Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 77
Dk. Slaa ampinga kuhusu Richmond, Kagoda
na Mwandishi Wetu
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzungumza na wananchi kwa staili mpya ya kujibu maswali ya papo kwa papo kwa njia ya redio na televisheni, wadau mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wameelezea kutoridhishwa kwao na majibu yake, hususan yale yaliyohusu hatua alizodai kuzichukua katika kushughulikia tatizo la ufisadi nchini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, akizungumza na Tanzania Daima katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam jana, alisema Rais Kikwete hakuwa mkweli alipojibu maswali mbalimbali, hasa yale yaliyohusu kampuni tata ya Richmond Development Company LLC na Kagoda, zinazotuhumiwa kwa ufisadi.
Alisema majibu aliyoyatoa kuhusu Richmond, yalionyesha dhahiri jinsi alivyohusika katika mchakato ulioipa ushindi wa zabuni ya kufua umeme wa dharura, bila kujua undani wa kampuni hiyo.
Alisema Rais Kikwete kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, alihusika moja moja ama kwa kukusudia au kwa kuzembea katika mchakato uliosababisha Richmond kupewa zabuni hiyo, kinyume cha taratibu.
Kikwete amekiri mwenyewe kuwa walijadili suala la Richmond na wenzake katika Baraza la Mawaziri, na eti aliagiza Richmond ichunguzwe ili kujiridhisha kama ilikuwapo kweli.
Sasa nataka Watanzania wajiulize wenyewe, rais wao alikuwa wapi hadi Richmond ikapewa kinyemela zabuni ya kuzalisha umeme bila yeye kujua matokeo ya uchunguzi huo aliouagiza? Yaani alisema tu ichunguzeni halafu kampuni ikapewa zabuni kabla yeye kupata matokeo?
Rais wetu hakutimiza wajibu wake, kama kweli aliagiza Richmond ichunguzwe, basi alipaswa kudai ripoti ya uchunguzi huo ili ajiridhishe kama Richmond ilikuwa ni kampuni iliyokuwepo kweli au ilikuwa ni kampuni ya maruhani tu kama alivyoiita mwenyewe jana (juzi). Vinginevyo, kilichotokea ni uzembe, anapaswa kuwajibika.
Sioni sababu kwanini kina Hosea na wengine watakiwe kuwajibishwa kwa uzembe halafu Rais Kikwete mwenyewe asiwajibike.
Rais huyu sijui kama anakumbuka maneno anayoyasema. Kikwete alirudi kutoka katika ziara moja Marekani sikumbuki vizuri ilikuwa ni wakati gani, lakini nafikiri ilikuwa ni Septemba 2006, akasema huko alizungumza na watu wake kuhusu matatizo ya umeme nchini, na akasema sasa tatizo la umeme nchini litakuwa historia. Rais huyo huyo aliyetoa maneno hayo baadaye akaanza kukaa na wenzake katika Baraza la Mawaziri kujadili umeme wa dharura kutoka Richmond. Anapaswa kuwajibika, alisema Dk. Slaa.
Akizungumzia kauli ya rais kuhusu Kampuni ya Kagoda inayotuhumiwa kwa wizi wa fedha zilizokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), Dk. Slaa alisema:
Namshangaa Kikwete anajisifia kwamba watuhumiwa wengine wa EPA wamefikishwa mahakamani, lakini anapoulizwa hawa wa Kagoda ni watu gani, maana wengine anahusishwa nao, anasingizia suala lao lipo kwa DPP (Mwendesha mashitaka wa serikali).
Kwani kesi za hizi kampuni nyingine hazikumhusu DPP? Sisi tuna ushahidi wa mawasiliano ya akina Sanze, Mkapa na Rostam Aziz ya jinsi walivyotoa pesa kutoka Benki Kuu. Sasa kama linaachiwa DPP tu wakati hizi nyingine anajisifia kuwa amezishughulikia yeye, huko ni kukwepa uwajibikaji, alisema Dk. Slaa.
Aidha, Dk. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu, alikosoa hatua ya Rais Kikwete kutumia televisheni ya taifa (TBC) inayoendeshwa kwa kodi za Watanzania wote, kuzungumzia pia masuala yanayokihusu chama chake cha siasa (CCM).
Lingine, haikuwa sawa yeye kutumia kipindi kile cha TBC, inayolipiwa kodi na Watanzania wa vyama vyote na wasio na vyama kuzungumzia propaganda zake za CCM.
Sisi tulitarajia azungumzie masuala ya kiserikali yanayotugusa Watanzania wote bila kujali itikadi zetu, na sio atumie kipindi kile kuanza kupiga kampeni zake za uchaguzi mkuu wa 2010, alisema Dk. Slaa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema suala la nyaraka za kidini linapaswa kushughulikiwa, kwani hadi hivi sasa inawezekana likawa limeshawagawa wananchi wanapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kinyume na alivyosema Rais Kikwete kuwa muda wa kulitatua bado upo.
Akikosoa zaidi majibu ya Rais Kikwete, kwamba serikali inapaswa kutangaza sera ya MPAMITA, yaani Mpango wa Misaada Tanzania kwani majibu hayo yanaonyesha jinsi serikali inavyotegemea sana misaada, ikiwemo misaada ya vyandarua ilhali nchi yetu ina rasilimali za kutosha kuiwezesha kujitegemea.
Nacho Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimeipinga kauli ya Rais Kikwete, kwamba walimu wote wa shule za msingi wamelipwa madai yao na kusisitiza kuwa kauli hiyo haikuwa na ukweli wowote.
Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba, alisema hadi wakati rais anatoa kauli hiyo, walimu wa shule za msingi walikuwa wanaidai serikali kiasi cha sh bilioni 35 na bado wanaendelea kuidai kiasi hicho cha malimbikizo ya mafao yao hadi sasa.
Alisema walimu wamekaa kimya toka walivyotaka kugoma Novemba 17, mwaka jana na kuzuiwa na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, lakini hadi sasa serikali imeshindwa kuonyesha uungwana wa kuwalipa mafao yao.
Alisema rais amedanganywa na watendaji wake kuwa walimu wamelipwa na kutoa kauli kuwa wameshalipwa, kauli ambayo alisema imewashitua walimu wote nchi nzima na sasa chama hicho kinatafakari upya juu ya hatma ya madai hayo ya walimu.
Rais asiridhike na maneno ya kuambiwa na watendaji wake juu ya kulipwa kwa madai ya walimu, hicho ni kitendo cha kuchezea akili za walimu, huku wenyewe wakiendelea kuwa wavumilivu licha ya kutaabika sana, alisema.
Mukoba alimtaka Rais Kikwete kubadili kauli yake hiyo na kukiri mbele ya umma kuwa walimu hao wa shule za msingi hawajalipwa ili wamuelewe.
Pia alikanusha kauli ya Rais Kikwete kwamba madai ya sh bilioni 20 za walimu wa sekondari yanahakikiwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kusema kuwa, kauli hiyo nayo haina ukweli wowote kwani ukweli ni kwamba madai hayo yamefungiwa katika ofisi moja ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Hata hivyo, pamoja na Rais Kikwete kukosolewa kwa majibu yake kadhaa, wananchi mbalimbali wameusifu utaratibu wake mpya wa kuzungumza na wananchi kwa kujibu maswali ya papo kwa papo kwa kutumia simu, ujumbe mfupi wa simu (sms) na barua pepe, kupitia televisheni na redio na kusema kuwa ameonyesha ushujaa wa hali ya juu.
Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti jana, wananchi hao walisema kwa ujumla, Rais Kikwete amebuni kitu adimu ambacho kimempandisha chati.
Rais kaonyesha ushujaa wa hali ya juu, kuzungumza na wananchi kwa stahili hiyo si mchezo, mtu mwingine anaweza kupiga simu na kukutukana, alisema Ayoub Seleman.
Naye Alois Shayo amesema rais amefanya jambo la kihistoria, hivyo hana budi kuifanya stahili hiyo kuwa endelevu hadi ifike hatua watu wakose maswali ya kumuuliza. Amewezesha kuwafanya watu watoe madukuduku waliyonayo mioyoni mwao. Ukiwa rais huwezi kujua yote yanayofanyika, ndiyo maana hata maofisini kunakuwa na vikao ili kuwapa fursa wafanyakazi kutoa kero mbalimbali na mambo mengine, wazo la rais ni zuri, alisema Shayo. Naye Jesca Ngonyani alimsifu Rais Kikwete kwa ujasiri aliouonyesha, hasa katika kujibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na wananchi, zikiwemo nyingine ambazo zilikuwa nzito na kusema amethubutu, hivyo anaamini marais wengine wajao wataweza pia kufanya hivyo.