Kikwete ampokea Ikulu kijana aliyesafiri kutoka Geita kwa baiskeli kwenda kumpongeza!

hongera kijana, hao ndio wakuigwa sio hawa wengine lawama tu mbele
Wakuigwa.... Are you serious.... Yaani machinga, wakulima, wapiga ramri, makahaba, vibaka, wajasiriamali, mahouse girl etc waache kazi zao ili waende kumpongeza mtu... tutafika kweli?, Nchi haijengwi kwa kupongezana bali kwa kuwajibika
 
Mpuuzi tu huyo, hakuna kijana anayeweza kuendesha baiskeli kwa umbali huo akaacha kujichanganya kwenye machimbo mapya ya dhahabu yanayolipa pesa kibao!
 
ila kwa umbali naoujua mini toka geita mpaka dar sio mchezo, tena anadai katumia siku 7 tu kufika dar, amakweli huyu jamaa anampenda rais wake,

what a joke siku saba ...geita - dar....jamani ni mbali...malori yanayopeleka mafuta geita yanatumia siku 3 hadi 4...halafu baiskeli siku 7....tusidanganyane jamani
 
Kwa mara nyingine tena, watanzania ni kusifiana na kupongezana. Huyu kijana angetumia huu muda hata kusoma vitabu si angekuwa amepata cheti? Tunapongezana miaka minne wa tano ni kampeni na kukaa vijiweni kupewa 500 ya chai na kusifiana, maisha yanakwenda
 
Nilipata uchungu sana baada ya kumuona huyo kijana,hv huo muda&energy aliyotumia angetumia kufanya kitu kingine isingekuwa beneficial kwa maisha yake kuliko kutafuta sifa za kijinga! Hata hivyo ujinga wa watanzania ndio mtaji wa JK na ccm yao
 
8E9U2498.JPG

huyu mpiga picha mbona amepiga picha kwa pembeni...hatuoni sura ya kijana ...ili wenzake pale kijijini wamtambue...angempiga kwa mbele..si unajuwa anaweza kupata ile zawadu ta ushujaa ya safari lager...
au wameogopa wangeitoa sura yake vema kina kubenea wangemtafuta wamhoji kama kweli au ni ndie rais tena kashaingizwa mjini na wasaidizi wake...si wanajuwa anapenda sifa na kupendwa!!
 
Hivi kumbe ni rahisi namna hii kutinga Ikulu na kuonana na mheshimiwa rais wa JMT?
 
Huyu Kikwete nae kakosa kazi, tunapongezana mpaka lini? Ipo mmoja kaamua atembee uchi kumuunga mkono, atampokea pia? Majuha wengi
 
sasa walikutana wapi? Maana inaonekana kama ni kitu kimechapangwa na kujulikana, yaani Jk anapatikana kiurahisi hivi na kukutana na mwendesha baiskeli, wote wawili ni njaa tu na wasanii wa kutupwa...jamani kama nchi inasema ina kiongozi mimi naogopa sana....yaani mambo yote ni ya kuigizaigiza....mmmmhhhhhh
 
Wandugu,

Mmeisikia hiyo???? Kuna kijana amesafiri kwa baiskeli kutoka wilayani Geita hadi Ikulu Dar es Salaam kumpongeza mhe. jk kwa kushinda kwa mara nyingine kiti cha urais. ITV wamemwonyesha kijana akiwa anamkabidhi mhe. jk bahasha ya kaki ya A4 sijui ilikuwa na nini ndani yake!!! Vipi wakuu, inaingia akilini hiyo????

Chanzo cha Habari: Taarifa ya Habari ya Saa 2 Usiku.

drama folded
 
Ampe ukuu wa wilaya. Huyu kijana si mzima, ni kitu gani sana ambacho huyo Kikwete kamfanyia binafsi au jamii kilichomfanya aamue kuchukua hatari zote za njiani kuja tuu kumpongeza?Majuha wamejaa
 
Kama kazi ya Rais ingekua inapimwa kwa mambo anayofanya huu muda aliotumia na huyu juha ingeonyesha amepoteza milioni ya pesa
 
8E9U2498.JPG

huyu mpiga picha mbona amepiga picha kwa pembeni...hatuoni sura ya kijana ...ili wenzake pale kijijini wamtambue...angempiga kwa mbele..si unajuwa anaweza kupata ile zawadu ta ushujaa ya safari lager...
au wameogopa wangeitoa sura yake vema kina kubenea wangemtafuta wamhoji kama kweli au ni ndie rais tena kashaingizwa mjini na wasaidizi wake...si wanajuwa anapenda sifa na kupendwa!!

Halafu mbona wako wawili tu> Yaani hata Jk hakuwa na mashabiki au mabodi gads.....if you want to know the real meaning of usanii, just check this...amazing drama
 
Halafu mbona wako wawili tu> Yaani hata Jk hakuwa na mashabiki au mabodi gads.....if you want to know the real meaning of usanii, just check this...amazing drama

Ukiangalia kulia utaona vivuli....I guec ni vivuli vya wapamba na mabodigurd
 
Wandugu,

Mmeisikia hiyo???? Kuna kijana amesafiri kwa baiskeli kutoka wilayani Geita hadi Ikulu Dar es Salaam kumpongeza mhe. jk kwa kushinda kwa mara nyingine kiti cha urais. ITV wamemwonyesha kijana akiwa anamkabidhi mhe. jk bahasha ya kaki ya A4 sijui ilikuwa na nini ndani yake!!! Vipi wakuu, inaingia akilini hiyo????

Chanzo cha Habari: Taarifa ya Habari ya Saa 2 Usiku.
Ni vigumu kuamini ingawa majuha wa namna hii na hata kumzidi hawakosekani. Ni nani anayeweza kutueleza kiwango cha elimu cha kijana masikini anayeonekana kutangaza ujuha wake mbele ya jamii ya watanzania. Nina mashaka kama alihitimu angalau darasa la saba na kama alihitimu darasa hilo au zaidi basi alifanya hivyo kwa kuchakachua maana enzi hizi si ajabu kumkuta kijana "aliyehitimu" elimu hiyo mweupee hata kuandika jina lake kwa ufasaha hawezi!
 
Kalamu daftari umenifurahisha sana eti kijana ni muuza mayai kutoka kitunda. You might be right
 
Uyu kijana akamatwe mara moja kwa kujaribu kuhatarisha maisha yake. Pia,uyo msanii kufika kumsabahi msanii mwenzie ni usanii mtupu! Ivi alibeba sh.ngapi ya spea na chakula na mavazi? Jumla ya ela haipungui elf50 piga ua. Je si angepanda basi? Ivi unajua friction ya barabara,je tairi zilibasti mara ngapi? Uyu kweli msanii,dah!
 
Back
Top Bottom