Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,420
- 2,271
Labda JK hana kipaji cha kusoma hotuba. Hii inatokea sana.. Kwa mfano Mkapa alikuwa anatumia nguvu nyingi sana alipokuwa akihutubia, wakati Mwinyi mzee wa ruska alikuwa akiipamba sana hutuba zake na kujaza maneno yenye mvuto.. Huku Nyerere akihutubia kwa kuweka vionjo mbalimbali ndani yake.
Hili linatokea sana, unaweza kuwa mahili wa kutunga na kuandika lakini ukawa sio mahili kusimama na kuhutubia kile ulichoandika. Mfano Mwanakijiji anauwezo wa kuandika makala kibao kwa ustadi wa hali ya juu, lakini anapokuja kutangaza kwenye redio yake siku zote hukwama kwama... haya yote hutokea.