Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

Tatizo la wanaJF ni ushabiki na sio reality. Kwanza lazima tutambue kuwa Rais ana haki Kikatiba (ambayo tumeiunda sisi wenyewe) kumteua yeyote kuwa waziri. Vilevile Rais ni binadamu kama binadamu mwingine na si malaika. Hata angemteua mjomba wako bado ungesema yule ambaye si mjomba ni mbaya.

Mimi binafsi nampongeza Mhe. RAIS kwa kutuondolea kero ya mawaziri waliochafuliwa na ripoti ya CAG. Pia kwa kuunda Baraza jipya ambalo binafsi najua litafanya kazi ya Watz.


Waziri asiyekuwa na Wizara maalum.
Kwanza, Hii wizara ilikuwepo siku nyingi
Pili, Prof. Mwandosya ni kichwa kila mtu anajua. Ni watu wachache sana ambao katika mfumo wa elimu hawajasoma (Masters) wakaruhusiwa kusomea (Phd), hivyo serikali inataka kumtumia kwa kazi maalum pale Ikulu kwa maendeleo ya Taifa, wala sio kiraka kama wengi mnavyodhani.

Waziri wa Fedha nimeona CV yake anafaa, Manaibu wake wote wazuri mfano huyu mama Janet anafaa sana tuache umimi na majungu

Waziri wa Ujenzi wote tunamjua

Waziri wa Uchukuzi (Dr. Mwakyembe) wote tunamjua

Waziri wa Africa Masharika wote tunamfahamu

Waziri wa Mambo ya Nje wote tunamfahamu

Waziri wa Makazi wote tunamfahamu


Kwa mtazamo wangu asilimia 80% ya mawaziri ni wazuri tuwaache wafanye kazi tusiwakatishe tamaa na kuwatisha kabla ya kazi.

www,

..tatizo ni JK.

..hata angeteua nobel laureates ktk kila wizara haiwezi kusaidia.

..hapa kwa kweli tusubiri tu mpaka 2015 tupate raisi mwingine.
 
ama kweli!! hii ndio list?ebu nilale tu sasa hii kali ya siasa za tanzania

labda...
 
Mwandosya kwa Wanyakyusa hawaambiwi kitu kwanza wanamtegemea aje kuwa rais kwahiyo wamepima upepo na kuona kuwa Mbeya kutakuwa hakuendeki kwa wana CCM kama wangemwacha kabisa.


Hatujaelezwa kama Prof. Mwandosya ana naibu au la??
 
Inafanana na Chelsea,bila kumfukuza kocha hakuna matokeo ya kueleweka. Mwenye macho haambiwi tazama
 
Huyu ni miongoni mwa wana-magamba waliotumainiwa wakashindwa kuuonja uwaziri wala unaibu waziri.
Pia watanzania wengi wanamchukulia kama Free thinker.

Je tuamini kuwa hakufaa ama ni adhabu ya kiherehere chake cha kutia saini..
 
Ha ha,ha..tusubiri kesho..,CCM namkubali tu Deofilikunjombe hana unafiki kama huyu daktari mwenye jina la bandia,ni mnafiki kwa sababu hata kwenye mgomo wa madaktari baadae aligeuka,,,hafai huyu hata kuwa balozi wa nyumba kumi,wananzega wamechemka
Usinikumbushe pia pale muchs enzi zile
 
Salam wakuu!
Ni muda sasa,nimekuwa nikijiuliza maswali mengi pasipo na majibu,kuhusu mama
huyo kwa jina la Sophia Simba,je ni nani hasa?kwa kuwa tokea nimeanza
kumfuatilia enzi zile kabla hajawa mbunge,wala nini,ni maajabu kuwa waziri!
Nasema ivyo kwa kuwa hata alipopewa uwaziri tokea mwanzoni,hakuna
cha ajabu alichokifanya cha kuweza kuigiwa mfano,amekuwa akihamishwa
hapa na pale au kubakizwa huku wale watendaji wazuri kushinda yeye.wa
kiachwa!yeye anatunda tu tena kwa tambo kubwa sana,who is she?
Pengine kuna wadau wanaweza wakanifahamisha utendaji wake,ili pengine
mimi nipate kuondoa fikra potofu,ikumbukwe hata alipoingia chama cha wanawake wa CCM na kuwa
mwenyekiti alianzisha mtafaruku kwa staili ya kusutana na watendaji wake
alioona wanaleta kilomolomo na kweli kwa ubabe wake mmojawapo akatolewa!
jeuri alionayo kwamba hata kama si mtendaji makini atabaki,anaitoa wapi amba
yo wengine hawathubutu kuwa nayo?
So who is Sophia Simba by the way for the Development of our Nation?
Please help me to know her better,maybe im wrong!
 
Pamoja na kuwa Baraza la Mawaziri ni kubwa sana likiwa na jumla ya mawaziri 55, bado isingewezekana kila mtu wa CCM awe waziri, hata kama kuna waliotegemewa wawemo lakini hawakupeta. Watu kama January walikuwa na uhakika wa kuwamo kutokana na ahadai za siku nyingi alizokuwa ameahidiwa siku nyingi sana hadi baba yake akatamba kuwa mtoto wake huyo ataukwaa uwaziri, ingawa baadaye Kikwete aliamua kumchelewesha kidogo.
 
Salam wakuu!
Ni muda sasa,nimekuwa nikijiuliza maswali mengi pasipo na majibu,kuhusu mama
huyo kwa jina la Sophia Simba,je ni nani hasa?kwa kuwa tokea nimeanza
kumfuatilia enzi zile kabla hajawa mbunge,wala nini,ni maajabu kuwa waziri!
Nasema ivyo kwa kuwa hata alipopewa uwaziri tokea mwanzoni,hakuna
cha ajabu alichokifanya cha kuweza kuigiwa mfano,amekuwa akihamishwa
hapa na pale au kubakizwa huku wale watendaji wazuri kushinda yeye.wa
kiachwa!yeye anatunda tu tena kwa tambo kubwa sana,who is she?
Pengine kuna wadau wanaweza wakanifahamisha utendaji wake,ili pengine
mimi nipate kuondoa fikra potofu,ikumbukwe hata alipoingia chama cha wanawake wa CCM na kuwa
mwenyekiti alianzisha mtafaruku kwa staili ya kusutana na watendaji wake
alioona wanaleta kilomolomo na kweli kwa ubabe wake mmojawapo akatolewa!
jeuri alionayo kwamba hata kama si mtendaji makini atabaki,anaitoa wapi amba
yo wengine hawathubutu kuwa nayo?
So who is Sophia Simba by the way for the Development of our Nation?
Please help me to know her better,maybe im wrong!
Ni mama mropokokaji sana. Anapewa cheo kwa sifa hiyo na labda zingine azijuazo mkulu.she's just goood for nothing. Si unamjua JK kwa kulipa fadhili kwa gharama za nchi?
 
Kakojoe ulale usiku wote huu unauliza maswali!!
Nipo serious bwana!naomba unijibu mana kuna wakati nikifikilia sana
kuhusu yeye huwa machozi yananitoka!
wanaachwa watu zaidi yake kiutendaji,kwa nini tunafanyiwa ivyo?kwa
maslai ya nani hsa jamani?inatia uchungu sana.
Mungu tusaidie.
 
Jamani hili baraza ni jipya kweli au wameamua tu kubadilisha jina? afu huyu waziri asiye na wizara maaalumu ndo sijaelewa kabisaaaaa,,sasa atakuwa na tofauti gani na waziri mkuu? msaada tutani wadau
 
Kama watoto ni wezi kwenye familia tukuwafukuza jeri ni baba yao na baba hajui kama wanae ni wadokozi mpaka aambiwe na majirani basi kosa si la watoto pekee na baba, kama si mwizi ni zoba itakuwaje, hutaki kujua mienendo yao... Hili ndo kwa Kikwete na baraza lake jipya la mawaziri kila mda anapanga baraza la mawaziri ambao utendaji mdogo na hafifu halioni hilo mpaka CDM waone naye afanye, mi naona kikwete ndo mweye tatizo, kampeni zake 2005 aliahidi kumaliza tatizo la umeme lkn mpaka leo kazi kwenda misibani, alafu anasingizia waziri wa nishati acha nchi mzee.
 
kiongozi hana jipya jk.
hawa ghasi,malima makamba,kombani na kigoda aliyetupeleka kwenye mikataba mibovu ya madini anamrudisha..kero yangu kubwa hawa ghasia jamani huu ni kihiyo na kibonde tutapoteza fedha nyingi huko tamsemi.
nilifurahi sana pale aliposema wenzetu watakao chukua jukumu hili.kimaoni jk ameshaona vijana wa kaki(CHADEMA) WANACHUKUA NCHI 2015.....

wazuri sana wakukosoa mlio wengi hata kuratibu mambo yenu binafsi huwa hamuwezi,punguzeni siasa wa tz fanyeni kazi!
 
Nauliza mmetumwa?????!!!!!!

Kwa nini hasa, nyingi ya thread zinazungumzia baraza jipya....nilidhani baraza jipya ni kama kungekuwa na kuvunjwa kwa baraza na kuundwa upya na si hii reshuffling iliyofanyika...au mimi sielewi maana ya baraza jipya na nyinyi advocates wa baraza jipya ndiyo waelewa zaidi???

Au mmetumwa?????? if YES basi kawaambieni waliowatuma kuwa, hamkukuta mtu kwa hiyo the message was not delivered!!!!

and if NO...nna mashaka kama mlifanya vizuri mtihani wa kiswahili, kwa hilo sina la kuwafanya...sorry for you!!!
 
ni jipya ila sura ni zilezile na watendaji ni walewale kwa hiyo matokeo ni yaleyale! Kwani mwenyewe anataka tuiteje? Si jipya? Kwani nyie hamfahamu mchezo wa karata tatu na bingwa wa kuucheza? Hana pool nyingine mwenzenu! Walobaki wote maadui. Kama hamuamini mwambieni zitto akomae na hoja yake muone atakavyobadili, sanasana atamwongeza mbatia na wale wenzetu wa baharini. Wabongo lazima mkubali mlifanya makosa makubwa kuchagua baby face...mpaka 2015 tena hivyo! Mbinyo wa kiuchumi palepale, inflation itakuwa imefikia asilimia 3000, subirini myaone ya Zimbabwe hivi karibuni! Mimi si tu kwamba sioni cha kumpongeza, lakini pia sioni cha kumlaumu. Ameshafanya, amepoteza confidence na mpaka waliomchagua-kama aliwahi kuchaguliwa...hana jipya!
 
Back
Top Bottom