Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko

Chama alishaanzisha....KIKWETE alienda london kuikamata pesa yake......

kuhusu ,monduli ni kweli kina waitara na masai sayore walikuwa wanamdharau sana JK kwa wakimuita NANGA......WAITARA ameshawahi kumnasa vibao....

Nyerere alikuwa hapendi unafiki....ukiona taarifa alipelekewa akazi ignore ..watu wa usalama walishampa taarifa kuwa ni majungu na rais wa nchi hawezi kufanyia kazi majungu....
acha uongo
 
Mkwere ndivyo alivyo fatilia anavyomshughulikia Mar Prof Kighoma Malima!
Hili huwezi kusikia ndugu zetu wanalisema. Na huwezi kusikia nani alimchafua salim Ahmed Salim wakati wanagombea. Kuna wakati mambo yanasambaratika sababu ya misingi iliyotumika kuyajenga.
Bado muda hujamaliza kutupa yale tunayopaswa kuyaona. Kimsingi hakuna anayeishi milele. Ipo siku wana mtandao watatuhadithia kinagaubaga nini kilikuwa nini
 
ukumbuke wakati huo tayari alishajiunga na chama cha akina olotu cha nra rafiki na tayari alishanunua nyumba dar ili iwe makao makuu ya hicho chama,hata hivyo adam hakukubaliana na baba yake,juu ya kuhama kwake mimi nilikuwa nikiishinlondon wakati huo,na adam alikuwa rafiki yangu

Kwahiyo hakukuwa na mazingaombwe?
 
Hahaa, mmenikumbusha Nyerere aka mchonga alivokua na majungu ya kufa mtu, wafanyakazi wa serikali wakihesabiwa bia kwenye mabaa hata uwe mratibu kata ukizungusha raundi baa taarifa wanampa Julius.

Kulikua na kipindi cha RTD Kinaitwa mikingamo acha bana mtu akichoma ujue kazi huna mimi kipindi hicho dingi akiwa usalama wa taifa niliona majungu mengi yasio maana ukiwa tajiri eti we mlanguzi,baada sokoine kushupalia issue waka engineer accident.

Nchi ikafiliska kwa aibu akarudi butiama kupalilia mihogo na kunywa breakfast ya mihogo ya kuchemsha kwa sturungi.
Duh!
 
Uzalendo gani kama priority ya uongozi ni kuwanufaisha familia, jamaa na marafiki zako? Huo sio uzalendo. Uongozi unakuwa ni project binafsi ya kuendeleza mambo yasiyo na tija kwa umma wote wa watanzania
Ila ukiangalia vizuri, hakuna ubaya kwa kundi fulani kuwa lenyewe ndilo liwe linatoa viongozi, hasa hawa wakuu wa nchi na viongozi wenye maamuzi...

Kama uongozi huo ungekuwa kama unga ngano ambapo kila aendae dukani anaweza nunua.... Basi kungekuwa na nguvu kubwa zaidi ya kuhangaikia uongozi, na hatimaye ingeleta vurugu zaidi...

So kina Kikwete wala hawakosei, karibu duniani kote mambo yapo hivyo kwenye siasa na uongozi

Kikubwa ni kwamba hili kundi la wachache wanaojirithisha uongozi, linatakiwa liwe na nidhamu na uongozi huo...
 
Hii story authenticity yake haijajulikana vizuri, so let's say all with a grain of salt. Lakini nilishawahi kusikia kwamba Kikwete aliondoka Monduli kwa political intrigue na alikuwa hapatani na "real soldiers". So I am not very surprised to hear these details.

1. Probably hapo kulikuwa na political intrigue and ladder climbing kama motive kwa Kikwete.

2. Hata kama 1. ni kweli, Kikwete alichofanya kilikuwa sawa (as much as I don't like him, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni). Huwezi kuwa na Mkuu wa Chuo anayeuzia Chuo chakula kutoka shamba lake, conflict of interest.

3. Inawezekana kabisa Kikwete karuka escalation points kibao katika food chain. Lakini vipi kama aliona katika mfumo wa jeshi kuna kulindana kwingi na hatua hazitachukuliwa? Vipi kama aliona mtu pekee mwenye uwezo wa kumaliza haya ni Nyerere?

4. Nyerere kwa kusema "nendeni kayamalizeni huko huko" bila hata kutoa msimamo wakati anajua jeshi linaenda kwa kulindana na kumpata whistleblower kama Kikwete ni adimu ali abdicate majukumu kama kiongozi.

5. Nyerere kwa kumsaliti whistleblower Kikwete alikiuka maadili, ni kama alikuwa anataka kulindana kuendelee jeshini halafu Kikwete apatwe na mabaya. Kiongozi gani anafuga migogoro na kuacha jeshi ligubikwe na kulindana? Kwa kusema "Nendeni kayamalizeni huko huko" ina maana alikuwa hajali outcome itakuwaje.

Kama hii story ingekuwa imeandikwa kwa nia ya kumpamba Kikwete ningekuwa na mashaka nayo zaidi, lakini kwa sababu imelenga kumpaka matope Kikwete kama "mnafiki" wakati kwa ukweli ukiangalia utaona ali act kama whistleblower aliyekuwa betrayed, kwangu mimi ni moja ya stories chache sana za Kikwete zinazonionyesha Kikwete katika a positive light.

Labda Kikwete ni kiongozi mbovu sasa kwa sababu alivyokuwa kijana zaidi katika siasa alijaribu kuja na moto wa kupinga ufisadi akaona disappointment tu. Mtu unaenda kuripoti ufisadi kwa rais, rais anakusaliti. Akaona ha, kumbe style yenyewe ndiyo hii, ngoja na mimi niwe fisadi tu kieleweke, maana unaweza kujidai unapinga ufisadi ukauawa bure.

I am just saying.
Noma sana
 
Ila ukiangalia vizuri, hakuna ubaya kwa kundi fulani kuwa lenyewe ndilo liwe linatoa viongozi, hasa hawa wakuu wa nchi na viongozi wenye maamuzi...

Kama uongozi huo ungekuwa kama unga ngano ambapo kila aendae dukani anaweza nunua.... Basi kungekuwa na nguvu kubwa zaidi ya kuhangaikia uongozi, na hatimaye ingeleta vurugu zaidi...

So kina Kikwete wala hawakosei, karibu duniani kote mambo yapo hivyo kwenye siasa na uongozi

Kikubwa ni kwamba hili kundi la wachache wanaojirithisha uongozi, linatakiwa liwe na nidhamu na uongozi huo...

Ungejisikiaje kama Nyerere angeachia madaraka kwa mmoja wa watoto wake? Tuache masihala...uongozi ni kipaji na anayetoa ni Mwenyezi Mungu. Hii ya kulazimisha tuendelee kuongozwea na kundi fulani, hata kama lina watu wasio na uwezo ni kujitafutia bahati mbaya.
Hatutafuti maendeleo ya wote. Tunataka neema binafsi
 
Hata kama leo hii mbowe na wenzake wapate huo uongozi, yanakuwa yaleyale... Ataongoza yeye na genge lake... Na kutakuwa na kurithishana kwa ndugu na marafiki
 
huo mkasa ni kweli ila hakutoka kama ulivyoeleza .. bali mwalimu alituma jasusi mmoja pale monduli kwenda kufatilia mkasa ule na kuchunguza.. riport ilipofika ofisini kwa mwalimu ile ripoti haikukidhi mataraijo ya mwalimu kwa ilikuwa hafifu na duni kwa mwalimu kuchukua hatua...
mwalimu akaamua kutuma jasusi mwingine kwenda monduli na kukaa kwa zaid ya miezi miwili.. na jasusi huyu si mwingine bali Benard Kamilius Membe.. akaenda pale akachunguzaa weee...na katika uchunguzi wake huo alimuhoji pia kikwete (huo nduo mwanzo wa jk kufahamiana na membe).... taarifa iliyorudi kwa mwl ikawa imekidhi matarajio maana moja ya vitu alivyopendekeza membe ni kulitenga jeshi na mambo ya siasa..na hapo ndipo kikwete akaondolewa monduli na kupelekwa kuwa katibu wa chama huko kusini......
 
Hata kama leo hii mbowe na wenzake wapate huo uongozi, yanakuwa yaleyale... Ataongoza yeye na genge lake... Na kutakuwa na kurithishana kwa ndugu na marafiki
Kivip? Sio wote wana akili ndogo..wengine wana akili zinawatosha. Tena wako ndani ya Chama Dola
 
Kipindi hicho mkuu wa chuo alikuwa Gideon Sayore, Kikwete alikuwa ni mmoja wakufunzi wa siasa chuoni hapo.

Sasa ilikuwa hivi:

Mzee Sayore alikuwa anafuga ng'ombe wengi pamoja kufanya shughuli za kilimo kwa wingi wakati huo huo akiwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli.

Hivyo basi baada ya kuona ng'ombe wanatoa maziwa mengi mno na mazao yametapakaa mashambani akaamua kuwa awe analiuzia jeshi mazao kama vile maharage na mahindi pamoja na maziwa na nyama kutoka kwenye mifugo yake na pesa anachukua yeye mwenye mazo.

Aliendelea kufanya hivyo kwa kipindi kirefu tu.. ikiwa ni kama sehemu yake ya maisha.

Sasa bwana kumbe Kikwette (JK) ilikuwa inamuuma sana sana, yaani mno! Sasa haieleweki kama ilikuwa kweli ni kwa uzalendo ua wivu tu akaandika barua kwa Rais kipindi hicho JK Nyerere.

Katika barua hiyo akaandika lawama nyingi mno na majungu mengi sana dhidi ya Sayore, akimwita bepari, bwenyenye, mnyonyaji n.k huku akisema hafai kuwa mkuu wachuo hicho kwa kuwa inavunja miiko ya uongozi na mambo mengine mengi (si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna!)

Basi bwana, akamalizia mwisho kwa kujiandika jina lake na sahihi yake huku akijiita mzalendo kamili barua ikapostiwa ikiwa imeadresiwa kwa Rais wa nchi wakati huo!

Mwalimu, aliipata barua ile aliifungua akaisomaaaa kisha akapiga hesabu zake....sijui aliwaza nini mzee yule, akaihifadhi ile barua ikaa sana ofini kwake bila kuchukua uamuzi wowote.

Siku moja alipokuja mkuu wa majeshi wakati huo "General Mtukula" (David Musuguli) ofisini kwa Mwalimu eaisi kipindi hicho, mwalimu akampa ile barua kutoka kwa Kikwete "akisema hayo ni mambo yenu kayamalizeni hukohuko".

Basi bwana ile barua Mkuu wa majeshi alikaa nayo muda hivi kwenye makabrasha yake. Sasa siku moja alikuja Mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli(Sayore) Dar es salaam kufanya shughuli za kikazi akaenda hadi ofisini kwa Mkuu wa majeshi.

Baada ya shughuli kwisha na Sayore akiwa anajiandaa kwenda Monduli Mkuu wa majeshi alimwita, akampa ile barua ya Kikwete aliyomwandikia Rais!

Sayore akaisoomaaa we akashangaa mno!! Na akafura kwa hasira yule mmasai, akuliza mwalimu kasemaje? Akaambiwa mwalimu kasema yamalizeni wenyewe. Akasema naam, na akaondoka na ile barua hadi Monduli.

Alipofika tu yule mmasai aliitisha kikao cha wakufunzi wote na wakuu wengine pale chuoni, wakati wanajikusanya kwenda kwenye chumba cha mkutano yeye aliamua kwenda kutoa copy ile barua ya Kikwete, kopi nyingi idadi sawa na wajumbe wa mkutano ule.

Alipoingia mkutanoni akawaona wakuu na wakufunzi wote wameketi wakimsubiri wajue alicho waitia, akaanza kwa kuwauliza. Jamani kama kuna mtu ana matatizo, au anaona kuna jambo haliendi sawa anyooshe mkono na saemekinacho mkereketa, watu wote wakawa kimya huku wengine wakisema hamna mkuu akiwemo Kikwete.

Basi bwana, tumalizie mkasa huu

Sayore akaanza kuwagawia zile nakala (copies) za ile barua ya Kikwete kwenda kwa rais akawagawia wooote including Kikwete!!! Huku yule mmasasi Sayore akiwa amefura kwa hasira, macho mekunduuu! Akagonga ngumi juu ya meza kwa hasira na kusema someni hiyo barua!! kisha akatoka na kusema anakuja muda si mrefu.

Hapo Kikwete akajua kifo chake kimefika, akikumbuka macho ya yuile mmasai! akatetemeka macho yakamtoka lip! kwa woga! Na wenzie wakamwanzishia zogo mle ndani.

Alichokifanya ni kuondoka haraka pale kikaoni wenzie wakajua bado yupo chuoni, kumbe safari ya Dar ikawa imeanza...!! Jamaa alitembea uchochoroni kwa muda mrefu sana huku akiogo kabisa kuingia barabara ya kuu.

Mashuhuda wanasema yule bwana akaja kupanda lift ya gari za vyama vya ushirika maeneo ya USA RIVER, hakukumbuka kubeba mzigo wowote! Just imagine kutoka Monduli hadi hapo jamaa aliteseka sana lakini yeye hakujali, cha muhimu ilikuwa kusalimisha maisha yake.

Basi huo ndiyo ukawa mwisho wa JK Monduli, hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!

Hicho ndicho chanzo cha JK kumchukia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadi leo! Yeye humwita mzee Nyrere tu au mwalimu baasi na mara chache akiwa nje ya nchi humwita 'Father of our Nation', lakini ni pale anapotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu.

Ndugu zangu hiki ni kisa cha ukweli kwa 100%, inawezekana uandishi wangu ukawa na upungufu, lakini niemekipata kutoka watu mbalimbali waliowahi kuwa karibu sana na mkasa huu.
Aisee hii noma sana.Ila sishangai watu wa pwani ni wanafiki halafu wana roho mbaya Sana.
 
Dahh
 
No! No! MkamaP,
Usifanye makosa kirahisi Mkuu. Tupo ambao tunamsifu Nyerere kuwa ni Baba wa Taifa ambaye kipindi chake cha kuanza kulikomboa na kiliongoza Taifa hili alipata changa moto kali sana kwa kuwa mfumo wa dunia wakati ule ulikuwa mgumu sana. Halafu nchi haikuwa na wasomi wa kuweza kuendesha nchi. Wakati mwingine wale ambao tunaelewa mambo yalivyokuwa hata kipindi cha miaka ya sabini tu wala si nyuma sana, mambo yalikuwa ovyo sana.

Halafu viongozi waliofuata baada ya Mwalimu ndiyo walitakiwa waendeleze kuliimarisha Taifa. Sasa badala yake wako katika juhudi za kuuza nchi. Kwa kifupi tunawiwa kumwonea huruma baba wa Taifa kuwa alitawala kipindi kilichokuwa kigumu sana, kuangalia wenzetu Afrika wakiteswa na kuuwawa, kubaguiliwa, na kudharauliwa kama wanyama.

Nakuhakikishia hilo lilitosha kumsamehe kabisa Nyerere. Wale waliosaidiwa na wanaofahamu maana ya uhuru leo hii watakuambia kuwa hawatamsahau Nyerere. Sisi hatukupitia kipindi kigumu kupigania uhuru wala hatukumwaga damu na kama ilitokea ni kidogo sana ukilinganisha na majirani zetu.

Viongozi waliofuata ndiyo wanaotakiwa kulaumiwa, maana walipoteza dira ya Taifa letu. Wamechafua muungano na umoja wa Kitaifa ambao Nyerere alijitahidi sana kuuunda. Baadhi yetu huwa bado wanabakia kulaumu sana, wapo wanaosema kuwa hakuwatendea waisalamu haki nk.

Wengine watakumbuka kuwa alituweka katika uhusiano mbaya na baadhi ya nchi kama Nigeria alipounga mkono uasi wa Biafra, wapo watakaomlaumu sana kwa kumpa support Savimbi, uhusiano wetu na Angola utaendelea kuwa mbaya kaisi kwa muda.

Lakini nataka tu uelewe kuwa Baba wa taifa aliliongoza Taifa letu kipindi kigumu sana cha siasa duniani. Kipindi cha vita baridi. Kiliendelea mpaka maraisi walioona kuwa hakuna manufaa kwa upande wowote wakaunda shirikisho la nchi zisizofungamana na upande wowote, lakini hata hilo halikusaidia sana.

Kwani nchi za magharibi zilikuwa na nguvu za kiuchumi na kisayansi waliendelea kutawala tena kwa nguvu na uhakika sana. Nchi moja baada ya nyingine zikawa zinaanguka na kuelekea upande wao. Kuanguka kwa Shirikisho la mataifa ya Kirusi kulihitimisha vita hiyo baridi duniani.

Baada ya jambo hili kila nchi duniani ilichukua mwelekeo wake, including China, ambayo mpaka leo hawajaweza kusema kama ni mfumo wa kibepari au la! Lakini nataka tu nifupishe maneno kuwa Nyerere hakustahili tena kubeba lawama za baada yake maana waliofuata walikuwa na wajibu wa kutafuta kwa haraka na umakini na kugundua wapi taifa lielekee. Utafiti huo ulitakiwa uwe wa kisayansi zaidi. Badala yake ukawa wa kichawi au kishirikina zaidi. Ndiyo maana tuko hapa tulipo.

Ndiyo maana unaanza kuona watu wanasema eti "hata yeye alishindwa". Sasa kama yeye alishindwa ndiyo ina maana na wewe ushindwe? Kwanini sasa uligombea uraisi? Maana anayegombea Uraisi wa nchi anatakiwa awe na lengo jema analotaka kulifanyia Taifa. Siyo tu kwenda pale Ikulu kufanya bishara binafsi kama alivyofanya Mwinyi, Mkapa na wanaoendeleza ufisadi.

Kipindi cha Nyerere mtanzania pamoja na umaskini watu tulikuwa tunajiskia vizuri. Kumbuka lile bango moja kwenye yale mazishi ya watu waliouwawa kwenye maandamano ya Arusha kuwa "Ni Bora kufa shujaa kuliko kuishi kwa aibu" Haya ni maneno mazito sana. Sijui kama viongozi wameyachukilia vipi maneno haya.

Kipindi chake Nyerere kilikuwa na mambo mengi sana yaliyolikumba Taifa, lakini hakukaa kimya mpaka kupelekea wananchi kuchanganyikiwa kwa kutopata majibu. Alikuwa na taratibu za kuhutubia Taifa kila jambo linapotokea na kutoa ufumbuzi na jambo jema sana kwake ni kwamba pale alipokosea alikiri tena wazi wazi au hadharani.

Tukizungumzia maswala ya uchumi, Nyerere was a complete failure. Hilo halina ubishi wala mjadala kabisa. Lakini pamoja na hilo ninakumbuka alipokataa kuanza kuchimba madini aina mbali mbali nchini kwa kuhofia wananchi kutopata faida ya madini ya nchi au ardhi yao. Hili mpaka leo tunaliona.

Viongozi wamefikiri kuwa wanatawala wakati muafaka kuchimba madini yaliyoko kwenye ardhi yetu lakini matokeo yake wawekezaji wanachukua zile almasi na dhahabu sisi wanatuonyesha vipande vya chupa na mabati kuwa ndivyo walivyopata tunabakia kuchekelea kama mazuzu! Hii ni pamoja na mikataba feki iliyokithiri serikalini. Si Mwinyi, si Mkapa na si Kiwete wataweza kukana hilo maana taifa limeendelea kudidimia kiuchumi baada ya kuanza kumilikisha wageni machimbo ya vito mbali mbali nchini.

MSAMEHENI NYERERE KUNA ALIYOKOSEA LAKINI ALILIPENDA TAIFA LAKE KWA MOYO WAKE WOTE NA AMELIFIA TAIFA. MPENI HESHIMA YAKE. HASWA BAADA YA KUONA WALIOMPOKEA WANAVYOBORONGA.

RIP MWALIMU.
Well said
 
Ukitoka chuoni unakatisha Barabara Kutoka Monduli inayopita umbali wa mita tano, mbele ya geti, unapandisha vilima vya Nengungu vinavyoanzia baada ya kukatisha Barabara, unapandisha Kwa Musa Barabara ya zamani inayotoka Arusha kwenda Monduli, ambayo wakati ule ilikuwa haitumiki sana. Unakatisha mashamba ya dengu, unashukia kilima Cha Kisongo, hadi Mnada wa Kisongo. Ni Kilomita 25, Kwa yeye Mjeshi huenda alizitembea tu. Halafu huenda hakufuata Barabara ya Dom-Ars ya kuingiza mjini Arusha au hapo mnadani yawezekana ndipo alipata malori ya ushirika akaenda Kwa Mjomba wa rafiki yake Shimbo huko USA River. Shida Iko Wapi?
Shida ni unafiki wake.
 
Back
Top Bottom