Kijue Kijiji cha Ikola na watu wake

TUENDELEE

Kwanza niwatake radhi ndugu zangu, naandika kwenye notipad halafu ndo nahamishia hapa, sasa simu ilijizima kabla sijasevu, ninatumia kitecno kinasumbua kweli.

BALAA LA PILI

Baada ya jamaa kukata moto, ndugu walikaa kikao wakatoka na azimio moja, kwamba kwa yeyote atakayekuwa amehusika na hicho kifo basi hatabaki salama, yeye na ndugu zake hadi mifungo yote wanayomiliki na panya walioko kwenye nyumba zao.
Wakamzika ndugu yao maisha yakawa yanaendelea.

Sasa yule jamaa aliyesema ameenda kwa waganga 20 alikuwa na mke na mtoto mmoja, siku moja wakatoka ili waende kuzunguka mjini, akapita kule kwenye boti yake ili aangalie kama wametia nanga kiusahihi. Mara mtoto akamwambia baba yake kwamba anataka kupanda boti, baba akamwita na mke wake wakaingia ili wazunguke kidogo ziwani. Sasa wakati wamefika mbele akaibuka yule mwamba aliyefariki, akazima injini, yule baba akashtuka, mara mtumbwi ukapigwa ukageuka. Hao wakawa wa kwanza kwenye ile listi.

ITAENDELEA
Tupo gia namba 3, si haba gari inaenda ila taratibu sana
 
Back
Top Bottom