Kiingereza..

Feb 20, 2012
93
11
Enyi ndugu na jamaa, salaam kwenu! Ktk kupita kwangu vidato mbalimbali nilikua nachanganya sana spelling au pronounciation ya maneno anuai ya kimombo. Mfano: Maintenance nakosea na kuandika maintainance, achieve>archieve. Matamshi ndio kabisaaa, mfano "great" natamka "griit" instead of "greet".. Loh! Kimombo kina wenyewe! Hayo ni machache tu ndugu zangu, nahisi hata wewe kuna mahali ulikua "unajikwaa" ama kwa kuandika spelling fyongo au kwa ku"pronounce".. Alamsiki
 
cycle na circle...kusoma na kuandika...
queue...kuiandika...
 
nakumbuka st kayumba primary school, std 3B na Std 4B

nikiulizwa;
what's your name!
Najibu,
Your name is Konnie.

Siku moja nilitaka toka nje niende msalani, nikamwambia mwalimu,

sorry madam, can you go to the toilet?

Akashangaa, akaanza kuniuliza sijui nini hata simwelewi. Nikakimbia nje bila hata kujua alikuwa anasemaje.
 
Mimi nakumbuka nilitoka shule za twanga pepeta nikahamia fm akademia darasa la 5 hapo.
Sasa tulikuwa mwisho wa muhula tunapewa ripoti zetu tunaweka kwenye bahasha.
Sasa zikagawiwa mimi nikakosa nikamwambia mwalimu' sir can i have an antellope?'instead of envelope nilichekwa na darasa zima
 
- Ilinichukua muda kujua kuwa verb inayofuata baada ya did inakuwa katika present. Kwa hivyo nilikuwa nikiandika na kusema kwa mfano, Did you saw my book badala ya Did you see my book?
- Na mpaka leo bado ninapata tabu kuandika exercise, ama ninataandika excercise au excise wakati hii ya mwisho ina maana tafauti.
- Siku moja nilimwuliza mwalimu wangu (Mwngereza); wakati tunakula yeye alikuwa ameacha kula nikamwuliza "Are you fed up" badala ya "Are you full up?". Lakini alinisahihisha kwa kunieleza maana ya fed-up; niliona haya sana.
 
Siku moja nikiwa darasa la tatu mwalimu alitoa passage fupi ilikuwa kama hivi: Juma said, Ally and Amina are brother and sister. Baadae akauliza je hapa kuna watu wangapi? Nikanyoosha mkono na kujibu watu wanne. Akasema wataje. Nikataja Juma, Said, Ally na Amina. Mwalimu alicheka sana.
 
- Ilinichukua muda kujua kuwa verb inayofuata baada ya did inakuwa katika present. Kwa hivyo nilikuwa nikiandika na kusema kwa mfano, Did you saw my book badala ya Did you see my book?
- Na mpaka leo bado ninapata tabu kuandika exercise, ama ninataandika excercise au excise wakati hii ya mwisho ina maana tafauti.
- Siku moja nilimwuliza mwalimu wangu (Mwngereza); wakati tunakula yeye alikuwa ameacha kula nikamwuliza "Are you fed up" badala ya "Are you full up?". Lakini alinisahihisha kwa kunieleza maana ya fed-up; niliona haya sana.

hio ya did you saw mbona iko correct?,au na mie nikapige msasa chiinglish changu?lol
 
Kiingereza chenye kutumia maneno kwa mfano 'kama ningemwona Juma ningefurahi sana' - 'if i could have seen Juma, i could have been very happy' kilikuwa kinanishinda kiasi kwamba nikawa nakwepa kujijengea mazingira ya kuyatumia hayo maneno kabisa..
 
Mi mgogoro ulikuwa kuandika quit na quiet....kwanza hata hapa sijui km nimezipatia
 
upatie wapi...hola aise...naomba sredi ibadilishwe title...co zaman tena ni wakati huu...

Teh wewe ngoja nikacheck kwenye dictionary chap...unaweza kuta nimepata halafu wewe ndo chaka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom