Kikwete atajivunia nini baada ya kumaliza kipindi cha utawala wake?

Mwalimu nyerere alijivunia utawala bora, Mwinyi alijivunia ruksa, Mkapa alijivunia kuimarisha uchumi, je Kikwete atajivunia nini, tulichambue hili kwa makini wana jf
Ameweza kuruhusu uhuru wa vyombo vya habari kuliko marahisi wote waliomtangulia ndio maana vyombo vya habari binafsi kama jf wanaweza kuandika porojo bila tatizo lolote
 
Rais ambaye ametangaza kuwavua magamba mafisadi na kushindwa kusimamia maamuzi yake, kwa sasa kisha waruka akina Nape. Hiyo yote ni kwa sababu katika listi ya Mafisadi pale Mwembeyanga 2007 JK naye alitajwa. Kama anataka kufanikiwa angeachia Uenyekiti kwanza kwa kuwa yeye ndo GAMBA LA KWANZA na baadaye angeweza kuwaona MAFISADI wengine.

JK siku hizi anamwita Nape "VUVUZELA"; je Nape haoni hata akina Mkama wemeishabadilika: wanasema hakuna maamuzi yaliyopitishwa na NEC kwamba mafisadi watapewa siku 90 wala NEC haikusema waandikiwe barua. Mafisadi wameishamuweka JK sawa kwani wanajuana naye na ndo walimwingiza IKULU 2005.
 
Back
Top Bottom