Elections 2010 Marando amlipua Kikwete

Nsaji Mpoki

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
396
65
Marando azilipua helikopta za Kikwete

• Awataja waliozitoa, asema ni mafisadi wakubwa

na Edward Kinabo

amka2.gif
MWANASIASA nguli na muasisi wa mageuzi nchini, Mabere Marando, amezigeukia helikopta mbili kati ya tatu zinazotumiwa na mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, na kuzihusisha na watu wanaokabiliwa tuhuma za ufisadi. Marando mmoja wa wanasiasa wenye kauli kali, alisema watuhumiwa hao wa ufisadi wamezitoa helikopta hizo kwa malengo ya kujihakikishia ulinzi.

Mwanasiasa huyo alitoa matamshi hayo mazito wakati akiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Ubungo, John Mnyika, uliofanyika juzi jioni katika eneo la Makuburi.

Alisema wakati mmiliki wa helikopta moja ni mtuhumiwa wa ufisadi katika kashfa ya EPA, nyingine inamilikiwa na kampuni moja ya nje ya nchi iliyopewa mgodi wa kuchimba dhahabu katika moja ya mikoa ya kanda ya ziwa.

Marando alisema ugunduzi wao huo umewafanya wathibitishe kwamba iwapo atashinda tena muhula mwingine wa urais, Kikwete ataendeleza maslahi ya wawekezaji wa nje na watuhumiwa wa ufisadi jambo ambalo Watanzania hawana budi kuhakikisha halitokei tena.

"Waandishi wa habari mliopo hapa mnisikilize kwa makini. Maofisa usalama fungulieni vinasa sauti vyenu. Marando nasema, helikopta mbili kati ya tatu anazotumia Kikwete hivi sasa, amepewa na mafisadi.

"Helkopta moja imetolewa na fisadi mmoja aliyehusika katika wizi wa fedha za EPA kule Benki Kuu. Huyu bwana tunamjua anafanya shughuli zake Oysterbay hapa Dar es Salaam.

"Helikopta nyingine amepewa na kampuni moja iliyopewa mgodi wenu wa dhahabu kule Shinyanga. Sasa niwaulize, rais wenu kapewa helikopta na wawekezaji ili amnufaishe nani? Awanufaishe Watanzania au mafisadi?" alihoji Marando na umati ukajibu ‘mafisadi', kisha akaongeza:

"Rais wenu mtu wa ajabu sana, anasema anapambana na ufisadi wakati wanaomfadhili ni mafisadi. Kama uongo wabishe…niwaumbue zaidi. Nayasema haya simuogopi mtu, ni ukweli mtupu," alisema Marando na kushangiliwa.

Alisema baada ya kupata uhakika kuwa helikopta mbili zimetolewa na mafisadi, sasa wanaifanyia utafiti helikopta moja iliyosalia kwani wanaamini upo uwezekano mkubwa kuwa nayo imetolewa na watu wa namna hiyo hiyo.

Akiendelea kuchambua Marando alisema hatua ya mkuu huyo wa nchi kuwanadi mgombea ubunge wa jimbo la Rombo, Basil Mramba, aliyefikishwa mahakamani na serikali yake kwa matumizi mabaya ya madaraka na Edward Lowassa wa Monduli aliyehusishwa katika sakata la kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura, Richmond, ni usanii wa waziwazi dhidi ya Watanzania.

"Juzi amekwenda Rombo akasema mchagueni Mramba huyu ni mzuri sana…ni panga la zamani lakini lina makali yaleyale. Akaenda Monduli kwa Lowassa akasema hajaona kama Lowassa. Ndio maana nasema rais wenu...anajifanya anapambana na ufisadi wakati ana ujamaa nao," alisema.

Alisema Watanzania wasibabaishwe na ahadi lukuki zinazotolewa na Kikwete na badala yake waelekeze akili zao zote katika kuchagua rais muadilifu, asiye na urafiki wowote na ufisadi kwani kikwazo kikuu cha maendeleo ya taifa sio ahadi bali ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Aliwataka Watanzania kote nchini kuendelea na dhamira yao ya kuleta mabadiliko na kuhakikisha Oktoba 31 mwaka huu wanamchagua Dk.Willibrod Slaa kuwa rais kwani ni mtu makini, muadilifu na ana rekodi nzuri ya kupigania maslahi ya Watanzania wote kwa miaka mitano mfululizo ambayo alikuwa mbunge wa jimbo la Karatu.

"Ni mtu jasiri asiyeogopa mafisadi, hawezi kuuza dhahabu zenu kwa mafisadi. Hajahongwa helkopta na mafisadi. Helikopta anayotumia Slaa ni mali ya mbunge wetu wa jimbo la Moshi Mjini, Mheshimiwa Philemon Ndesamburo. Sasa niwaulize, mtamchagua Slaa aliyewafichua mafisadi wote pale Mwembeyanga au Kikwete anayepokea helkopta zao?" alihoji Marando na umati ulisikika ukisema, "Slaa."

Alisema ahadi ya kutoa huduma za afya na elimu bure iliyotolewa na Dk. Slaa itatekelezeka kwani taifa litakuwa na rais muadilifu atakayesimamia matumizi mazuri ya kodi za wananchi pamoja na raslimali kama madini.

"Mimi mwenyewe nilisoma bure kuanzia darasa la tatu hadi chuo kikuu, nikapata digrii yangu bure. Nilitibiwa bure wakati wa Mwalimu Nyerere….Mwalimu alikuwa muadilifu na ninyi chagueni mtu muadilifu. Tumesema tutahakikisha taifa linakuwa na hisa ya asilimia hamsini kwenye migodi, sasa hivi wawekezaji wanaoihonga CCM helkopta wanachukua mrahaba wa asilimia 97, nchi inapata kiduchu," alisema Marando.

Akimzungumzia mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Ubungo, John Mnyika, alisema ni kijana mwenye akili nyingi na mwenye uwezo wa ajabu katika kuchambua mambo na kujenga hoja zinazohusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kuwasihi wakazi wa jimbo hilo kumpigia kura na kuzilinda mwaka huu kwani hali halisi inaonyesha kuwa alishinda mwaka 2005 lakini aliibiwa kura.

Alisema ana uhakika kuwa Mnyika atalitikisa Bunge na kuwawakilisha vizuri wakazi wa Ubungo kwani hoja na mikakati yake ya kushughulikia matatizo ya maji, barabara, afya ajira, migogoro ya ardhi na elimu, amezipitia na kuridhika kuwa zinatekelezeka.

"Huwa najiuliza mheshimiwa Mnyika alishindwaje kama haya anayowaambia mwaka huu ndiyo aliyowaambia 2005. Ni hoja nzito zinazotekelezeka, wana wa Ubungo mpelekeni bungeni ….mtajivunia umahiri wa kijana wenu, nina hakika Mnyika atalitikisa Bunge. Anajua mambo mengi sana….ana akili nyingi sana, ana uwezo wa ajabu katika uongozi.

"Mwaka huu msifanye ule mchezo wa 2005 wa kupiga kura na kuondoka. Mkishapiga kura kaeni mbali kidogo mtazame yanayoendelea kituoni hadi mpate matokeo, kisha muende kwenye majumuisho hadi mtangaziwe mbunge wenu," alisema Marando na kushangiliwa.

Kwa upande wake, Mnyika alisema yeye na wagombea udiwani wake katika kata zote 14 za jimbo hilo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanalinda kura mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuweka mawakala watatu waaminifui katika kila kituo kimoja wasiofahamiana watakaolinda kura zao.

"Nilikuwa kamanda mkuu wa kampeni za CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Tarime, kule tulishinda. Mbinu nilizotumia kule ndizo nitakazozitumia Ubungo mwaka huu. Tofauti na uchaguzi uliopita ambapo niliokoteza mawakala wasiowaaminifu wiki ya mwisho, mwaka huu maandalizi ya kupata mawakala makini yalishaanza tangu nilipozindua kampeni zangu.

"Na safari hii tutakuwa na mawakala watatu katika kila kituo watakaolinda kura zetu huku wakiwa hawajuani. Nendeni mkapige kura zenu, tutazilinda," alisema Mnyika na kushangiliwa.
 
biashara inakaribia kuisha yaani hadi sasa hivi tunaangalia mbinu za kulinda kura zetu .
 
Yule Msomali analo hapa la kujibu? Aliingia mitini baada ya kugundulika risiti za ndege ya Salma zilikuwa za kufoji! Nasikia anatafutwa Hong Kong kujibu shitaka la contena la meno ya tembo lililokamatwa huko hivi karibuni.
 
Anahangaika kufoji risiti zinigine kwa ajili ya nyara hizo!!!!
 
Mambo ya ukijua huu, mi najua ule, na ukijua ule, mie nakwenda zangu. I love siasa za kaba nikukabe
 
Is Kikwete that daring! mabobishi yake yote yale na miahadi chungu mbovu jinsi alivyo-committed kwenye anti-ufisade crusade, kweli anathubutu bado kuwatumia ili kupata kiti cha uraisi. Huyu Vipi, is he alright! I bet Mabere anawavuta tu miguu, I do not want to believe any of these!!!!! and if it is true, then TUMEKWISHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
na Edward Kinabo

MWANASIASA nguli na muasisi wa mageuzi nchini, Mabere Marando, amezigeukia helikopta mbili kati ya tatu zinazotumiwa na mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, na kuzihusisha na watu wanaokabiliwa tuhuma za ufisadi.
Marando mmoja wa wanasiasa wenye kauli kali, alisema watuhumiwa hao wa ufisadi wamezitoa helikopta hizo kwa malengo ya kujihakikishia ulinzi.

Mwanasiasa huyo alitoa matamshi hayo mazito wakati akiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Ubungo, John Mnyika, uliofanyika juzi jioni katika eneo la Makuburi.

Alisema wakati mmiliki wa helikopta moja ni mtuhumiwa wa ufisadi katika kashfa ya EPA, nyingine inamilikiwa na kampuni moja ya nje ya nchi iliyopewa mgodi wa kuchimba dhahabu katika moja ya mikoa ya kanda ya ziwa.

Marando alisema ugunduzi wao huo umewafanya wathibitishe kwamba iwapo atashinda tena muhula mwingine wa urais, Kikwete ataendeleza maslahi ya wawekezaji wa nje na watuhumiwa wa ufisadi jambo ambalo Watanzania hawana budi kuhakikisha halitokei tena.

“Waandishi wa habari mliopo hapa mnisikilize kwa makini. Maofisa usalama fungulieni vinasa sauti vyenu. Marando nasema, helikopta mbili kati ya tatu anazotumia Kikwete hivi sasa, amepewa na mafisadi.

“Helkopta moja imetolewa na fisadi mmoja aliyehusika katika wizi wa fedha za EPA kule Benki Kuu. Huyu bwana tunamjua anafanya shughuli zake Oysterbay hapa Dar es Salaam.

“Helikopta nyingine amepewa na kampuni moja iliyopewa mgodi wenu wa dhahabu kule Shinyanga. Sasa niwaulize, rais wenu kapewa helikopta na wawekezaji ili amnufaishe nani? Awanufaishe Watanzania au mafisadi?” alihoji Marando na umati ukajibu ‘mafisadi’, kisha akaongeza:

“Rais wenu mtu wa ajabu sana, anasema anapambana na ufisadi wakati wanaomfadhili ni mafisadi. Kama uongo wabishe…niwaumbue zaidi. Nayasema haya simuogopi mtu, ni ukweli mtupu,” alisema Marando na kushangiliwa.

Alisema baada ya kupata uhakika kuwa helikopta mbili zimetolewa na mafisadi, sasa wanaifanyia utafiti helikopta moja iliyosalia kwani wanaamini upo uwezekano mkubwa kuwa nayo imetolewa na watu wa namna hiyo hiyo.

Akiendelea kuchambua Marando alisema hatua ya mkuu huyo wa nchi kuwanadi mgombea ubunge wa jimbo la Rombo, Basil Mramba, aliyefikishwa mahakamani na serikali yake kwa matumizi mabaya ya madaraka na Edward Lowassa wa Monduli aliyehusishwa katika sakata la kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura, Richmond, ni usanii wa waziwazi dhidi ya Watanzania.

“Juzi amekwenda Rombo akasema mchagueni Mramba huyu ni mzuri sana…ni panga la zamani lakini lina makali yaleyale. Akaenda Monduli kwa Lowassa akasema hajaona kama Lowassa. Ndio maana nasema rais wenu...anajifanya anapambana na ufisadi wakati ana ujamaa nao,” alisema.

Alisema Watanzania wasibabaishwe na ahadi lukuki zinazotolewa na Kikwete na badala yake waelekeze akili zao zote katika kuchagua rais muadilifu, asiye na urafiki wowote na ufisadi kwani kikwazo kikuu cha maendeleo ya taifa sio ahadi bali ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Aliwataka Watanzania kote nchini kuendelea na dhamira yao ya kuleta mabadiliko na kuhakikisha Oktoba 31 mwaka huu wanamchagua Dk.Willibrod Slaa kuwa rais kwani ni mtu makini, muadilifu na ana rekodi nzuri ya kupigania maslahi ya Watanzania wote kwa miaka mitano mfululizo ambayo alikuwa mbunge wa jimbo la Karatu.

“Ni mtu jasiri asiyeogopa mafisadi, hawezi kuuza dhahabu zenu kwa mafisadi. Hajahongwa helkopta na mafisadi. Helikopta anayotumia Slaa ni mali ya mbunge wetu wa jimbo la Moshi Mjini, Mheshimiwa Philemon Ndesamburo. Sasa niwaulize, mtamchagua Slaa aliyewafichua mafisadi wote pale Mwembeyanga au Kikwete anayepokea helkopta zao?” alihoji Marando na umati ulisikika ukisema, “Slaa.”

Alisema ahadi ya kutoa huduma za afya na elimu bure iliyotolewa na Dk. Slaa itatekelezeka kwani taifa litakuwa na rais muadilifu atakayesimamia matumizi mazuri ya kodi za wananchi pamoja na raslimali kama madini.

“Mimi mwenyewe nilisoma bure kuanzia darasa la tatu hadi chuo kikuu, nikapata digrii yangu bure. Nilitibiwa bure wakati wa Mwalimu Nyerere….Mwalimu alikuwa muadilifu na ninyi chagueni mtu muadilifu. Tumesema tutahakikisha taifa linakuwa na hisa ya asilimia hamsini kwenye migodi, sasa hivi wawekezaji wanaoihonga CCM helkopta wanachukua mrahaba wa asilimia 97, nchi inapata kiduchu,” alisema Marando.

Akimzungumzia mgombea ubunge wa chama hicho jimbo la Ubungo, John Mnyika, alisema ni kijana mwenye akili nyingi na mwenye uwezo wa ajabu katika kuchambua mambo na kujenga hoja zinazohusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kuwasihi wakazi wa jimbo hilo kumpigia kura na kuzilinda mwaka huu kwani hali halisi inaonyesha kuwa alishinda mwaka 2005 lakini aliibiwa kura.

Alisema ana uhakika kuwa Mnyika atalitikisa Bunge na kuwawakilisha vizuri wakazi wa Ubungo kwani hoja na mikakati yake ya kushughulikia matatizo ya maji, barabara, afya ajira, migogoro ya ardhi na elimu, amezipitia na kuridhika kuwa zinatekelezeka.

“Huwa najiuliza mheshimiwa Mnyika alishindwaje kama haya anayowaambia mwaka huu ndiyo aliyowaambia 2005. Ni hoja nzito zinazotekelezeka, wana wa Ubungo mpelekeni bungeni ….mtajivunia umahiri wa kijana wenu, nina hakika Mnyika atalitikisa Bunge. Anajua mambo mengi sana….ana akili nyingi sana, ana uwezo wa ajabu katika uongozi.

“Mwaka huu msifanye ule mchezo wa 2005 wa kupiga kura na kuondoka. Mkishapiga kura kaeni mbali kidogo mtazame yanayoendelea kituoni hadi mpate matokeo, kisha muende kwenye majumuisho hadi mtangaziwe mbunge wenu,” alisema Marando na kushangiliwa.

Kwa upande wake, Mnyika alisema yeye na wagombea udiwani wake katika kata zote 14 za jimbo hilo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanalinda kura mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuweka mawakala watatu waaminifui katika kila kituo kimoja wasiofahamiana watakaolinda kura zao.

“Nilikuwa kamanda mkuu wa kampeni za CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Tarime, kule tulishinda. Mbinu nilizotumia kule ndizo nitakazozitumia Ubungo mwaka huu. Tofauti na uchaguzi uliopita ambapo niliokoteza mawakala wasiowaaminifu wiki ya mwisho, mwaka huu maandalizi ya kupata mawakala makini yalishaanza tangu nilipozindua kampeni zangu
“Na safari hii tutakuwa na mawakala watatu katika kila kituo watakaolinda kura zetu huku wakiwa hawajuani. Nendeni mkapige kura zenu, tutazilinda,” alisema Mnyika na kushangiliwa.

Source: Tanzania Daima.
 
Nchi imeuzwa hii jamani!!
Tumepoteza mwelekeo na dira kama alivyosema yule mkuu waliemwekea sumu kwenye kipaza sauti!
 
Hivi hawa chama cha mazuzumagic wanadhani watafanya uovu hadi lini bila kuonekana?
Mwaka huu ni wetu, tuitumie kura yetu kuisambaratisha ccm
 
Hili la wizi wa kura ndo huwa linanilaza macho kila siku nini kifanyike? Hasa katika kura za urais maana safari hii kikwete hatoki, wale watu milioni tano ambao hawakupiga kura uchaguzi uliopita, safari hii wanapiga maana wamehamasika kwamba jk nchi imemshinda.
 
Marando azilipua helikopta za Kikwete

• AWATAJA WALIOZITOA, ASEMA NI MAFISADI WAKUBWA

Inapendeza iwapo wananchi wanaielewa inavyoelezewa na kuifanyia kazi ipasavyvo; READ: VOTE CCM OUT !
 
Huu ujumbe Marando auvikishe pia Mwanza, Tabora, Shinyanga na Mara, Mikoa yenye migodi mikubwa ya dhahabu!!!
 
Back
Top Bottom