Kikao cha wabunge wa CCM na kamati ya Mwinyi Dodoma

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
kikao hiki muhimu kinchohusisha kumwaga lazi kwa mafisadi kama chanzo cha kuivuruga CCM ndo kinaendelea hapa bungeni Dodoma.

Wait for more information.
 
naangalia lowassa hayupo ndani ila pia fisadi rostaam hayupo hadi muda huu nipo mtamboni amemtuma kibaraka wake peter serukamba from kigoma mjini kumchukulia taarifawait for updates
 
Naamini wabunge wengi wa ccm wanadhani kinachofanyika ni kutafuta muafaka wa ndani kwa ndani.

Chama chochote makini kingeunda kwanza mfumo wa kujisahihisha badala ya kupatanisha walio safi na mafisadi. Hivyo basi aslimia zaidi ya 50 ya viongozi sio safi ndo maana wanag'aka wakiambiwa kuwa kuna ufisadi ktk uongozi wao. Hata ushahidi ukiwa peupe msidahni kwamba CCM yetu ipo kwa maslahi ya mwananchi wa kawaida. Ni kwa ajili ya wawekezaji na kuwavutia matajiri kuja kuvuna maliasili zetu kwa malipo kiduchu (wanayofaidi viongozi)
 
Hata wakivaa ngozi ya kondoo, lakini bado ni mbwa mwitu wakali. Asilimia kubwa ya viongozi wa CCM na serikali yao akianziaa na JK hawaifai hata kidogo kuwa viongozi wa watu, ila wanawatawala watu kwa mabavu ili kutimiza malingo yao na si kwa ajili ya wananchi.
 
mzee mwinyi anafungua kikao sasa kwa kutoa dukuduku lake hasa mwelekeo chama ilichonacho sasa wah. ni wengi sana wamefika
 
naangalia lowassa hayupo ndani ila pia fisadi rostaam hayupo hadi muda huu nipo mtamboni amemtuma kibaraka wake peter serukamba from kigoma mjini kumchukulia taarifawait for updates

Lowassa yupo nje ya nchi kwa matibabu ya macho, Rostam sijui lakini wabunge wengi hawapo Dodoma. Nafutialia vikao vya Bunge kupitia TBC na viti vingi havina watu. Lakini mafisadi wabunge ni hao tu? au hata wale wanao kula posho tatu tatu na kujifanya wema kwa wananchi?
 
Kasabau ya ubinafsi walio nao, ndo maana makundi yamekuwepo CCM, wanatafuta jinsi ya kuungana lakini sidhani kama watafanikiwa.
 
naangalia lowassa hayupo ndani ila pia fisadi rostaam hayupo hadi muda huu nipo mtamboni amemtuma kibaraka wake peter serukamba from kigoma mjini kumchukulia taarifawait for updates
tunaambiwa lowasa yupo ujerumani kwa matibabu ya macho sijui kweli.
Makamba vipi yupo au bado ana kizunguzungu .
Lakini hakuna lolote hapo ,bunge limeburuzwa leo kwa ajili ya kikao hicho nchi hii bwana kweli tunakoelekea sijui ni wapi???? giza nene .
 
Lowassa yupo nje ya nchi kwa matibabu ya macho, Rostam sijui lakini wabunge wengi hawapo Dodoma. Nafutialia vikao vya Bunge kupitia TBC na viti vingi havina watu. Lakini mafisadi wabunge ni hao tu? au hata wale wanao kula posho tatu tatu na kujifanya wema kwa wananchi?

mkuu mbona hii ilikuwa kitambo, hayo macho hayajapona na amerudi tena?
 
Kwani hamjasikia kwamba mambo yalikuwa mazito? Sendeka karipua kila mtu kuanzia Spika hadi kina Rostam na kundi lake, yaani kapiga kote kote kama upanga. Tutasikia.
 
Mkutano uko mida hii ama umeanza mapema mchana ? Sendeka kalipua nini mbona habari hizi nusu ?
 
Hakuna jipya hapa, mazingaombwe yanaendelea kama kawaida.

Utaniambia.
 
Lowassa yupo nje ya nchi kwa matibabu ya macho, Rostam sijui lakini wabunge wengi hawapo Dodoma. Nafutialia vikao vya Bunge kupitia TBC na viti vingi havina watu. Lakini mafisadi wabunge ni hao tu? au hata wale wanao kula posho tatu tatu na kujifanya wema kwa wananchi?
Huyu lowassa yupo israel kaenda kupanda milima alioyopanda yesu na nilisafiri nae kwenye ndege moja ya ethiopian.sijui kama kaenda kutibiwa macho ninachojua ni kupanda milima ya yesu .pengine kaenda kutubu huko
 
"UPINZANI WA KWELI KATIKA NCHI HII UTATOKANA NA CCM. CCM WAKIVURUGANA WAKATENGANA, HAPATAKUWA NA CHAMA TAWALA TENA, HIVYO ITAKUWA RAHISI KWA MTU YEYOTE ATAKAYEKUBALIKA KUINGIA MAHALI PATAKATIFU, IKULU" Kwa miaka mingi CCM imeliongoza Taifa hili kwa kujiamini na kuchukulia kila kitu ni rahisi. Na cha ajabu zaidi kila aliyekuwa tofauti na msimamo wa chama Bungeni kwa awamu moja, kipindi kilichofuata aliondolewa mapema kwenye kura za maoni. Naomba tuamini kuwa kipindi hicho kimepita. Kwa sababu ya kulindana na kushikilia msimamo wa chama pasipo kuelewa hata shabaha na maslahi ya yule aliyeuleta, nchi yetu imejikuta ikingia mikataba mfu inayoididimiza kila kukicha. CCM kama imechoka madaraka ifanye lile linalotamaniwa na watu wengi; "IWAZIBE MIDOMO WALOPOKAJI" Sipendi kuamini kama wanaharakati wa kweli wanaochomoza ndani ya CCM wakifanyiwa kinyume watapata ujasili wa kusubiri hisani ndani ya chama, na ninashawishika kusema wanakubalika kwa wananchi hata wasipokuwa na chama (kama serikali itashindwa tena kesi). Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Tubariki Wavuja Jasho.
 
Ndo faida ya makundi yaliyoanzishwa na JK na mitandaao yake kuwania uongozi. Waliwachafua wengine kwa tuhuma za kuwa wameua na wengingine tuhuma kibao. Ukipanda chuki utavuna chuki. Sasa ni zamu yao kuvuna nafikiri wawe wavumilivu wavune tu.
 
Back
Top Bottom