Jamani wanabodi,
Bila kuona haya napenda kusema kwamba Jakaya hana la maana alilosema na pia hakuna ukweli aliosema. Ametia aibu na kuchekesha. Wakati naangalia TV nilikuwa nacheka kwani hana tofauti na ze comedy original.
Ni jambo la aibu mno kwa Raisi wa nchi kukubali na kujisifia kwamba Tanzania ni omba omba. Bila haya anatueleza jinsi alivyopanga mikakati ya kuzunguka duniani na kuomba omba misaada. Nilitegemea atueleze ni jinsi gani amekuja na mikakati ya kuzalisha ili kuondokana na kuwa omba omba.
Hivi kweli Raisi wa nchi na wapambe wake anapanda ndege mpaka USA kwenda kuomba msaada wa vyandarua milioni 14?. Vitu kama hivi ni kujitia aibu kwani viko ndani ya uwezo wetu. Siwezi kukubali na wala sintakubali kwamba safari za Jakaya zinafaida zaidi kwa Taifa kuliko hasara.
Watanzania wenzangu ukweli tumeula wachuya. JK ni mtupu na wala si utani. Ni uswahili na ujanja ujanja tu wa lugha.
Waalimu wa shule za msingi hawajalipwa mpaka leo, Raisi bila haya anatuambia waalimu wamelipwa. Tumuelewe vipi?.
Kufanya kosa si kosa, bali kurudia kosa ni kosa. 2010 tusifanye makosa ya kuchagua sura. Ni bora kumpata mtu mwenye sura kama Remmy Ongala akawa Raisi, la maana ni kichwa kilichokamilika.