Na haya ndio majibu ya Rais Jakaya Kikwete kwa viongozi wa dini waliompa saa 48 kuwataja viongozi wa dini wanaojihusisha kwa biashara haramu ya dawa za kulevya. Soma, tafakari kisha chukua hatua.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa za Maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kumpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete saa 48 kuwataja kwa majina viongozi wa dini wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya, ni kauli ya kusikitisha na ambayo haikutegemewa kutoka kwa viongozi hao wa dini.
Viongozi wa dini ni watu wa kutumainiwa sana katika jamii yeyote, lakini ikizingatiwa kuwa wao sio malaika ama watakatifu hapa duniani, kwani nao wanatumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa kabisa.
Katika Hotuba yake kwenye sikukuu ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo kuwa Askofu wa Jimbo la Mbinga, Rais Kikwete alitoa ombi ambalo si geni kwani alishalitoa katika hafla zingine pia zilizohusisha viongozi wa dini.
Katika sherehe hiyo Rais alitoa ombi la kuwataka viongozi wa dini wajihusishe kwa ukamilifu katika mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya.
Rais Alisema, "Ni tatizo linalozidi kukua pamoja na jitihada za Serikali kupitia vyombo vya usalama kuwabana, kuwawajibisha watumiaji na wafanyabiashara ya dawa za kulevya. Athari zake kwa jamii zinaeleweka hivyo haihitaji kuzirudia" Rais alieleza, "Hata hivyo niruhusuni niseme tu kwamba tusipofanikiwa kulidhibiti tatizo hili, hasara yake ni kubwa mno. Watoto wetu wengi wataharibika, uhalifu, hasa wa wizi na mauaji utaongezeka. Taifa litaharibikiwa." Amesema Rais na kuendelea kueleza kuwa,
"Siku hizi kila siku kuna watu wanaokamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya. Inaashiria kuimarika kwa vyombo vyetu vya usalama, Lakini inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu. Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana. Nawaomba mtoe uzito unaostahili kwa tatizo hili. Viongozi wa dini mnasikilizwa, Nawaomba kemeeni, onyeni na elimisheni jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya, waelimisheni vijana ambao ndiyo walengwa wakuu, waepuke na waache kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya". Rais alisema.
Kwa maneno haya, tunategemea viongozi wa dini kuchukua onyo hili la Rais kama ishara (Clue) na kuanza kuifanyia kazi.
Mtu akikuonya kuwa nyumbani kwako kumeonekana nyoka, huanzi kwa kuuliza kama kweli, ni wa rangi gani? Unatakiwa kushtuka na kuweka na kujiandaa kumsaka kwa nia ya kumuondosha nyumbani kwako hata ikibidi umuue ili asije akaleta madhara makubwa kwako na kwa familia yako. Rais ana nia njema sana katika kulielezea jambo hili na mwenye nia njema haumbuki.
Hivi karibuni wapo viongozi wa dini wamekamatwa kwa rushwa, ngono na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali ambavyo ni kinyume na maadili yasiyo tegemewa na jamii kwa ujumla, wapo ambao wameshakamatwa na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria, wapo wanaochunguzwa, tumeshawashuhudia na bado wataendelea kushuhudiwa. Hili si jambo dogo la kujitetea kwa kauli nyepesi kutoka kwa watu wanaotegemewa na jamii kwa kumpa Rais saa 48.
Anaejishuku ajisalimishe mwenyewe, anaeshukiwa na jamii afichuliwe ili afanyiwe uchunguzi na hatimaye sheria ichukue mkondo wake lakini msisubiri Rais awataje hadharani ndiyo muanze kuchukua hatua.
Mnategemewa muweke mikakati na vipaumbele vya kufanyia kazi changamoto hiyo, na sio kuaihirisha tatizo hili ambalo linazidi kuwa kubwa. Kazi hii ya kupambana na madawa ya kulevya haimhusu Rais peke yake inamhusu kila Mtanzania, popote alipo katika nafasi yake na viongozi wa dini wananafasi kubwa sana kwa sababu wao wanasikilizwa, wanatoa ushauri na wanategemewa kuwa na maelekezo yanayompendeza Mungu.
Mwisho.
Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
Dar-Es-Salaam.
07 Juni, 2011
nakubaliana na mchangia mada hapo juu, kwani anaonekana kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuchambua mambo, ukweli ni kwamba, suala hili tusijetuka lipotosha mbele ya umma, kwani Rais alichokisema si kuwa baadhi ya maaskofu au baadhi ya mashekhe bali baadhi ya watumishi wa Mungu. hata hivyo si vibaya kwetu sisi kuona si jambo jema sana kwa mtu kama Rais kutoa tamko la ujumla kiasi kile "a such generic statement", inaonekana naye ni sehemu tu ya watu wengi wanao lalamika ili watu wengine waweze kujibu hayo wanayo yaona kuwa hawatendewi haki. kwa Rais hili si sawa kabisa, yeye ana uwezo mkubwa wa ku-identify wale wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na si-kulalamika kama mwanchi wa kawaida tu.......hii inaonesha udhaifu wa hali ya juu ya utendaji wake kwa ujumla.
watu wanahitaji utekelezaji wa sheria bila kuonea watu wa tabaka lolote na si kuwa sawasawa na watu wa vijiweni ambao hukaa na kuzungumza mambo bila kuya fanyia utafiti yakinifu.
Haaa haaa haaa! Angalia usije ukajikuta ni juha baada ya hayo masaa!Kumbe na yeye huwa anaogopa ultimatum, asipindishe ukweli awataje ama sivyo baada ya masaa 48 tumembiwa tumdharau.
Msaidizi mahususi wa Raisi hawezi kusema anayejishuku ajisalimishe....naona kama vile ni kama mipasho flani hivi niliyowahi kusikia kwenye taarabu na akina mama wa mtaani wakisema kama limekukugusa/ukijishuku basi ni wewe!! Nadhani mimi wametumia style hii toka Kwa Hadija Kopa kwani si Mwana CCM pia??mi napata mashaka na utashi wa wasaidizi wa rais!
Lakini, inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata baadhi ya watumishi wa Mungu. Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana. Nawaomba mtoe uzito unaOstahili kwa tatizo hili.
Kwenye red ina maana ni pamoja na maaskofu
hapa ndipo makanisa yanapokuwa na nguvu. ccm ikitishwa kidogo na makanisa yanakuwa taharuki. mbona huwa kimya kwa waislam?
Msaidizi mahususi wa Raisi hawezi kusema anayejishuku ajisalimishe....naona kama vile ni kama mipasho flani hivi niliyowahi kusikia kwenye taarabu na akina mama wa mtaani wakisema kama limekukugusa/ukijishuku basi ni wewe!! Nadhani mimi wametumia style hii toka Kwa Hadija Kopa kwani si Mwana CCM pia??