Elections 2010 Kikwete aapa kwa kutumia katiba

emt, soma sura ya 266 sheria za nchi (The Official Oaths Act) ndiyo imeanisha kiapo cha rais na maafisa wengine was serikali.
 
JK hawezi kuapa kwa kutumia Quruan yake ya Kiislamu hata wanasiasa wengi walio Wakristo hawawezi kuthubutu kutumia Biblia.
Kama wapo ni minority few! You know what?
Wengi ya wanasiasa si wakweli wala waaminifu KWASABABU WENGI WAO WANAINGIA KWA KURA ZA WIZI NA UDIKTETA.
Kwa hiyo they are clever enough to know that once they touch those SACRED BOOKS, surely they gonna be punished by the Author of those Books Who is GOD Himself!!!

Hivi wewe unategemea Kikwete ashike msahafu wakti DHAMIRA YAKE INAMSUTA KUWA KAINGIA MADARAKANI KWA KURA ZA WIZI??Hawezi.
Mungu anajua mioyo ya Watu kwa hiyo hawawezi kutumia Biblia or Kuruani.

NI DR.SLAA PEKE YAKE ANGELIWEZA KUAPA KWA KUTUMIA BIBLIA KWASABABU NI MCHA MUNGU!!!!.

Wanasiasa wengi wanashiriki mambo ya nguvu za giza so ni wachache sana wanaoweza kuapa kwa kutumia sacred books!
 
Utamchanganyaje shehe Yahya na Mungu. Issue hapa ni kuwa Mtu anaapa mbele ya Mungu (Quran au Biblia) kuwa ataheshimu katiba. kwa hiyo kwa kutotumia Quran hakuna kiapo hapo!
 
Yule hajui hiloo dini ameichakachua pia...maana kama kweli aliapa kwa dini akakumbatia mafisadi na kudanganya wa tz wote sio mshika dini.....
 
Nisaidieni!!
Ukisoma thread kama hii, utagundua wazi kabisa kampeni za mwaka huu ziligubigwa na udini wa hali ya juu kuliko uhalisia. Hili lililopandwa uchaguzi huu, litakuwa tayari kuvunwa uchaguzi zijazo. Wapo watu wameathirika na hili na kuiweka CHADEMA hasa kwenye wakati mgumu wa kujinasua na tuhuma za dini.
Ukweli ni kwamba wale wanaojiita ndio wasomi (maana wengi wanaaccess na internet), wao ndio chanzo cha vurugu zoote. Wanapandikiza chuki mitaani lakini kwenye vurugu wao hawaonekani. Kwa ujumla ni TABIA MBAYA SAANA. Lazima tuanze kubadilika sasa, vinginevyo waliojeruhiwa kwa kampeni za nyumba za IBADA wataamua na wao kulipa kisasi na hapo usalama hautakuwepo tena. Tumemaliza uchaguzi huu 2010 lakini hali ni tete zaidi 2015 km tutaendelea kuamini kuwa mahitaji ya Watanzania ni dini zao na si maendeleo.
 
umesema kweli mzee kuwa dhamira zao lazima zinawapinga:doh:
JK hawezi kuapa kwa kutumia Quruan yake ya Kiislamu hata wanasiasa wengi walio Wakristo hawawezi kuthubutu kutumia Biblia.
Kama wapo ni minority few! You know what?
Wengi ya wanasiasa si wakweli wala waaminifu KWASABABU WENGI WAO WANAINGIA KWA KURA ZA WIZI NA UDIKTETA.
Kwa hiyo they are clever enough to know that once they touch those SACRED BOOKS, surely they gonna be punished by the Author of those Books Who is GOD Himself!!!

Hivi wewe unategemea Kikwete ashike msahafu wakti DHAMIRA YAKE INAMSUTA KUWA KAINGIA MADARAKANI KWA KURA ZA WIZI??Hawezi.
Mungu anajua mioyo ya Watu kwa hiyo hawawezi kutumia Biblia or Kuruani.

NI DR.SLAA PEKE YAKE ANGELIWEZA KUAPA KWA KUTUMIA BIBLIA KWASABABU NI MCHA MUNGU!!!!.
 
Ukisoma thread kama hii, utagundua wazi kabisa kampeni za mwaka huu ziligubigwa na udini wa hali ya juu kuliko uhalisia. Hili lililopandwa uchaguzi huu, litakuwa tayari kuvunwa uchaguzi zijazo. Wapo watu wameathirika na hili na kuiweka CHADEMA hasa kwenye wakati mgumu wa kujinasua na tuhuma za dini.
Ukweli ni kwamba wale wanaojiita ndio wasomi (maana wengi wanaaccess na internet), wao ndio chanzo cha vurugu zoote. Wanapandikiza chuki mitaani lakini kwenye vurugu wao hawaonekani. Kwa ujumla ni TABIA MBAYA SAANA. Lazima tuanze kubadilika sasa, vinginevyo waliojeruhiwa kwa kampeni za nyumba za IBADA wataamua na wao kulipa kisasi na hapo usalama hautakuwepo tena. Tumemaliza uchaguzi huu 2010 lakini hali ni tete zaidi 2015 km tutaendelea kuamini kuwa mahitaji ya Watanzania ni dini zao na si maendeleo.

Nime msikia Zitto Kabwe Akiongea na idhaa ya kiswahili ya Ujerumani ,amekiri ya kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulitawaliwa sana na udini,hata kwenye mitandao ya internat kulikuwa na ushabiki sana wa kidini,sasa sijui alikuwa ana kusidia mitandao ipi!
 
Nime msikia Zitto Kabwe Akiongea na idhaa ya kiswahili ya Ujerumani ,amekiri ya kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulitawaliwa sana na udini,hata kwenye mitandao ya internat kulikuwa na ushabiki sana wa kidini,sasa sijui alikuwa ana kusidia mitandao ipi!
Unauliza mitandao ipi? Kwani ulikuwa hupiti JF na ukaona nini kinaendelea? Na mpaka sasa huoni watu wanaandika nini? Kwakifupi, CCM itaendelea kuonekana bora kama kampeni zitakazokuwa zinapigwa zinakuwa zipo kidini. Kwa maana nyingine tusitarajie maendeleo kwa kampeni za aina hii. Wengi kati yetu hatujawahi kufika sehem zenye machafuko zaidi ya kusikia. Pia credibility ya JF inaondoka kama watu wataanza kujadili utendaji au ufanisi kwa kuzingatia dini ya mtu badala ya uwezo wa muhusika.
 
Kuapa kwa kutumia vitabu vya dini kunataka usafi wa moyo...ni rahisi kuchakachua wanadamu wenzako lakini kuthubutu kuuchakachua hadi uwepo wa muumba yataka moyo!!!
 
Kikwete ana haki ya kuapa kwa kutumia katiba au Kurani au hata Biblia. Ila naomba niwakumbushe kuwa hata Marekani ambapo kuna wale wasioamini Mungu (atheist) mara nyingi huwa wanapenda kuficha imani hiyo na huapa kwa kutumia kitabu cha dini. Hii ni muhimu kwani unaonekana kuwa umekula kiapo kweli kwani unawaahidi wananchi wako mbele ya Mungu wako unayemwamini, unayemwabudu na unayemwogopa kuwa atakuhukumu siku ya mwisho - kuwa utalinda katiba ya nchi. Sasa kwa nchi conservative kama Tanzania kutotumia kitabu cha dini kuapa ni sawa na kuwa hujaapa.
Mi nadhani kwa case ya Kikwete hii ni ishu kubwa zaidi ya kuwa tunavyofikiri kwani ina maana:
1. Hamwamini Mungu - hivyo wale waislamu ambao walimpigia kura kwa sababu ya dini kawadanganya na kuwapotosha
2. Hakuapa kweli - ameogopa kutoa kiapo ya kweli maana anaogopa laana ya Mungu, hivyo hatalinda katiba
3. Alitaka kuonekana siyo mdini - yaani yeye atawatetea watu wa imani zote, ila hii ni very weak excuse kwani hata kama Muislamu au Mkristo anaweza kulinda haki za wote.
 
Huu ni mfululizo wa ukiukwaji wa kanuni, taratibu na sheria za nchi. Inabidi aelezwe ukweli kuwa amechemsha hata kama kuna jambo alikuwa anajaribu kuliepuka. Tusipofanya hivi tutaona mengi.................
 
Sio Rais wa Tanzania kwa kuwa hakuapa kwa unyoofu wa Moyo kwa kitabu cha imani yake
 
Kikwete aapishwa rasmi
dudkikwete.jpg
Rais Jakaya Kiwete akiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania General Mwamunyange

Rais Jakaya Kiwete ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwashinda wapinzani wake kwa asilimia 61 za kura zote zilizopigwa.
Akitoa hotuba mara baada ya kuapishwa alisema kuwa kipao mbele chake kwa hivi sasa ni kuhakikisha kuwa wanajenga umoja wa kitaifa na kurudisha amani iliyokuwepo awali kwani anaamini kuwa uchaguzi uliweza kuwagawa watanzania kwa namna moja ama nyingine
Alisema mchakato wa jinsi serikali yake itakavyofanya kazi ataitoa hivi karibuni wakati akilihutubia Bunge jipya
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Leon Bahati na Godfrey Nyang'oro

TUME ya Uchaguzi (Nec) jana ilimtangaza mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa nafasi ya rais baada ya kupata asilimia 61.17 ya kura zote zilizopigwa Oktoba 31.Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame alimtangaza mshindi huyo kwenye hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee iliyotawaliwa na ulinzi mkali huku mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa akiikosa hafla hiyo.
Kwa mujibu wa Jaji Makame, Kikwete alikusanya kura kura milioni 5.27 kati ya kura milioni 8.62 zilizopigwa na anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Dk Willbrod Slaa aliyepata milioni 2.3 sawa na asilimia 26.34.
Lakini katibu huyo wa Chadema Dk. Slaa, ambaye alisema atayakataa matokeo hayo kutokana na taratibu nyingi kukiukwa, hakuhudhuria hafla hiyo.

"Nawapongeza wananchi, wanachama wa CCM na viongozi wa upinzani kwa kuonyesha ushirikiano," alisema Kikwete katika hotuba yake ya shukrani baada ya kutangazwa kuwa rais mteule.
"Napenda kuwathibitishia wananchi kwamba nitatekeleza ahadi zote nilizoahidi kwa mujibu wa ilani ya CCM; ahadi za papo kwa hapo nilizozitoa baada ya kutathmini matatizo ya wananchi na mambo mazuri ambayo yalielezwa na wapinzani.
"Katika yale waliyotoa wapinzani, yapo yanayoshabihiana na ya kwetu lakini kuna baadhi waliyoyatoa mazuri zaidi kuliko sisi. Tutayazingatia.

"Lengo la wagombea ni kuijenga nchi kimaendeleo na siyo kugombana. Tunajenga nyumba moja, hatugombei fito."
Lakini Kikwete, ambaye aliingia Ikulu kwa kuzoa asilimia 81 ya kura zote mwaka 2005, alionyesha kustushwa na ushindi mdogo wa mwaka huu wa asilimia 61.1.


afrikawakuu.jpg
Wakuu wa nchi wakifuatilia kwa makini kuapishwa kwa Rais Jakaya Kikwete

"Kuna changamoto nyingi zilijitokeza ambazo zitaifanya CCM ijiulize na kukaa chini ili kutafuta ufumbuzi wake... kutafuta nguvu mpya katika chaguzi zijazo," alisema Kikwete.
"Pamoja na wapinzani kuonyesha kuimarika, itabidi tukae kitako kuangalia ni namna gani tutafanya ili katika chaguzi zijazo tuweze kufanya vizuri zaidi."

Wagombea wengine watano walihudhuria hafla hiyo ambayo ilikuwa hitimisho la mtifuano wa kisiasa wa wagombea wote saba waliokuwa wakizunguka nchi nzima kwa takriban miezi mitatu wakiomba ridhaa ya kuongoza Watanzania.
Mgombea wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alishika nafasi ya tatu akiwa amepata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06, akifiatiwa na Peter Mziray wa APPT-Maendeleo aliyepata kura 96,933 sawa na asilimia 1.12, Hashimu Rungwe wa NCCR-Mageuzi kura 26,388(0.31%), Muttamwega Mgahywa wa TLP kura 17,482(0.20%) na Fahmi Dovutwa wa UPDP 13,176 (0.15%).

Hata hivyo, ni asilimia 42.8 tu waliojiandikisha, ndio walioshiriki kupiga kura Oktoba 31, idadi ambayo ilikuwa gumzo miongoni mwa wengi walioshiriki hafla hiyo kutokana na kutofautiana sana na hamasa iliyoonekana wakati wa kampeni.
Takwimu za Nec zinaonyesha kuwa waliojiandikisha kupiga kura walikuwa watu 20,137,303, lakini waliojitokeza kupiga kura ni watu 8,626,283 tu, kiwango ambacho hakifikii hata nusu ya walioandikishwa kwenye daftari la wapigakura.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Jaji Makame alisema kwa mujibu wa ibara ya 41(6) ya katiba, mshindi anapatikana kwa kupata kura nyingi zaidi ya wenzake.

"Kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... Namtangaza Jakaya Mrisho Kikwete wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika tarehe 31 mwezi wa kumi (2010)," alisema Jaji Makame.
Tangazo hilo lilichafua utaratibu mzima wa hafla hiyo kutokana na wakereketwa wa CCM kuanza kushangilia na kuimba na kumfanya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Nec, Rajabu Kiravu awakemee.
"Kinachofanyika hapa ni kuiharibu hii hafla hii," alilalamika Kiravu, lakini wapenzi wa CCM waliendelea kuimba nyimbo, kushangilia huku wakipeperusha bendera ndogo za CCM.

Hali hiyo ilimlazimisha Kiravu kuchukua kipaza sauti na kuwataka viongozi wa CCM wawatulize wakereketwa hao.
Jaji Makame alisema kwamba matokeo hayo yanatoka kwa wasimamizi wa majimbo 239 kote nchini.
Alisema majimbo saba hayakufanya uchaguzi wa wabunge na kata 23 hazikuchagua madiwani wao, lakini akasema chaguzi hizo zitafanyika mapema iwezekanavyo.
Baadaye Jaji Makame alimkabidhi Kikwete cheti cha ushindi na kufuatiwa na hotuba fupi iliyotolewa na Prof Lipumba kwa niaba ya wagombea urais walioshindwa.
Profesa Lipumba alisema katika hotuba yake kuwa alipewa nafasi hiyo kutokana na mshindi wa pili, Dk Slaa kutofika kwenye hafla hiyo.

"Salamu hizi zilikuwa zitolewe na Dk Slaa. Tulikuwa tumekubaliana mshindi wa pili ndiye atakayewawakilisha wenzake, lakini kwa kuwa hayupo, imenibidi nichukue nafasi hiyo," alisema Prof Lipumba.
Prof Lipumba alisema wote kwa pamoja wanampongeza Kikwete kwa ushindi alioupata.

Lakini alitoa lawama nyingi kwa Tume, akidai kuwa ilishindwa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura.
Alisema kuna watu wengi walioshindwa kupiga kura kwa sababu tu majina yao hayakuorodheshwa katika karatasi zilizobandikwa kwenye vituo mbalimbali vya wapiga kura nchini.
Alisema ushindi wa Kikwete si wa kujivunia kwa sababu alichaguliwa na asilimia 27 tu ya watu waliojiandikisha kupiga kura.
"Pamoja na kutambua Kikwete ni mshindi, waliomchagua ni asilimia 27 tu. Hili si jambo la kujivunia. Tume wametuangusha hawakuweza kuwahamasisha wengi wajitokeze kupiga kura," alisema Profesa Lipumba.
Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa vikali na baadhi ya maofisa wa Nec waliozungumza na Mwananchi kwa sharti la kutotajwa majina gazetini.

Walisema kazi hiyo si ya Nec pekee, bali pamoja na vyama vya siasa kuhakikisha wafuasi wao wamejiandikisha na kujitokeza kupiga kura.
Profesa Lipumba alielezea pia kuwa vyama vya upinzani havina imani na Nec na vimekuwa na wasiwasi kama kweli wanauendesha kwa njia huru na ya haki kama wanavyojinadi.
Viongozi hao wa upinzani walipendekeza kuwa muundo wa tume hiyo ubadilishwe ili uweze kuwa na watu watakaoaminika pande zote.
Mwakilishi hiyo alisema suala la kukubali matokeo wamekuwa waklilichukulia kama ni moja ya njia za kutekeleza uvumilivu wa kisiasa.

Lipumba alimaliza kwa kumkabidhi Kikwete ilani ya CUF kwa tahadhari kwamba hakutumwa na wagombea wengine, bali ni kwa utashi wake ili kiongozi huyo aitumie katika kuleta maendeleo nchini.
Akitoa hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi, Kikwete alianza kwa kuwakemea wafuasi wa CCM waliokuwa wakishangilia kwenye hafla hiyo bila ya kujali utaratibu.

"Tafadhali shughuli hii inasimamiwa na Tume; tafadhali tutulie; tusubiri iishe kama ni kujimwaga, mfanye hivyo baadaye," alisema rais huyo mteule.
Rais huyo mteule alielezea tathmini ya uchaguzi huo akisema kuwa imeonyesha demokrasia nchini inaimarika.
Aliigeukia Nec akisema kuwa nao wajitathmini na kujipanga kukabili kasoro zilizojitokeza, akiwaasa kwamba kazi yao ni ya lawama.

Katika kuendelea kutathmini uchaguzi uliomalizika, alisema mambo mengi yenye madhara yanayoelekea kuligawa taifa kama vile siasa za udini, ukabila na kuchochea uhasama miongoni mwa wananchi yalijitokeza.
Aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na vyombo vya habari kujitahidi kufuta chokochoko hizo ili Tanzania iendelee kuwa ya amani na utulivu.

Aliviasa vyombo vya habari kwamba vikitia chumvi chokochoko hizo vitakoleza moto na hata kulifanya taifa kuangukia kwenye matatizo ya ubaguzi.
Hata hivyo, alivisifu vyombo vya habari nchini kwamba vilifanya kazi nzuri wakati wa kipindi chote cha kampeni.
Katika hatua nyingine aliwataka waangalizi kutoka sehemu mbalimbali kutoa taarifa zao ili Tanzania izitumie kama njia ya kujitathmini na kurekebisha kasoro kwenye chaguzi zijazo.

Watu mbalimbali walialikwa kuhudhuria hafla hiyo na miongoni ni mabalozi wa nchi mbalimbali wanaowakilisha hapa nchini, wakurugenzi wa mashirika ya umma na binafsi, wahariri watendaji wa vyombo vya habari, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, mawaziri wanaomaliza muda wao, wabunge wateule wa CCM na wanachama wakereketwa wa CCM.
Wengine ni marais wastaafu, Benjamin Mkapa wa awamu ya tatu na waziri mkuu mstaafu, Joseph Warioba na majaji wa Mahakama Kuu na wastaafu.

Kikwete ataapishwa leo.
Sherehe hizo zitahudhuriwa na marais kutoka Kenya, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya Nje pamoja na Ushirikiano wa Kimataifa, nchi nyingine zitakazotuma wawakilishi wake ni Burundi, Msumbiji, Algeria, Botswana na Uganda

Chanzo. Gazeti la Mwananchi
 
wangetumia tu vitabu vitakatifu, ungesikia Puuuuuuuh chini, lete ambulance, pipiiiiiiiiiii, pipiiiiiiii horn everywhere Mungu si mnafiki, ila hivi mwishoni baada ya kumalizia kuapa kama vile kasema eee.. Shekhe Yahya nisaidie, ole wao wezi angetaja tu Mungu nisadie ingekuwa balaa, Biblia inasema Usilitaje bure jina la Mungu wako.
 
Wanasiasa wengi wanashiriki mambo ya nguvu za giza so ni wachache sana wanaoweza kuapa kwa kutumia sacred books!

ur right and among few of them is my favourite presidaa obama aliaapa kwa bible,yaani yule am 99%sure no uchakachuaji mana kabla ya apo alikua na vipingmizi ving vya kushindwa but chaguo la mungu halipingwi no matter what,so even wit us its jst a matter of time my frnds...the patientdog eats the fattest bone:israel:
 
Jamani ehhh! tusisahau swali la thread hii. Je unaapa kwa kutumia katiba au vitabu vya dini yako?? sio uislamu wala ukristo hapa.

Kwa uelewa wangu mimi, kuapa (popote pale, including mahakamani na kwenye politics) ni kwa kutumia kitabu cha dini yako e.g Quran au bible.

Mfano: mahakamani kama muislamu unaapa kwa Quran, never wil u use criminal procedure act or constitution au elections act (kama ipo). 4 that, believe there must b an error o a gud reason 2 use the constitution kuapa.

Ni hayo tu!!
 
Back
Top Bottom