake si rahisi kuwatosa wakina RA na EL akifanya hivyo atakuwa anacommit suicide; the most he does ni kujifanya akiwa jukwaani kuwa anapinga ufisadi kumbe nyuma yake anaukumbatia; kudhihilisha ninayosema nyie ngojeni maadam amepitia Dubai akirudi tu, utasikia serikali imeamua kununua mitambo ya Dowans!! Msijekushangaa huyo ndio mnamuita mpambanaji wenu!!
 
Itafika siku mambo haya yatawaumbua zaidi wanaohusika.

Kwasasa sioni kama kuna mtu mwenye uwezo wa kufikisha wahusika wa ufisadi mahakamani. Watavuna kila tone la jasho letu ili wawe na uwezo wa kuamua maisha ya waTanzania kwa kipindi kirefu. Ila kwa kufanya hivyo, wanachochea hasira za waTanzania ambazo haziko karibu sana (time bomb). Itafika siku tutaanza kuona yalitokea Romania (Ceausescu) na French revolution. Tukiwa na bahati yatatokea ya Madagasca.
 
Alikuwa london na wenzake akina Zenawi et al wakibeba bakuli kwa wazungu kutuongezea mahela wakati wao (wazungu) wanakabiliwa katika hali ngumu. Halafu anapitia Dubai kupanga namna bora na thabiti ya kumpa huyo mwarabu wa Dowans Sh 60bn kutoka katika hazina yetu kwa kununua mitumba yake.

Hawa akina Brown vipi? Hivi wanajua viongozi wetu wanavyofanya wakisha rudi huku na ahadi za mapesa?
 
Last edited:
Itafika siku mambo haya yatawaumbua zaidi wanaohusika.

Kwasasa sioni kama kuna mtu mwenye uwezo wa kufikisha wahusika wa ufisadi mahakamani. Watavuna kila tone la jasho letu ili wawe na uwezo wa kuamua maisha ya waTanzania kwa kipindi kirefu. Ila kwa kufanya hivyo, wanachochea hasira za waTanzania ambazo haziko karibu sana (time bomb). Itafika siku tutaanza kuona yalitokea Romania (Ceausescu) na French revolution. Tukiwa na bahati yatatokea ya Madagasca.

Na iwe hivyo
 
najiuliza watu wakishapata hizi habari wanafanya nini?

Hatufanyi chochote kwa sababu tunasubiri shujaa wa ukoo wa mashujaa azaliwe ili atukomboe kutoka katika makucha ya wakoloni weusi walio ndugu wa damu moja.
Tulizaliwa katika ukoo wa mwewe damu yetu ni ya mwewe, sura zetu ni za mwewe, hata makucha na mbawa zetu ni za mwewe.

Lakini kwa vile maisha yetu yote tumeishi katika banda la kuku na kulelewa kama kuku. Wote tunaishi kwa hofu ya kuku ya kuogopa kisu kutoka kwa mlakuku au kunyakuliwa na mwewe na kufanywa kitoeo.
Baada ya uwezo wetu wa kimwewe kuukalia na kudumisha woga wa kuku, Mzee MM unategemea nini kutoka kwetu?

Laiti tungejua kwamba sisi si kuku ila ni mwewe halisi.....!!!
 
juzi nimesema kama hukubaliani na suala la Dowans nitakupa namba za viongozi uwapigie kuwapa habari yao guess what? Mtu mmoja tu hapa na huyo ni mtu ambaye nina uhakika anaweza kufanya hivyo. Wengine wote wamebakia "conflict of interests"! doomed we are!
 
Huwa wanajifanya hawajaziona,obviously

NN huwa anasema JF ni kama kijiwe tu watu wanapiga soga, wanabishana, wanatambiana, wanaoneshana ujuaji, n.k halafu hao wanaondoka zao waiting for the next day. Naanza kuamini labda kuna ka ukweli fulani. Hivi tunapopata hizi taarifa zote tunafanya nini?

Well you might be very right.. we act as if we don't know. Are we anyway different from the typical Tanzanians?
 
najiuliza watu wakishapata hizi habari wanafanya nini?

Ni sawa na siku zile za pwagu na pwaguzi kama kawaida ya wa TANZANIA wanasubiri issue nyingie ije waongelee hakuna jipya kwao na ndio maana serekali inajuwa kuwa ina ongoza mamubumbu nothing they can do wanaonge sana kupindukia ni sawa na kelele za mlango hazimfanyi mwenye nyumba kushindwa kupata usingizi waswahili husema serekali imeshika mpini na wananchi wameshika makali
 
Nadhani I'll have to change strategy.. no I will change strategy. This is not working.
 
Nadhani I'll have to change strategy.. no I will change strategy. This is not working.

Mwanakijiji, ukweli ni kuwa watanzania walio wengi hawana ujasiri wa ku-grab the bull by the horns. Wengi tumeshindwa kuangalia the bigger picture kwamba hii impunity inayoonyeshwa na baadhi ya watu na hasa viongozi inatokana na nini. The bottom line ni kuwa uongozi kwa ujumla umeoza kwa kuwa umetokana na jamii iliyooza - na katika hali kama hiyo nani tumwamini tena. Hao wote tunaowaita mashujaa ndani ya mfumo huu, hawana ubavu wa kusimama wahesabiwe when things get too hot.

Siwezi kumwita shujaa mtu anayesita kusimamia analoamini kwa kuanza kuangalia maslahi yake kwa wakati huo - mabadiliko popote hayapatikani kirahisi namna hiyo. Fikiria mwana CCM ambaye anaamini chama chake ni kisafi ila kinachafuliwa na wachache, anapojikuta njia panda - nipinge, nisipinge...halafu kwa kulinda kinachoitwa mshikamamo - he agrees to swim with the current !! Baada ya hapo ana haki gani kutupa mawe. tunapenda vya rahisi rahisi.

Siku moja nilishuhudia mwanafunzi akinyanyaswa ndani ya dala dala na sikuweza kuvumilia nikanyanyuka kumtetea. Ghafla nilizungukwa na vijana wawili - mpiga debe na kondakta, wakinionya nisiwaingilie kazini. Pamoja na na dala dala kujaa abiria, hakutokea hata abiria moja aliyeniunga mkono na kila niliyemkazia macho alibaki kutazama chini. Niliogopa na kwa sauti ya unyonge niliwauliza kama kati yao hakuwepo mzazi - sikupata jibu. Ndio sisi watanzania tulivyo - je, hii ni laana ?.
 
Ukitoa makucha ya mkoloni mzungu, kisha pale pale penye kidonda cha makucha ya mkoloni mzungu ukapachika makucha ya mkoloni mweusi, unyonge utakuisha??
Tunatakiwa kupambana kwa nguvu zote ili kujitoa katika makucha ya wakoloni weusi.
 
najiuliza watu wakishapata hizi habari wanafanya nini?

Mkubwa taarifa hizi hazitulii zinapeperushwa kila kona. Kimsingi ndio zinazoharibu move zinazotegemewa kwani wakisha jua jamii ishastukia na iko very informed wanapunguza kasi au kuachana na deal hiyo kwani inakuwa feki tayari. Hivyo mkuu usichoke moto uleule. Hii inakuwa inculcated vichwani mwa waliowengi hivyo impact yake itakuwa njuri zaid kwa kizazi chipukizi wazee/mafisadi watapukutika naturally.
 
Back
Top Bottom