Kikwete ampokea Ikulu kijana aliyesafiri kutoka Geita kwa baiskeli kwenda kumpongeza!

Kijana kafanya biashara, kwanza kaahidiwa msaada mkubwa wa kuendeleza shughuli zake za kilimo ambapo sidhani kama asingekuja angepata. Vilevile kwa kule kijijini kwake cv imepanda kwa kupiga picha na rais wakiwa wawili ikuru.
 
kwani kaenda Ikulu au kakutana wapi na huyo JK hadi waandishi wa habari wakaida hiyo news? Staki kuamini kumbe hata mimi nikitaka kwenda ikulu naanzisha inshu yangu tu nikifika naruhusiwa kuonana na mkulu. kweli ikulu ni ghetto
 
Anataka nae apate heshima ya kupewa jina la mtaa kama seti Benjamin. Labda atapata hata ukuu wa wilaya si mnajua tena siku hizi vigezo havieleweki wala hakuna chombo cha kuthibitisha uteuzi. Akishasema JK basi, imetoka,
 
kwani kaenda Ikulu au kakutana wapi na huyo JK hadi waandishi wa habari wakaida hiyo news? Staki kuamini kumbe hata mimi nikitaka kwenda ikulu naanzisha inshu yangu tu nikifika naruhusiwa kuonana na mkulu. kweli ikulu ni ghetto
Hapo ndipo unajua usalama wa Taifa unavyofana kazi kwa
Umakini. Kazi tunayo Tanyania
 
Je alipowasili alipimwa afya yake au ndo yale yale ya kuku wa kienyeji?
Hata hivyo ana roho nzuri kwa raisi wake kama si ushabiki!
 
huyu wampitilize moja kwa moja kwenda muhimbili kupima akili. What's productive there???? KAMA UMAARUFU TU ALALE BARABARANI WAKATI WA MSAFARA WA KIKWETE.
 
Siwezi kumpongeza anaonekana ni njaa tu inamsumbua au hana kazi za kufanya huyo!
 
Ni vizuri zipatikane tarehe ambazo ametoka Geita ili iwe ni kitu muhimu, otherwise "disguise labour"
 
Hamna lolote hapo, hiyo ni deal imefanywa ili kumweka Jk juu na ku-boost morale yake baada ya kuchakachua, labda baiskeli kapanda karibu na Dar, lakini mpango ulishafanyika.....huyo wa kulipwa nawaambieni, hatudanganyiki
 
Wandugu,

Mmeisikia hiyo???? Kuna kijana amesafiri kwa baiskeli kutoka wilayani Geita hadi Ikulu Dar es Salaam kumpongeza mhe. jk kwa kushinda kwa mara nyingine kiti cha urais. ITV wamemwonyesha kijana akiwa anamkabidhi mhe. jk bahasha ya kaki ya A4 sijui ilikuwa na nini ndani yake!!! Vipi wakuu, inaingia akilini hiyo????

Chanzo cha Habari: Taarifa ya Habari ya Saa 2 Usiku.


sanaaa hiyo tena ya hadhi ya chini ...tena kwa level ya presidency ni propaganda ya kitoto hiyo.....

unafikiri GEITA hadi DAR ni Mchezo............tena mtu yuko peke yake...
 
Ila kwa umbali naoujua mini toka Geita mpaka Dar Sio mchezo, tena anadai katumia siku 7 tu kufika dar, amakweli huyu jamaa anampenda rais wake,
 
yote hayo ni mapenzi anampenda rais wake jamani kuweni na nyinyi mfano kama huyu jamaa anavyompenda rais wake

siwezi kupongeza kichaa kwa kuvua nguo. Nikifikia hapo natafanya kikao na vichaa wa mirembe kuleeee dom.

Kama anampendea mengine sawa, wafanye kwa siri huko huko.
 
Huu ndo umasikini kwelikweli, badala akae huko kwao aandae majaruba ya mpunga msimu wa kilimo unakaribia ye anakwenda kuwapongeza waloshiba tayari?
 
basi usikute ni muuza mayai katoka kitunda eti wanajifanya geita..unafanya mchezo nini kutoka geita kwa baiskeli..hivi jk utaacha uchekibobu na uongo lini???

i like this ...huyu jamaa ...katoka kitunda .......acheni utani mwana hivi mnajuwa geita,,,ni mbali....yaani ni unatoka geita...sengerema....unavuka mv misungwi..unaingia mwanza...unaitafuta shinyanga ...tabora...singida..dodoma.....moro...[msoga-chalinze]..pwani..dar....its more than 1,200 km....kati kati kuna mapori..wanyama wakali..majambazi..milima na mabonde......
kwanini alipoanza matembezi hatukuambiwa ili watu angalau ...wamuunge mkono huko mabarabarani...na safari hiyo haata iweje ni lazima itumie siku 40 hadi 60..just assuming kila siku alikuwa anatembea kilometa 20 hadi 30...assuming hakuugua au kupata uchomvu uliopitiliza....tuacheni usanii jamani..
 
Back
Top Bottom