Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,080
Binafsi mimi naona kijana kakosea, huenda alikuwa sahihi kumuacha ila namna alivyomuacha alikosea, ilibidi amuache kivingine, mkasa huu hapa nawapeni.
Kuna kijana mdogo wa kiume miaka 26 tupo nae kazini alikuwa kwenye uchumba na binti wa miaka 22, wote ni wasomi binti kamaliza degree mwaka jana.
Kijana alikuwa tayari kabisa mwezu huu kwenda kujitambulisha nyumbani kwa binti ili amuoe.
Wiki 3 ziliyopita kijana alipata safari ya kikazi kwenye mkoa anakotokea huyo binti, alikaa huko kama wiki hivi
Huko alipofika na kuamua kuchagua malazi ni mitaa karibu na nyumbani kwa huyo binti, katika kujichanganya na wakazi wa hapo akitoka kazini aliulizia kama wanamfaham mzee wa binti akaongezea na maelezo ya ziada, wakamwambia ni mtaa huo huo tu na wanaijua familia ya hapo.
Kijana ikabidi aanza kukamua intelejensia, akagundua kuwa pale nyumbani kwa binti kuna wanafamilia wawili wana matatizo ya kutosikia vuzuri na kuna mwengine huwa yupo ndani tu ana matatizo ya akili tangu mdogo.
kuna wawili wengine hawana shida wamesoma na wana kazi na biashara zao.
Hapa sasa nitaongea zaidi kama yeye mwenyewe alivyojitetea, ndipo penye kuamua kazingua au lah, twendeni pamoja.
Kijana ni kama alipata mstuko akataka kumuacha binti kienyeji ila alishindwa, ikabidi amuweke wazi kwamba anampenda lakini anachukua tahadhari hawezi kurisk kumuoa sababu ndoa bila watoto ni ngumu na anahofia alichokigundua kwenye familia anayotokea huyo binti, alimwambia kwamba mtu yeyote anaweza kupata ulemavu muda wowote maana hujafa hujaumbika, pia mtu yoyote anaweza kupata mtoto mlemavu maana hakuna anaemuumba mtoto atakavyo lakini yeye anahofia kwamba uwezekano wa kupata mtoto mlemavu utaongezeka zaidi endapo wao wakipata mtoto kwa kuhofia kwamba ulemavu wa wanafamilia ni magonjwa ya kurithi, hivyo hata kama binti ni mzima yawezekana karithishwa genes / genetics zinazoweza kuleta mtoto mwenye ulemavu, sababu ya zaida ambayo hakumwambia binti ni kwamba anahofia kuna mambo ya kiafrika kwenye mila au matambiko yaliyowahi kudanyika huko zamani yanarithishwa,
Alimwambia binti wanaweza kuwa na mahusiano mengine ila si kwenye kupata watoto, Binti hakumwelewa kabisa ikawa ndio mwisho hapo.
Je, ni sawa?