Kikwete 'awapakazia' viongozi wa dini biashara ya madawa ya kulevya

Amakweli RAIS HUYU AVUNJA REKODI .atasahaulika kwa haya.VIONGOZI WA DINI WANAUZA UNGA . AU alimaanisha unga wa sembe au ngano . kwa maana hiyo WAUMINI NDO WANAONUNUA UNGA NA KUSAMBAZA MTAANI?.mhmm Hii kali ya mwaka .Ngoja tusikie wauza unga watajibu nini
Mkuu mbona ueleweki punguza Rubisi
 
It is time to act. If he is serious, he will dedicate hiyo inteligensia and resources as well kuwafikisha sehemu husika e.g. FFU, police, and helicopters etc . Kiongozi wa nchi haumbui, ana act. Mambo yakuumbuana yanafanywa na viranja mashuleni not leaders at that level!!!.

Tangu Januari Makamba aliyekuwa mmoja wa waandaaji wa hotuba za Kikwete aondoke na kuwa mbunge, hotuba zinazotoka sasa ni utumbo tupu, hazijafanyiwa tathmini ya kutosha kuwa kauli ya mkuu wa nchi. Yamkini ni anahitaji wazee wenye kupitia hotuba zake kabla hajapanda jukwani, vinginevyo tutazidi kufedhehesha taifa tokana na kauli hili za mkuu wa nchi.
 
rais kikwete alisema kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafanya mipango ya kuwatafutia vijana hati za kusafiria kwenda nchi za kufanya biashara hiyo.

kutokana na hali hiyo aliwataka viongozi wa dini kukemea biashara hiyo na kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya dola kuhakikisha biashara hiyo haramu inakomeshwa kwa kuwafichua wahusika wanaofanya biashara hiyo ili wachukuliwe hatua za kisheria.nje

“inasikitisha sana na kutisha biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili, baadhi yenu tumewakamata”, “kauli zenu kemeeni jambo hili kwa kuelimisha jamii hususani vijana waweze kuepuka na matumizi ya dawa ya kulevya,” alisema rais kikwete.

majira

vipi kuhusu prince ridhiwani? Mbona nayeye anauza unga na king hajamuonya? Au mkuki kwa nguluwe?
 
kauli bila kuchukua hatua wahusika n upumbavu ulokubuhu,jk ni mnafiki na mwanamitindo wa kauli.Kimeo hiki kwa ndoto hakijambo pana siku atajuta kuzaliwa tz.mnafiki sana tena hana adabu,umalaya umemzidi anaweza kumweka kimada mwanaume hana aibu huyo jk kimeo mtaalam wa porojo
 
Jamani rais wangu mpendwa JK...you know the dons you have the names..what r u waiting for?!!

Ama kweli katika mapungufu hili ni namba moja..'Nawaasa waliochukua hela warudishe kable sheria haijachukua mkondo wake' haya Kagoda wamerudisha?

JK u r a living JOKE!
 
ulipewa majina ya wauza unga na nguvu zako zote ulizonazo hukuchukua hatua yeyote leo unawaagiza regular citizen wawachukulie hatua wauza unga utaacha lini usanii wako wewe shame on you JK.
 
JUMUIYA ya Kikristo Tanzania (CCT), imempa Rais Jakaya Kikwete saa 48 ikimtaka awataje hadharani viongozi wa madhehebu ya dini aliosema wanahusika na biashara ya kuuza dawa za kulevya na kwamba asipofanya hivyo itakuwa ni aibu kiongozi huyo wa taifa.

Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa alisema hayo jana wakati jumuiya hiyo ilipokuwa ikitoa maazimio ya Mkutano wa 45 wa Halmashauri Kuu ya jumuiya hiyo.Askofu Mokiwa alisema kauli ya Rais Kikwete imewasikitisha kwa kuwa amewahusisha viongozi wote wa dini jambo ambalo si zuri mbele ya jamii.

" Rais ataje majina ni kina nani wanahusika na ndani ya saa 48 awe ameyataja la sivyo itakuwa ni aibu zaidi kwake na serikali," alisema Mokiwa.Alisema wanategemea Rais Kikwete atafanya hivyo na kinyume chake atakuwa hajawatendea haki wananchi.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, juzi kwenye ibada maalumu ya kupewa daraja la Uaskofu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo wa jimbo hilo, Rais Kikwete aliwaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini akiwataka kuacha tabia ya kushiriki biashara ya kuuza dawa za kulevya, badala yake washirikiane na viongozi wa serikali katika kudhibiti biashara hiyo haramu.

Alisema kuwa baadhi ya viongozi hao wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafanyia mipango vijana kuwatafutia hati za kusafiria kwenda nchi za nje kwa ajili hiyo.

“Inasikitisha sana na kutisha. Biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili, baadhi yenu tumewakamata,” alisema.

Msimamo juu ya Katiba Mpya

Akisoma tamko lao baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu wa 45, Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula alisema jumuiya hiyo imeitaka serikali kusimamia kwa umakini suala la Katiba Mpya hasa katika ukusanyaji wa maoni.

Alisema kuwa ukusanywaji huo wa maoni kwa wananchi na makundi yote ya kijamii ni muhimu ukafanywa na chombo huru.

"Kazi hii isiharakishwe na wala isicheleweshwe. Yafaa iwe imekamilika mapema ndani ya muda wa kadri kabla ya kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015," alisema.

Askofu Kitula alisema kuwa serikali inapaswa kuangalia ufa uliopo kati wananchi wa kawaida na wale wenye nacho kwani unazidi kupanuka na kuibua matabaka."Hali hii inasababisha malalamiko miongoni mwa wananchi dhidi ya serikali yetu. Malalamiko na ukweli huu umechukuliwa na wadau wa vyama vya siasa kufanya maandamano ambayo yamekuwa yakiwavutia wananchi wengi."

Alisema hali hiyo inachangia hali ya kisiasa kuwa tete hasa ikilinganishwa na baadhi ya nchi jirani ambako bei ya mafuta iko chini zaidi ya Tanzania na nchi hizo zinapitisha mafata hayo hapa."Serikali isahihishe jambo hili pasipo kuchelewa. Vyama vyote vya siasa vihamasishe wananchi kuleta maendeleo bila kujadi itikadi za vyama vyao."

Askofu Kitula alionya kuhusu siku za ibada na kutaka ziheshimiwe na watu wote na mamlaka zote. Alisema ni vyema serikali isipange matukio muhimu ya kitaifa kama uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa siku za ibada.

"Kadhalika, wahadhiri na wakufunzi wa vyuo vikuu, vya elimu ya juu na taasisi zake wasiwapangie wanafunzi mitihani au mazoezi ya vitendo siku za ibada," alisema Askofu Kitula.

CCT yazungumzia tiba asilia

Kuhusu tiba asilia, CCT imetoa wito kwa serikali kusaidia katika utafiti na matokeo yake yawekwe bayana ili kuwaondolea wananchi hofu ikiwa ni pamoja na huduma zitakazothibitishwa kupatikana mahali pengine nchini.

"Kadhalika, serikali isimamie utunzaji wa mazingira ili miti na mimea mingine yenye vyanzo vya tiba asili istawi na kupatikana muda wote," alisema Askofu Kitula.Aidha, CCT imesisitiza msimamo wake kutaka mambo ya kuendesha shughuli za dini yatenganishwe na mamlaka ya kuendesha nchi.

Kauli ya Rais Kikwete yawakera maaskofu
 
Kwani Raisi kikwete ni Dini Gani? mi naona amefanya hivyo Kwa Interest zake za Kidini,, Kwasababu yeye ni Mbaguzi wa kidini
 
Katoa angalizo tu,lakini kiukweli si kuna wachungaji wamekamatwa na bwimbwi....japokuwa alikuwa amahanishi wa kanisa Katoliki
 
kwani raisi kikwete ni dini gani? Mi naona amefanya hivyo kwa interest zake za kidini,, kwasababu yeye ni mbaguzi wa kidini

hapana hajafanya hivo kwa interest zake bali kwa interest za taifa. Yeye kama kiongozi wa taifa ana source za kumpa taarifa nyingi sana zaidi ya ujuavyo.yeye akipelekewa hupelekewa na majina kwahiyo anaweza kuwaanika au kuwapotezea kwa maslahi zaidi ya kuangalia impact yake after. Waingiza madawa ya kulevya mostly watakuwa wenye pass za kidiplomasia kwani hawakaguliwi na milango yao ya kuingilia ni tofauti na walalahoi. Jk mpaka anataja usidhani hajui anachokitaja. Ila wewe ukilichukulia kama ni suala la kishabiki itakuwa juu yako
 
Kwani Raisi kikwete ni Dini Gani? mi naona amefanya hivyo Kwa Interest zake za Kidini,, Kwasababu yeye ni Mbaguzi wa kidini
acha kabisa mtizamu huo finyu,udin haukubaliki punguza mtizamo hasi,unapofanya hivi unazidi kuchochea udin ambao hata haupo
 
Askofu Mokiwa ame kurupuka na ku overact kwa statment aliyoitoa JK kule Mbinga. Tatizo letu kubwa ni kufanya uchambuzi wa mambo pasipo kuwa na taarifa za uhakika.

Nimeisikiliza ile hotuba tena kupitia radio WAPO na ku transcribe Alichokisema JK ni hiki "

Siku hizi kila siku kuna watu wanaokamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya. Inaashiria kuimarika kwa vyombo vyetu vya usalama. Lakini, inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata baadhi ya watumishi wa Mungu. Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana. Nawaomba mtoe uzito unaOstahili kwa tatizo hili. Viongozi wa dini mnasikilizwa. Nawaomba kemeeni, onyeni na elimisheni jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya. Waelimisheni vijana ambao ndiyo walengwa wakuu, waepuke na waache kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Hiyo text haiongelei JK kasema maaskofu wanauza dawa....imesema baadhi ya WATUMISHI wa mungu. Katika orodha hiyo yawezekana kuwa wapo wachungaji, mashehe na watendaji wengine.

Rais hakurupuki kusema mambo yasiyokuwepo. Hadhara ile haikuwa mahala pa kutaja majina....sio utamaduni kwenye mahubiri ya kanisani mtu kutaja majina.....mbona hata huyo askofu Mokiwa kila siku anahubiri kanisani na kukemea ufisadi, lakini hataji majina ya mafisadi? Je kwa kutokutaja majina ya mafisadi anaowakemea kila mara, ndio maana yake mafisadi hawapo?

Ukweli ni kwamba watumishi wa mungu sio MALAIKA, ni binadamu kama binadamu wengine wote....na wao hupotoka kama binadamu wengine wote.....ndio maana Mwenzi Mungu akaweka provision ya KUTUBU! Ndio maana kila jumapili.....wachungaji wanaongoza sala ya TOBA......THEY ARE NOT EXEMPTED kwenye sala ile ya TOBA......

By the way ukirejea kwenye historia ya dini...... Yesu Mara kadhaaa ame point out kwamba Mafarisayo na viongozi wa dini hawatendi yale wanayohubiri...soma kitabu cha MATHEW 23:
Matthew 23

A Warning Against Hypocrisy

1 Then Jesus said to the crowds and to his disciples: 2 “The teachers of the law and the Pharisees sit in Moses’ seat. 3 So you must be careful to do everything they tell you. But do not do what they do, for they do not practice what they preach. 4 They tie up heavy, cumbersome loads and put them on other people’s shoulders, but they themselves are not willing to lift a finger to move them.
5 “Everything they do is done for people to see: They make their phylacteries[a] wide and the tassels on their garments long; 6 they love the place of honor at banquets and the most important seats in the synagogues; 7 they love to be greeted with respect in the marketplaces and to be called ‘Rabbi’ by others.

8 “But you are not to be called ‘Rabbi,’ for you have one Teacher, and you are all brothers. 9 And do not call anyone on earth ‘father,’ for you have one Father, and he is in heaven. 10 Nor are you to be called instructors, for you have one Instructor, the Messiah. 11 The greatest among you will be your servant. 12 For those who exalt themselves will be humbled, and those who humble themselves will be exalted"

Ukiendelea kusoma hawa viongozi wamekuwa warned 7 times.....Matthew 23 - Passage Lookup - New International Version - BibleGateway.com

Hivyo, Mokiwa hana haja ya kuja juu na kutoa ultimatum. Alichotakiwa kufanya ni kuwahubiria watumishi wa kanisa lake kwamba endapo wao ni sehemu ya wanaojishughulisha na biashara hiyo, basi waache.....kwani ni kinyume na mafundisho ya Mungu.

Lakini tukirudi nyuma....hili suala la kashfa dhidi ya baadhi ya watumishi wa "Mungu" si geni...huko Bolivia Mchungaji mmoja mashuhuri, alikamatwa na kilo 240 za cocaine soma taarifa yake hapo kwenye website:
Pastor Caught Got 240 Kgs Cocaine

A priest of the Aymara Indians, who gave his blessing to the President of Bolivia Evo Morales during his inauguration ceremony four years ago, was arrested for having 240 kilograms of cocaine.

Anti-narcotics police found a cocaine laboratory in the vicarage was named Valentin Mejillones. Besides the pastor, children, and a pair of Colombian citizens were also arrested. Raw cocaine is appraised at a value of about 240,000 U.S. dollars.

The priest says he was framed by the Colombian people. Bolivian Vice President Alvaro Garcia said Morales did not choose it as the pastor who took the presidential oath of office four years ago.

Morales, who is also from Aymara Indian and former farmer of cocaine, was sworn in as the first president to come from local indigenous people. Pastors should preach, not the narcotic involved directly or indirectly.

Similar story imetokea marekani pia....angalia Corapi accuser promised to ‘destroy’ priest after being fired: claim | LifeSiteNews.com

Hata hapa kwetu,wapo wachungaji kadhaaa waliofungwa kwa makosa mbalimbali....likiwemo kosa la kubaka......kumbukeni story iliyowahi kuripotiwa hata hapa jamvini juu ya mchungaji wa KKKT kufungwa miaka 30 kwa kubaka: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/69196-mchungaji-afungwa-miaka-30-jela-kwa-kubaka.html
Hivi mtu mwenye propensity ya kubaka, atashindwa kuuza madawa ya kulevya, akipata opportunity?

ALL IN ALL mimi nadhani badala ya kukurupuka na jazba.....tuli address tatizo kubwa la madawa lililo mbele yetu....soooote ni wadau kwani athari za madawa ni kwa watoto wetu, kaka zetu, ndugu zetu, dada zetu, marafiki zetu na taifa letu kwa ujumla......
 
JK has been concluded to be kimeo so ni aibu kibishana wakati facts zote zinaonesha jk kihiyo
 
Nakubaliana na mchangia mada hapo juu, kwani anaonekana kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuchambua mambo, ukweli ni kwamba, suala hili tusijekuta ilipotoshwa mbele ya umma, kwani Rais alichokisema si kuwa baadhi ya maaskofu au baadhi ya mashekhe bali baadhi ya watumishi wa Mungu.

Hata hivyo si vibaya kwetu sisi kuona si jambo jema sana kwa mtu kama Rais kutoa tamko la ujumla kiasi kile "a such generic statement", inaonekana naye ni sehemu tu ya watu wengi wanao lalamika ili watu wengine waweze kujibu hayo wanayo yaona kuwa hawatendewi haki.

Kwa Rais hili si sawa kabisa, yeye ana uwezo mkubwa wa ku-identify wale wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na si-kulalamika kama mwanchi wa kawaida tu.......hii inaonesha udhaifu wa hali ya juu ya utendaji wake kwa ujumla.

Watu wanahitaji utekelezaji wa sheria bila kuonea watu wa tabaka lolote na si kuwa sawasawa na watu wa vijiweni ambao hukaa na kuzungumza mambo bila kuya fanyia utafiti yakinifu.
 
Na haya ndio majibu ya Rais Jakaya Kikwete kwa viongozi wa dini waliompa saa 48 kuwataja viongozi wa dini wanaojihusisha kwa biashara haramu ya dawa za kulevya. Soma, tafakari kisha chukua hatua.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa za Maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kumpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete saa 48 kuwataja kwa majina viongozi wa dini wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya, ni kauli ya kusikitisha na ambayo haikutegemewa kutoka kwa viongozi hao wa dini.

Viongozi wa dini ni watu wa kutumainiwa sana katika jamii yeyote, lakini ikizingatiwa kuwa wao sio malaika ama watakatifu hapa duniani, kwani nao wanatumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa kabisa.

Katika Hotuba yake kwenye sikukuu ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo kuwa Askofu wa Jimbo la Mbinga, Rais Kikwete alitoa ombi ambalo si geni kwani alishalitoa katika hafla zingine pia zilizohusisha viongozi wa dini.

Katika sherehe hiyo Rais alitoa ombi la kuwataka viongozi wa dini wajihusishe kwa ukamilifu katika mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Rais Alisema, “Ni tatizo linalozidi kukua pamoja na jitihada za Serikali kupitia vyombo vya usalama kuwabana, kuwawajibisha watumiaji na wafanyabiashara ya dawa za kulevya. Athari zake kwa jamii zinaeleweka hivyo haihitaji kuzirudia” Rais alieleza, “Hata hivyo niruhusuni niseme tu kwamba tusipofanikiwa kulidhibiti tatizo hili, hasara yake ni kubwa mno. Watoto wetu wengi wataharibika, uhalifu, hasa wa wizi na mauaji utaongezeka. Taifa litaharibikiwa.” Amesema Rais na kuendelea kueleza kuwa,

“Siku hizi kila siku kuna watu wanaokamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya. Inaashiria kuimarika kwa vyombo vyetu vya usalama, Lakini inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu. Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana. Nawaomba mtoe uzito unaostahili kwa tatizo hili. Viongozi wa dini mnasikilizwa, Nawaomba kemeeni, onyeni na elimisheni jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya, waelimisheni vijana ambao ndiyo walengwa wakuu, waepuke na waache kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya”. Rais alisema.

Kwa maneno haya, tunategemea viongozi wa dini kuchukua onyo hili la Rais kama ishara (Clue) na kuanza kuifanyia kazi.

Mtu akikuonya kuwa nyumbani kwako kumeonekana nyoka, huanzi kwa kuuliza kama kweli, ni wa rangi gani? Unatakiwa kushtuka na kuweka na kujiandaa kumsaka kwa nia ya kumuondosha nyumbani kwako hata ikibidi umuue ili asije akaleta madhara makubwa kwako na kwa familia yako. Rais ana nia njema sana katika kulielezea jambo hili na mwenye nia njema haumbuki.

Hivi karibuni wapo viongozi wa dini wamekamatwa kwa rushwa, ngono na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali ambavyo ni kinyume na maadili yasiyo tegemewa na jamii kwa ujumla, wapo ambao wameshakamatwa na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria, wapo wanaochunguzwa, tumeshawashuhudia na bado wataendelea kushuhudiwa. Hili si jambo dogo la kujitetea kwa kauli nyepesi kutoka kwa watu wanaotegemewa na jamii kwa kumpa Rais saa 48.

Anaejishuku ajisalimishe mwenyewe, anaeshukiwa na jamii afichuliwe ili afanyiwe uchunguzi na hatimaye sheria ichukue mkondo wake lakini msisubiri Rais awataje hadharani ndiyo muanze kuchukua hatua.

Mnategemewa muweke mikakati na vipaumbele vya kufanyia kazi changamoto hiyo, na sio kuaihirisha tatizo hili ambalo linazidi kuwa kubwa. Kazi hii ya kupambana na madawa ya kulevya haimhusu Rais peke yake inamhusu kila Mtanzania, popote alipo katika nafasi yake na viongozi wa dini wananafasi kubwa sana kwa sababu wao wanasikilizwa, wanatoa ushauri na wanategemewa kuwa na maelekezo yanayompendeza Mungu.

Mwisho.

Imetolewa na:

Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
Dar-Es-Salaam.

07 Juni, 2011
 
mbona umeumwa hvyo??
Wewe ni msemaji wa jk au??
Matatzo ya kuropoka yanamponza rais wako.
 
Lakini, inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata baadhi ya watumishi wa Mungu. Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana. Nawaomba mtoe uzito unaOstahili kwa tatizo hili.

Kwenye red ina maana ni pamoja na maaskofu
 
Back
Top Bottom