Kikwete hajui maana ya urais!

Kenge unaonesha moyo wa kitanzania kwelikweli, manaake watanzania hatuna kisasi, hatujali kuhusu raslimali zetu kama nchi, mtu akiiba asiibe yote ni sawa, kweli sote tunakuwa kama jinsi jina lako lilivyo! Hebu soma thrd ya Maige uona jinsi alivyokamatwa na TISS harafu! akili ni mali kila mtu anazake, lakini za kikwetu zina mushkeri!

Wewe Kasimba sina haja ya kulumbana na wewe, kwa sababu kama ni mwanafunzi basi wewe ni spoon feeding, wanafunzi wa aina hii hata mwalimu akiandika matusi ubaoni ananakili akijua ni sehemu ya mada aliyofundishwa. Ni kawaida kwa watu wasiotafakari jambo kukurupuka kuamini kila jambo. Subiri tu hao tunaowaamini kuwa ndiyo suluhisho la matatizo yetu yote hata lile la kujipatia fedha kununulia makufuli watimize malengo yao ya kutuletea utawala wa majimbo ili kuweze kufahamiana vizuri nani mchaga, na nani mkurya ili baadaye nasi warombo tutafutane manake ndugu zangu wengi wametawanyika sana
 
JK siyo mtu wa papara Mkuu, angalia suala la madaktari alivylimaliza kistaarabu?
Amemaliza vipi mkuu? Hivi unajua maana ya kumaliza tatizo? Au kwa sababu madaktari wapo kazini? Kweli wewe umetiwa upofu na hiyo nafasi uliokuwa nayo. Lakini kumbuka hapa duniani tunapita tu so hayo yote yanayokupa kiburi utayaacha. Ulaaniwe kwa dhihaka zako unazotupa sisi wa hali ya chini. Nakwambia kama hutotubu kwa hizi kejeli zako basi kila siku mpya ikianza utaona unavyoanguka hadi utakapotubu kwa mungu wako!
 
I don't want to quote you in any thing, but I strongly believe in INDIVIDUAL DIFFERENCES and Individual PERCEPTION...Haya uliyoandika ni mawazo yako na wala usitake kutulazimisha tuamini kama wewe. To me JK is nothing but like a shadow, it doesn't move unless the object moves....Huyo ndiyo JK. Hata kama ni ushabiki, kumshabikia JK lazima uwe waziri, mkuu wa wilaya, au mtu mwingine mweye cheo kikubwa serikalini au kwenye CCM. Lakini kwa sisi walalahoi...kumshabikia JK ni dhambi, tena dhambi kubwa....Sasa hivi imefikia watu wanavumilia kuwa watz na wala hakuna anayejivunia kuwa Mtz. Kikwete anafanya nini kikubwa ambacho kinaonekana hapo Magogoni?
1. Hakuna uwajibikaji serikalini....pengine kwa sababu na yeye anaogopa atawajibishwa kwa sababu na yeye ni wale wale.
2. Gharama za maisha zinapanga huku shilingi ikizidi kuporomoka....hakuna juhudi za dhati zinazoonekana kuhakikisha hali hii inaondoka.
3. Umeme wa kusua sua kila siku, na ahadi zisizotekelezeka.
4. Huduma za afya mbovu...hakuna dawa, hakuna vitanda na hakuna vifaa vya kufanyia kazi.
5. Elimu iko taabani....hadi leo, miaka hamsini ya uhuru, kuna shule kibao watoto wanakaa chini, waalimu hawana makazi, hakuna vifaa vya kujifunzia wala vya kufundishia
6. Maliasini kama madini, gas, magogo na wanyama, tunabadilishana na neti....
7. Serikalini hakusanyi kodi kwa wafanya biashara wakubwa na wawekezaji...mapato ya serikali leo yanategemea mtu kama mimi ninunue kipande cha sabuni nikatwe VAT...
8. Kilimo kwanza kimefeli...hakuna pembejeo, hakuna maafisa ugani....hakuna mbegu bora...
9. Rushwa imeongezeka na Takukuru haijawahi kuwa na meno wala haina meno....
10. Haki mahakamani hakuna, na wala JK hakuna anayemuwajibisha...kila kitu collapsed
11. Bado watu nchi hii wanasafiri siku tatu kutoka ndani ya nchi hiii, MIUNDOMBINU HOVYO...kutoka Moshi hadi Mpanda au Kigoma, almost three days..
12......
13......
14.......

Unapata wapi ujasiri wa kumsifia JK na CCM yake? Kwa lipi jipya linaoonekana? Aliahidi meli mpya ziwa Tanganyika, ziwa Victoria na Ziwa nyasa....hadi sas karibu 1/3 imeisha hakuna hata dalili za kununua meli hata moja...

Lazime uwe na MTINDIO WA UBONGO KUMSIFIA KIKWETE...LABDA UWE MKEWE WA NDOA......

Acha kulalama, hakuna aliyekulazimisha umsifie, isitoshe mimi nachokisema kinatokana na tafakari yangu na kuona Wanasiasa wanavyotaka kuyumbisha nchi kwa kisingizio kuwa ni mihimili iliyoko nchini. yote ulioyaandika hayana tofauti na yanayosemwa na SLAA, MREMA, ZITTO, CHEYO, na wengine wengi na ni haki yao kama wanasiana ili siku ya mwisho nao waweze kuwa na msafara wa magari, kupigiwa mizinga 21 kama niliyoisikia leo kule uwanja wa uhuru, waweze kusafiri kwenda ujerumani, uingereza, Amerika na kwingine huku wakitumia kibwagizo cha uzalendo kwa watu ambao hatujua hata uzalendo ni nini, kibwagizo cha ufisadi huku wakiwa mafisadi wakubwa na kusingizia kuwa utajiri wao ni biashara. Nani amabye hajui kuwa Mkurugenzi mtendaji wa IPP alianza biashara kwa kuuza nyuzi za katani na kalamu za BIC nchini kenya? Mbona hatuambiwi Mwenyekiti wa CHADEMA alianza vipi biashara na kufikia hapo alipo? au kipindi hicho raslimali za Taifa hazikuwepo?
 
HAkika upofu wa viongozi na wanaccm ndo umeifikisha nchi mahala hapa ukiunganisha na unafiki! Hakuna nchi rahisi kuongoza kama Tanzania! Hii nchi rais kikatiba ana mamlaka makubwa mno. Ebu tujikumbushe yafuatayo chini ya utawala wa jk:

1.wizi mkubwa kupitia mkataba feki wa richmond ambapo kila siku matapeli hawa walilipwa Tshs.152,000,000.Hakuna hatua iliyochukuliwa na tumeshuhudia Lowasa analipwa kodi ya watanzania kama w/mkuu mstaafu.

2.wizi mkubwa wa epa ambapo mabillion ya shilingi yalichotwa benki kuu na jk kama kawaida yake akawaomba warudishe. hakuna ushaidi kwamba hiyo pesa ilirudishwa! waliotolewa kama chambo wanajulikana na sababu zinajulikana pengine waliwagusa akina Vick kamata!

3.Msisahau aggreko,iptl, kagoda, meremeta, na mikataba mingine ya kijambazi ambayo imeenderea kushamiri kwenye utawala wa Jk! tulitegemea awakamate wezi waliomtangulia akina Mkapa!

4.wizi mkubwa unaondelea kwenye halmashauri na wizara nyingi. mfano,millioni 400 kukarabati nyumba ya waziri wa afya huku madaktari wakinyimwa mishahara mizuri eti hakuna fedha! na ktumia billion 1.1 kwa maonyesho kwa siku tatu na rais akiwa kimya!

5. matumizi makubwa ya serikali kuliko mapato yakichangiwa na safari nyingi nchi za nje! mfano, zipo tetesi nyingi kwamba safari moja inaweza kuchukua million 400 na akaomba msaada wa vyandarua vya millioni 4!

6.Ahadi alizotoa wakati wa kampeini 2010 ni kipimo tosha kuona aina ya rais tuliyenaye! ili zitimie, anatakiwa atawale si chini ya miaka 30! tujiulize, akielekea kuanza mwaka wa 3 amefanya nini! nauliza tena amefanya nini?

wana jf, mambo ni mengi ila nisiwachoshe cha msingi ukombozi waja. lazima ccm waondoke na kimbunga 2015!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom