Kamkimbia mumewe baada ya harusi

mawardat

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
23,950
131,282
Wasalaam,

Ni hivi kuna binti jirani alipata mchumba wa dini tofauti, na kijana alimpenda binti, kijana alibadili dini na ndoa ikafungwa.

Kumbe binti alikuwa na danga lake jibaba, danga likaenda nyumbani kwa wazazi wa binti na kuwaambia kuwa anamtaka mke wake na yupo tayari kurudisha gharama za harusi. Danga likaonyesha chatting za yeye na binti, binti anasema kuwa anampenda jibaba na kuhusu kuolewa alilazimishwa na mama take.

Kijana aliyemuoa binti hadi sasa yupo hospitali, inasemekana kachomwa sindano ya sumu na wasiojulikana, na binti kamtorka kijana.

Inauma kwasababu kijana kabadili hadi dini kumfuata mwanamke na kuambulia maumivu. Mtu ukijiona haupo tayari kuolewa ni bora ukakataa kuolewa.


Tukio limetokea,wilaya ya Mbinga,na harusi imefungwa tarehe 13/7/2023
 
Mwanaume ameshatoa talaka? Kama bado, maana yake aliyemuiba huyo mwanaume kaiba mke wa mtu.

Mwanaume alipie tu gharama za kubadili dini. Unaamuaje kubadili dini kwa sababu ya mwanamke? Pumbavu!.
Mwanaume hajatoa talaka,yaani katorokwa,na Hadi Sasa kijanayupo hospital anapambania uhai wake.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom