Andrew Kellei
JF-Expert Member
- Sep 11, 2009
- 348
- 123
Wana JF,kwa wale waliokua wanafuatilia kampeni za JK alipokua Rombo aliwaeleza kuwa Mramba ni panga la zamani lakini makali ni yaleyale(haliishi makali),hii kauli ilichukuliwa na Mgombea wa CHADEMA bwana Selasini kama ni kejeli kwa Warombo kwani akihutubia wakazi wa kilesi bwana Selasini aliwauliza wapiga kura kama kuna yeyote mwenye panga la babu yake nyumbani,katika mahojiano ikaonekana yale mapanga ya zamani(ya mababu)yamenolewa mpaka yameisha na kubaki mpini tu.
Akasema Kikwete amewashangaa warombo kwa kumng'ang'ania Mramba ambaye ni panga la zamani lililokwisha nolewa na kubaki mpini,je rombo hamna mapanga mapya yenye makali zaidi?
Hapo ndipo wapigakura walipoanza kumsikiliza Mramba kwa makini zaidi hasa alipokua anawakejeli kwamba ni afadhali kuzaa mtoto mwizi kuliko kuzaa mjinga(yeye ni mjanja kwa kuwa amefunguliwa kesi ya matumizi mabaya ya ofisi).Akasema kichwa chake ni kizuri na hakuna mrombo atakayeweza kuzaa mtoto awe waziri.