Kikwete alipokea taarifa ya uchunguzi siku 1 baada ya Luhanjo kuamua kumrudisha Jairo

Once more, hopeless Ikulu machinery. Although anyone would acknowledge at the extravagant expenditure of their overly inflated annual budget; everything else by these guys seem useless and hopeless, even propaganda for that matter!!
 
aisee this is Tanzania..hizi movie tunazochezewa hazina tofauti na wale ''the company'' wa kwenye ''prison break''
 
Kwa mujibu wa tbc taifa raisi Kikwete alipokea taarifa ya uchunguzi juu ya Jairo asubuhi ya tarehe 25 na baada ya kuisoma aliamuru Jairo asirudi kazini hadi yeye mwenyewe rais atakapoamua namna muafaka ya kufanya hivo. Taarifa ya ikulu inasisitiza kuwa rais hakushinikizwa na mtu yeyote kuamua Jairo asirudi kazini. Itakumbukwa kuwa Luhanjo alikutana na waandishi asubuhi ya tarehe 24 na kutangaza kumrudisha kazini. Niishie hapo, tu maana nimepata kichefuchefu niliposikia habari hiyo. So ngoja nikatapike kwanza.

hii nchi inatia hasira kila siku
 
Kujichanganya katika kutoa taarifa zote zikitokea sehemu mmoja yaani ikulu ni kidhibitisho tosha kwamba kuna matatizo makubwa kiutawala ndani ya ikulu,kama hizo basic prosedures za kutoa taharifa zinawapiga chenga ,je wanaposafiri nje kufanya mikataba na nchi au makampuni si ndio kutia sahihi hata bila kusoma yalio ndani ya mikataba?
 
Kama ya kweli, nakupa 5 bora. Nikisema kuwa hakuna serikali, nani atabisha? Rais na baraza la mawaziri+makatibu si ndo serikali?

Kwa nini wawe na matamko tofauti wkt wote ni madereva wa merikebu moja? Itoshe tu kwa kusema, hakuna serikali na kama ipo kupingana huku kusababishe mmoja kung'atuka, kwani cdhani kama atafurahi kuona uamuzi wake unasilibwa na bado akawa na nguvu ya kuendelea na utumishi.
 
Hayo ni matokeo ya kawaida kwenye nchi yenye ombwe la uongozi,ufisadi wa kimfumo,ujambazi wa kiserikali,raisi msanii na serikali legelege.
 
Ikulu tumewazoea. Walishakabidhi kwa mkuu wa wilaya asiyehusika sembuse hili? Oooh jamani tukumbushane. Tar 23 luhanjo alimwamuru Jairo arejee kazini siku ya j5 tar 24. Siku hyo ya tar 24 matukio mawili yakafanyika.

1. Bunge kupitia mh.ZITTO Kabwe hoja iliibuliwa. Mh. Olesendeka akaiboresha.

2. Jairo arejea ofisini kwa mbwembwe. Ni siku gani hyo? Tar.24

3.Tar 25 Mbowe anauliza swali kwa mh PM Pinda kwanini Jairo asiende likizo kupisha kamati teule ya bunge kufanya kazi yake? PM anasema tyr mh.Rais amechukua hatua dhidi zake. Sasa je rais alitoa uamuzi kabla Zitto hajatoa hoja?

We are not fool as much as what they think huko Ikulu sawa wanaJF?
 
Kwa mujibu wa tbc taifa raisi Kikwete alipokea taarifa ya uchunguzi juu ya Jairo asubuhi ya tarehe 25 na baada ya kuisoma aliamuru Jairo asirudi kazini hadi yeye mwenyewe rais atakapoamua namna muafaka ya kufanya hivo.

Taarifa ya ikulu inasisitiza kuwa rais hakushinikizwa na mtu yeyote kuamua Jairo asirudi kazini.

Itakumbukwa kuwa Luhanjo alikutana na waandishi asubuhi ya tarehe 24 na kutangaza kumrudisha kazini. Niishie hapo, tu maana nimepata kichefuchefu niliposikia habari hiyo. So ngoja nikatapike kwanza.

Mkuu Pole kwa kupata kichefuchefu ghafla, baada ya kumaliza kutapika tafadhali rudi utuhabarishe zaidi.
 
CAG wetu naye sijui atasafishika vipi hapa, maana kwenye kila uchunguzi wa mizengwe inayoonesha rushwa za waziwazi bila hata ya kutumia darubini, yeye huja na vi-ripoti vyake vya kinafiki vikiwasafisha waovu!!

Ama kweli tunaishi kwenye nchi yenye viongozi wasio na morals, ethics wala uzalendo!!
 
Kawaida huwa siyo mwimbaji lakini taarifa hii naona imekoleza chorus ya KIGEUGEU, KIGEUGEU ... KIGEUGEU ...
Naomba mwenye clip atuwekee hapa ili tusherehekee maamuzi ya ikulu.

Mkuu video nzima ya wimbo huu iliwekwa hapa na mimi niliipakuwa yote. Iliwekwa juzi. Sikumbuki aliyeiweka ila mwekaji alishauri CDM watumie wimbo huu kwenye kampeni za Igunga. Itafute kwenye jukwaa la siasa
 
Ukifikiri sana wanayo ongea na kufanya kazi zao unaweza kujinyonga jambo zito kila mmoja atatoa tamko tafauti kuanzia rais waziri mkuu mpaka waziri ...mfano katiba mpya
 
<b>aisee this is tanzania..hizi movie tunazochezewa hazina tofauti na wale ''the company'' wa kwenye ''prison break''</b>

Wakuu kwa mujbu wa taarifa ya hiyo kurugenzi inaonekana ya kwamba Luhanjo alimpuuza rais. Kwa mantiki hiyo naye angeomba tu ama angelazimishwa kupumzika.

Bunge linasema limepuuzwa na waziri mkuu pia kapuuzwa sasa ikulu nayo inaonyesha rais kumbe naye hakupata taarifa kwa wakati kwa hiyo alipuuzwa.
 
Kuna bahadhi ya maswali tunaweza kujiuliza tusipate majibu, kwa mfano:

CAG alimaliza ukaguzi wiki moja kabla katibu mkuu kiongozi kuitisha mkutano na wanahabari
Katika hiyo wiki nzima katibu mkuu alikuwa amekaa na hiyo ripoti bila kutoa taharifa kwa umma.

Hivi ofisi ya katibu mkuu kiongozi ipo wapi? (kama sio ndani ya ikulu) au ndo nyumba moja lakini hamuonani?
Mheshimiwa rais alikuwa wapi

Nani alimtuma katibu mkuu kiongozi kumpa likizo Jairo?
 
Naweza kukubaliana na taarifa ya ikulu kuwa hawakuwa VIGEUGEU ila hawawezi kuepuka lawama za UGOIGOI.
 
Kwa mujibu wa tbc taifa raisi Kikwete alipokea taarifa ya uchunguzi juu ya Jairo asubuhi ya tarehe 25 na baada ya kuisoma aliamuru Jairo asirudi kazini hadi yeye mwenyewe rais atakapoamua namna muafaka ya kufanya hivo.

Taarifa ya ikulu inasisitiza kuwa rais hakushinikizwa na mtu yeyote kuamua Jairo asirudi kazini. Itakumbukwa kuwa Luhanjo alikutana na waandishi asubuhi ya tarehe 24 na kutangaza kumrudisha kazini. Niishie hapo, tu maana nimepata kichefuchefu niliposikia habari hiyo. So ngoja nikatapike kwanza.

Taarifa ya Luhanjo inaonyesha imeandikwa tarehe (26 Agosti) na ilisomwa kwa mbwembwe mbele ya waandishi wa habari siku ya Jumanne tarehe (23 Agosti) -siku tatu kabla ya kuandikwa (tar 26 Agosti) na inaonesha "Imetolewana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dares Salaam.

Kwa mujibu wa TBC Taifa Rais Kikwete alipokea
taarifa ya uchunguzi juu ya Jairo asubuhi siku ya Alhamisi tarehe (25 Agosti) -(siku mbili baada ya kusomwa na Luhanjo mbele ya Media, na siku moja kabla taarifa hiyo haijaandikwa tar 26 Agosti) na baada ya Rais kuisoma aliamuru Jairo asirudi kazini hadi yeye mwenyewe rais atakapoamua namna muafaka ya kufanya hivyo.

Angalia jinsi overlapping ya tarehe katika sakata hili, Taarifa aloisoma Luhanjo inaonyesha, barua hiyo imeandikwa siku tatu mbele. Nina imani siyo bahati mbaya. Bado kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya uyumbishaji wa tarehe za sakata hili. Kwa kuwa wanajiitaga ni watendaji makini "inawezekana pia kwa uyumbishaji wa hizi tarehe, unaumakini ndani yake, so we need to dig down.

Maswali yangu ambayo hayajajibiwa, aliyemsimamisha Jairo kazi alikuwa ni Luhanjo au Rais???Mwenye mamlaka ya kumrudisha Jairo ni Rais au Luhanjo? Kwa nini Rais apewe taarifa baada ya Luhanjo kuwa ameshafanya maamuzi na kuutangazia umma? Nani yupo juu ya mwingine kati ya Rais na Luhanjo?

Kurugenzi ya Ikulu huwa inatoa tarifa kutoka kwa nani??Rais au Luhanjo??Baada ya Luhanjo kudhihirisha kuwa ndiye anayeongoza Dora, Rais analichukuliaje hilo? Kwa nini Rais asimwajibishe Luhanjo kwa kuvuka mipaka ya kazi yake na kumharibia nchi kwa kufanya kazi kihuni? Kwa kweli maswali ni mengi naomba nisiwachoshe.......

Ndugu zangu kwa namna jambo hili linavyoshughulikiwa, inaonesha dhahiri hapa UONGOZI UMEJAA UBABAISHAJI. na sisi wananchi tunaweza tukawa tunafikiria nchi inaongozwa na Rais aliyepigiwa kura 2010 na kushinda kwa mizengwe, kumbe nchi inaongozwa kihuni na kina Luhanjo et al.

Kama taarifa hii ya ikulu ni sahihi basi maana yake ni kwamba Rais hayupo kabsa!!! Mana angekuwepo likizo wangemconsult.mimi nahisi JK kaacha kuiongoza nchi na uongozi/madaraka kamwachia Luhanjo wakati sisi watanzania tunajua bado Rais yupo madarakani..............

RAI yangu kwa Rais; kwa kuwa wewe ni kiongozi Dhaifu na wa serikali legelege, basi ni bora hiyo nafasi ya mshauri wako mkuu (Katibu Mkuu Kiongozi) uweke mtu mwenye kichwa Kizuri na makini ili afiche udhaifu wako, otherwise there will be endless movies in our country. Usidhani kuwa twafurahia kutumia muda wetu kukushauri namna ya kuongoza nchi badala ya kufanya kazi zetu wakati faida za kuongoza nchi wafaidi mwenyewe.................................................Rais fanya kazi yako/timiza wajibu wako.






 
Nanukuu

"Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliamua kuwa ndugu Jairo asirudi kazini mpaka kwanza yeye rais atakapoamua namna gan ya kurud kazini, lini na wapi."

Kwa hayo maelezo napata maswali mengi

1. Rais aliamua kumsimamisha Jairo, unaweza kuamua kufanya kitu bila sababu ya msing. Hapa kuna mashaka. Kwann ameamua? Hajasema...,

2. Rais atakapoamua kuwa arud vp, hapa rais ametuonyesha kuwa anaandaa mazingira ya kumrudisha. Hajazungumzia kumuwajbsha.
Sioni maana ya kamati ya kumchunguza wakati rais ameshasema mpaka atakapoamua kuwa Jairo arudi vipi?
 
Back
Top Bottom