Kijijini kuzuri - gorofa ya kisasa, setilaiti dish 4 nyumba moja?

Inawezekana mwenzetu macho yake yana makengeza hadi anaona hilo ghorofa ni imara. Hapo si pa kuingia, ni pa kupita ukikimbia.

Kumbuka kifo hakichagua pa kukuchukuli so utapita hapo ukikimbia utaenda kulala g.mboto mabomu yatakumaliza ambayo pia yalinunuliwa kwaajili ya maisha bora kwa kila mTz
 
mkuu ukipewa picha za majumba ya vijijini huko kilimanjaro si utakufa kwa presha?

Kote huko nimetalii, hakuna mkoa nisiotia mguu isipokuwa Kigoma tu.

Kinachonitoa kamasi ni chafya ya jengo la gorofa hapa kijijini ambayo teknoljia ya kawaida tu imetumika na jengo linadunda. **** mambo mengi tunahangaika gharaza zisizo za lazima na hata kama ile gorofa mnaikumbuka iliyojenwa kwa miti tu kule Rufiji, Tunaanza na hayo kwanza wakati uwezo wetu umeishia hapo. Mengine tuyaache hadi uwezo utakapoturuhusu.
 
mkuu ukipewa picha za majumba ya vijijini huko kilimanjaro si utakufa kwa presha?

GHOROFA%2BKIJIJINI.JPG

Hili ghorofa limejengwa katika wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma. Hawa wamatengo ni kama wachaga, wanajenga vijiji kwao, ukifika mjini Mbinga hakuna pilikapilika nikama ilivyo moshi ya Kilimanjaro. Vijijini kwao hawa wamatengo wakati ngeleja anakejeli megawati zake wao hawana habari, maana kahawa inawapo kiburi sana cha kutengeneza ulimwengu wao.
 
f3.jpg

2561810630_8c2007899b_z.jpg
Kendalvle_damg1.jpg

Nyumba hizo hapo juu za ghorofa za wazungu huko marekani zinavyoshindwa kuhimili vishindo vya dhoruba ya hali ya hewa, linganisha na ghorofa ya mtanzania iliyojengwa mathubuti kwa matofali imehimili vishondo vya dhoruba miaka yote hii na bado inaendelea kupeta tu.

GHOROFA%2BKIJIJINI.JPG

Tuwape moyo kuendeleza wafanyayo ndio ukombozi kuliko kuwakandia kwani itadidimiza jitihada zao.
 
Hilo ghorofa sio imara kabisa si umeona limebend hapo kwenye slab

Siku likianguka na "kumchania mtu nguo" kama kawaida yetu tutaishushia Serikali lawama utafikiri wanaokaa humo hawaoni kuwa jengo lina matatizo!
 
Siku likianguka na "kumchania mtu nguo" kama kawaida yetu tutaishushia Serikali lawama utafikiri wanaokaa humo hawaoni kuwa jengo lina matatizo!

Kwa taarifa yako ujenzi wa ghorofa hiyo hautofautiani na mfumo wa ujenzi wa majengo mengi ya zamani yaliyopo Dar es Salaam Ikulu ikiwa moja wapo. Kuna majengo mengi si Tanzania tu, hata mataifa mengine ya Asia, Ulaya na Marekani yalijengwa kwa mtindo huu na yana umri wa zaidi ya karne mbili au tatu na bado yanatumika, hakuna vyuma aina ye yote vilivyotumika hata mapaa yake. Steel truss zilianza kujitokeza mwishoni mwa 1800 AD, ni majengo machache sana yaliyo na mfumo huo.

Sasa jengo hili kwa vile liko kijiji mnalibeza, lakini yaliyoko dar ambayo siku zote tunafanya kazi na kuishi humo hamoni kama ipo siku yatadondoka?
 
Umetumia nguvu nyingi isivostahili kupinga hoja yangu! Nilichoandika kinahusiana na hoja ya member aliyetangulia kuhusu "ku-bend" kwa gorofa hilo na siyo "ubora" na wala siyo kwa sababu ya kujengwa kwake "kijijini."
 
Sidhani kama nguvu nyingi, ni kitu cha kawaida kama uwapo kwenye kutetea tesisi yako, jopo la maprofesa likija na hoja ya kutokukubaliana na baadhi ya hoja zako, inabidi ujipange kwa hoja nyingine kujenga utetezi, na ndio ulimwengu wa falsafa ulivyo.
 
Sawa Mkuu, haya "tumekubaliana" nini hapo?
 
wanaolalamika kuhusu maisha ni wavivu wa kufikiri,kwani yeye kaweza ana nini na anaeshidwa ana nini? nimeipenda sana hii. tukiamka tukaachana na kupenda kutafuniwa tutafika mbali.
 
Raha jipe mwenyewe

Wengi wetu tunafikiri maisha mazuri ni mijini, wakati hali ya maisha mijini inazidi kuwa ngumu na pengine mazingira ya wengi mijini yanawakosesha hata faragha ya kifamilia. Kijijini ukiwa na nyumba yako ya kawaida tu two bedroom, sebule na jiko, weka solar, maisha poa sana maana unahakina unaweka dishi la news dunia yote iko kijijini, cooler ndogo kuweka ulanzi, komoni au mbege, bila kusahau chimpumu, chakula usiseme maana ile organic original ndio kwenye jiko, nini ukose yakhe? nakubaliana maisha jipe mwenyewe, hakuna wa kumyooshea kidole.
 
Nakumbuka nyumba ndogo lakini ya ghorofa ilikuwa katika barabara kati ya Peramiho kwenda Mbinga hivi ndiyo hii? Kuna wakati Rais msaatafu mzee Mwinyi alitoa msaada wa mabati kwa kuwa wakati huo iliezekwa kwa nyasi.
 
Inawezekana ndo hii, nilipita mitaa hiyo zaidi ya 15 years ago na kwa kumbukumbu yawezekana ndo hii. Nashangaa wanayoibeza lakini inadunda tu. Tulitembelea huko wakati mkeka wa Makambako-Songea unali mbichi
 
Back
Top Bottom