Kijijini kuzuri - gorofa ya kisasa, setilaiti dish 4 nyumba moja?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
GHOROFA LA KISASA KIJIJINI

GHOROFA%2BKIJIJINI.JPG


Nani amesema ghorofa ni lazima liwe mjini tu? Wilayani Mbinga eneo la kijiji cha Mahande lipo hilo ghorofa ambalo halikuhitaji utaalamu wa wakandarasi kulijenga na liko imara kwelikweli.


MADISHI MANNE NYUMBA MOJA KIJIJINI

MADISHI%2BMANNE%2BWILAYANI%2BMBINGA.JPG


Pichani ni nyumba ambayo iko kijijini ikiwa na Satelaiti Dish. Hapa ni nyumba yenye nyungo nne tofauti kwa ajili ya kupata taswira mbalimbali za kidunia kwa kila ungo na kazi yake. Haya ni maendeleo vijijini kwani kwa kuwa na vifaa hivyo ina maana huyu ndugu ni lazima awe na jenereta kwani hapa kijijini hakuna umeme.
 
Labda solar mkuu!
Well na quality yake ya maisha itakuwa nzuri. Chakula natural, hewa safi maisha yanaendelea.
 
nimewahi kupita kijiji kimoja huko iringa nikaona nyumaba kama hii.....
 
Hapa kweli dhamira nzuriya sirikali ya cciem imefanikiwa. Maisha bora kwa kilamtz ghorofa na madishi vijijini.Muda si mrefu magari yatakuwa mengiya kumwaga vijijini. Nani alisema chama tawala hakijafanikiwa?
Labda solar mkuu!
Well na quality yake ya maisha itakuwa nzuri. Chakula natural, hewa safi maisha yanaendelea.
 
sure sio imara kabisa! Maana sioni hata beams hapo!sijuhi hata hiyo slab imebebwa na nini!

mwenzio kasema hiyo ghorofa haikuhitaji utaalamu wa mkandarasi kujengwa, we unauliza beams, SLAB sijui nini? Aliposema "haikuhitaji utaalam" we umeelewaje?
 
Sure sio imara kabisa! Maana sioni hata beams hapo!sijuhi hata hiyo slab imebebwa na nini!

Tembea uone. Nyumba za vijijini hawatumii beams kwenye madirisha na milango kama ulivyozoea mjini. Nimezaliwa vijijini katika nyumba kama hizo, na mpaka leo nyumba niliyozaliwa na kukulia hapo mlangoni ubao uliowekwa kukinga matofali umepinda vivyo hivyo nadi leo, kumbuka nimezaliwa nimekuta hivyo na hadi leo umri huu nyumba ingali na niendapo nalala kwenye nyumba kama hizi. Nyumba hizi hazijajengwa kwa saruji, ila matofali ya kuchomwa kwenye tanuru za kienyeji na kisha kujengwa nyumba kwa kutumia udongo wa kawaida tu nyumba inadunda miaka nenda rudi. Achana na uachitekicha wenu sisi wa vijijini hatuutaki. Mnataka kutulalia tu. Ona mijini mnahangaika na megawati huku vijijini tuna setilaiti zetu zinakula mzigo bila megawati za Ngeleja.
 
maisha bora kwa kila mtanzania yametimia.... not

Huenda kweli yametimia si unaona hata foleni zimeongezeka kwenye majiji ya Tz? Ndivyo rais wenu alivyofanya tathmini yake jama msijefikiri mimi ndo nimenena hayo maneno
 
Hapa kweli dhamira nzuriya sirikali ya cciem imefanikiwa. Maisha bora kwa kilamtz ghorofa na madishi vijijini.Muda si mrefu magari yatakuwa mengiya kumwaga vijijini. Nani alisema chama tawala hakijafanikiwa?

Kimefanikiwa but in negative way
 
Back
Top Bottom