Kikwete aamuru mitambo ya IPTL iwashwe mara moja!

Ninajiquote nilichosema tarehe 15/10/2009

Ninapendekeza;

  • Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.
  • Sikutaka kusema chochote nikiamini kwamba Shirika la TANESCO, Serikali, na kwa upande wa bunge, Kamati ya masuala ya Nishati na Madini, wangeweza kutoa majibu ya tatizo linatukabili. Badala yake, juhudi nyingi zimetumika kutafuta chanzo cha tatizo na kuchelea kutoa suluhuInaumiza sana kuona kuwa tunaendekeza siasa rahisi tunaposhugulikia masuala mazito ya kitaifa kama Nishati. Inasikitisha zaidi pale tunapoona kuwa serikali inashindwa kuchukua hatua mahususi za kuhami uchumi wa Taifa letu. Serikali na Bunge hazitoi suluhisho la hali hii na ni wazi kuna kutupiana mpira wakati nchi inaumia. Serikali imewekwa madarakani ili ifanye maamuzi na tuihukumu kwa maamuzi hayo. Serikali ni lazima sasa iamue.
  • Mazingira magumu kama haya yanahitaji maamuzi magumu (extra ordinary circumstances require extra ordinary decisions). Ninaamini serikali itazingatia ushauri wangu.
Mnisamehe kwa kujiquote!

Ikulu inasema wafanyabiashara ndio wamemwomba Rais. Ni sawa tu........
Usijali Zitto, cha msingi watu wenye akili zao timamu wameona mchango wako kama ulivyoutoa na umezingatiwa kama ulivyoshauri, whether tey acknowledge it or not, thats their problem. We have already noted it in our histrory. Ndo uzuri wa kuweka vitu kwenye maandishi, yaani hawawezi kukweepa kwamba ni idea yako hata kama watasema ni wafanyabiashara wa kihindi na kichina ndo wameomba. They are this bad, they are ready to praise outsiders (investors so they call them) than one of their own, what a shame!
 
Mkuu Mkandara kula tano. Hii kwa vyovyote vile ilipangwa na sasa imefika wakati wa kutekeleza. Sijui kama Zitto na yeye alifahamu hili na akaja kuwawahi kwa kusema iwashwe mitambo. Alijuaje kuwa iko tayari? Au kwa sababu wenzetu wako chunguni? Basi kumbe hatufahamu mengi na hapa kwa kweli tunacheza wanavyoimba WANASIASA.

What to expect from Mafiosos? They plan in advance na huwa probability zao zimechezwa vizuri sana kiasi kwamba ukisema false inajibu true!
( Ukienda ndani sana unakuta akina Sir Andy wamo)
 
BRAVO BROTHER ZITTO
Si mara zote binadamu wanakubali ukweli wa mambo. Brother nakupa bravo kwa ushauri wako wa last week kuhusu mgao wa umeme.
Kila la heri ktk masomo. Watanzania naamini wanahitaji mawazo yako kwa nyakati zote.
 
kuna kitu mwanakijiji kadokeza in one if the threads sijui ndo hivi vinaanza kitokea.... Lets wait. Huenda mapendekezo yote ya Zitto yakatekelezwa lakini wakatwambia kiujanja ujanja ni initiative zao. Ama kwelu serekali yetu.
Watanzania lazima tukubali kuwa sera ya kukosolewa imo ndani ya chama cha Mapinduzi. Kwa kumbukumbu zangu Mwl alisema kitu kama hicho ndani ya sera za chama cha mapinduzi na mara zote nafikiri chama cha mapinduzi kimekuwa kikifuata sera hii. Lazima tukubali Rais wetu amefuata sera hii. Zitto ni Mtanzania na ushauri wake pamoja na watu wengine ambao walipendekeza kuwa mitambo iwashwe imetekelezwa kwani CCM ni chama kinachokubali kukosolewa. Na ndivyo Mwenyekiti wa chama amefanya. Hakuna kosa hapo Watanzania.
 
What?. Sasa mbona kipindi chote watu wanaumia na mgao wa umeme wao walikuwa wanavuta miguu tu, kweli bongo tambarare!.

Alikua anasubiri Zito Kabwe aseme. Ama kweli semi kama Polepole ndio mwendo, harakaharaka haina baraka n.k zimetulemaza au zinatuelezea tulivyo.
 
Huu ushauri wa kutumia IPTL ndio unasifiwa kiasi hiki?

Ama kweli miafrika ndivyo tulivyo. Yaani tatizo la umeme limekuwa linatabiriwa kwa mwaka mzima sasa na Kikwete hakufanya chochote ila leo ndio anaamka na kuanza kutoa amri kuwa IPTL iwashwe?

Alikuwa wapi siku zote? Zitto alikuwa wapi muda wote?

kwani Zitto ni waziri au mshauri wa rais? Soma mada uelewe ndo uanze kuchangia sio unakurupuka tu...yaani rais anasema ameamuru mitambo iwashwe kwa vile wafanyabiashara wameomba !! so wananchi wanavyoteseka he is not concerned au??
 
Watanzania lazima tukubali kuwa sera ya kukosolewa imo ndani ya chama cha Mapinduzi. Kwa kumbukumbu zangu Mwl alisema kitu kama hicho ndani ya sera za chama cha mapinduzi na mara zote nafikiri chama cha mapinduzi kimekuwa kikifuata sera hii. Lazima tukubali Rais wetu amefuata sera hii. Zitto ni Mtanzania na ushauri wake pamoja na watu wengine ambao walipendekeza kuwa mitambo iwashwe imetekelezwa kwani CCM ni chama kinachokubali kukosolewa. Na ndivyo Mwenyekiti wa chama amefanya. Hakuna kosa hapo Watanzania.

Raisi na watendaji wake ni incompetent.

Ni jambo la kawaida kuwa mitambo hata kama ni mipya lazima kuna siku itaharibika, na watu makini hata kwenye vikampuni vidogo lazima kuna reserve kwa ajili ya emergency kama hizo. Sasa kama unaendesha taasisi nyeti kama Tanesco bila kuwa na escape route tukuiteje. Halafu hiyo break down ya miezi kadhaa ni ya namna gani??

Alichofanya JK alitakiwa afanye from day one angekua ni mwenye uwezo wa kutoa maamuzi, na sio suala la sera ya kukubali kukosolewa. Kwa ujumla kazi ya uraisi ni kubwa sana kwa uwezo wake.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya M. Kikwetwe ameamuru mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL iwashwe mara moja, mitambo hiyo ina uwezo wa kuzalisha umeme wa 80MW -100MW huku akiitaka wizara ya Sheria na katiba kufuatilia maswala yote ya kisheria juu ya Serikali na IPTL.

MJ

Jamani mpaka JK aseme ndio watu watekeleze kwanini wasimsaidie huyu mzee kazi jamani mpaka asemee!!!!!!!!!!!!
Kwanini watu hawajitumi Rais anamambo mengi kwanini msimsaidie hili suala dogo la umeme.
 
hili si moja ya pendekezo la Zitto la juzi? Walikuwa wapi mda wote huo? Eti mpaka raisi afanye where is ze minister?

Wewe unashangaa hili la umeme kuamuliwa na Rais? Hivi hujui kwamba hata pale beach ya Ocean Road ni majuzi tu ndio rais kahoji kwa nini watu hawaruhusiwi kupumzika pale? Ndipo pakafunguliwa!

Watanzania tumelogwa, na aliyetuloga alishakufa, kwa hiyo hakuna dawa!
 
Ameogopa kuwapa shavu washikaji zake....kuuza dowans.....kazi ipo sijui watazirudishaje pesa za watu arabuni huko
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya M. Kikwetwe ameamuru mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL iwashwe mara moja, mitambo hiyo ina uwezo wa kuzalisha umeme wa 80MW -100MW huku akiitaka wizara ya Sheria na katiba kufuatilia maswala yote ya kisheria juu ya Serikali na IPTL.

MJ

Hongera sana Mh. Rais kwa kutimiza wajibu wako.
Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda, na akupe afya njema, uendelee kutuongoza.
 
Kwani Rais wetu yupo juu ya sheria? Kama IPTL na Serikali wana kesi mahakamani, Mhe Kikwete ni nani hadi aingilie uhuru wa mahakama?Jaji wa mahakama husika ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza hivyo.
 
Hapa wanatafuta pa kutokea, wameanza IPTL, kesho utasikia DOWANS nayenyewe iwashwe! watu hawalali.

Tulishang'amua tiyari - mitambo iuzwe ghafla itaifishwe!! yetu macho . Bado nina imani na kamati nzima ya madini wanajua wanachokifanya, hawakurupuki.
 
Ngeleja must go!

In Tanzania unlike in other countries, the vocabulary of Ministers resigning does not exist even people loose their life. (eg the recent Mbagala bombs issue) and therefore why should Ngeleja be the first.
 
Bila JK kusema hakuna kinachofanyika Tanzania..!!


after how long...u dont know, after investing how much energy..u dont know....u just find it happen n badly enough u dont think far from the limit, then what can i say than HOPELESS!
 
JK alikuwa anamsubiri Ngeleja, lakini amegundua kuwa jamaa ni bomu la wakati.
ZITTO aliongea wakasema ni mambo ambayo hayapelekwi tu kijuujuu, WAFANYABIASHARA!!!! wameongea tu na JK amereact. SO IT MATTERS NI NANI KASEMA!!! Tutafika???
 
Back
Top Bottom