Kikwete afanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri - Aprili 2012

Wee vipi??????????????? Hili jembe limesepeshwje? Lipo linadunda labda kama wewe mwenyewe ndo umesepeshwa. M,wanry yupo ndani ya baraza au umesoma na kusikiliza between the line?
 
Tatizo la wanaJF ni ushabiki na sio reality. Kwanza lazima tutambue kuwa Rais ana haki Kikatiba (ambayo tumeiunda sisi wenyewe) kumteua yeyote kuwa waziri. Vilevile Rais ni binadamu kama binadamu mwingine na si malaika. Hata angemteua mjomba wako bado ungesema yule ambaye si mjomba ni mbaya.

Mimi binafsi nampongeza Mhe. RAIS kwa kutuondolea kero ya mawaziri waliochafuliwa na ripoti ya CAG. Pia kwa kuunda Baraza jipya ambalo binafsi najua litafanya kazi ya Watz.


Waziri asiyekuwa na Wizara maalum.
Kwanza, Hii wizara ilikuwepo siku nyingi
Pili, Prof. Mwandosya ni kichwa kila mtu anajua. Ni watu wachache sana ambao katika mfumo wa elimu hawajasoma (Masters) wakaruhusiwa kusomea (Phd), hivyo serikali inataka kumtumia kwa kazi maalum pale Ikulu kwa maendeleo ya Taifa, wala sio kiraka kama wengi mnavyodhani.

Waziri wa Fedha nimeona CV yake anafaa, Manaibu wake wote wazuri mfano huyu mama Janet anafaa sana tuache umimi na majungu

Waziri wa Ujenzi wote tunamjua

Waziri wa Uchukuzi (Dr. Mwakyembe) wote tunamjua

Waziri wa Africa Masharika wote tunamfahamu

Waziri wa Mambo ya Nje wote tunamfahamu

Waziri wa Makazi wote tunamfahamu


Kwa mtazamo wangu asilimia 80% ya mawaziri ni wazuri tuwaache wafanye kazi tusiwakatishe tamaa na kuwatisha kabla ya kazi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,


Huyu mheshimiwa tangu nimeanza kusikia jina lake sijawahi kusikia kitu alichofanya, labda kubadilishwa wizara kila baada ya siku chache tu!
 
Ni kweli uachosema hila naamini kumfumania mkeo hakumaanishi ulipomchagua ulikuwa mjinga na kumaanisha mjinga.Jiulize kwenu nyote mnafana? Kipindi chako chote wakati unasoma hukutumia vibaya mali za familia? au ya kwetu tunayasahau?
Kila mmoja wetu aweke kioo ndani ya roho yake ajiangalie ktk ngazi aliyo nayo ni msafi kiasi gani alfu peleka shmbulio kwao. Kama unatamani kupata kazi nzuri siyo ili upate nafasi ya kuiba kama wengine na si kutumika jisafishe. Waache wajaribu mbovu ni mbovu hata umtoe ccm umweke chadema atabaki mbovu. Naamini ktk mtu na si watu.Matusi hayatojenga taifa tufanye supportive and constructive ideas. NI MAONI YANGU SIIJUI SIASA MI NI MWANASAYANSI. Kama uongo uanasiasa sifa yake ni uongo. Nawachukia nyie wanasiasa na wanasheria mnageuza + iwe-
 
Hahaha...kweli Mwanzisha uzi amekurupuka. Nimemsikiliza JK Mwanzo mwisho sikulisikia jina la mwanri. Kama kweli yupo kesho nitakwenda kwa daktari wa Masikio.
 
Hivi mwari anakuwaje chini ya hawa ghasia!!
Kwani hata wakati akiwa na mkuchika alikuwa anamfunika! Jk ana vituko! Unamwonea sana huyu mama ana nini mbona Jk anambeba sana?
 
Hahaha...kweli Mwanzisha uzi amekurupuka. Nimemsikiliza JK Mwanzo mwisho sikulisikia jina la mwanri. Kama kweli yupo kesho nitakwenda kwa daktari wa Masikio.

Kama ulisikiliza kwa makini na hukusikia inabidi uanze kujiandaa sasa hivi kwenda kwa daktari!!!!
 
Mwanri anaendelea na wadhifa wake kama Naibu waziri TAMISEMI. Ila kwa sasa atakuwa chini ya Hawa Ghasia! (Mwanri chini ya Hawa Ghasia) kweli dunia imejaa vituko!

Mimi nilidhani Angalau angepewa uwaziri kamili Huyu jamaa...kumbe bado hajapata admiration ya JK .....inabidi aendelee kupiga kelele zake chini ya Hawa Ghasia
 
Mimi nilidhani Angalau angepewa uwaziri kamili Huyu jamaa...kumbe bado hajapata admiration ya JK .....inabidi aendelee kupiga kelele zake chini ya Hawa Ghasia

I can imagine bajaj kutangulia mbele ya Rav 4 tena kwenye single lane. Siasa kweli si hasa
 
Back
Top Bottom