Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,427
Nashindwa huyo Kijakazi anatuona sie ni wajinga. Anakazana kwamba Nyerere hakutoa mchango wowote kukifanya Kiswahili kitie mizizi Tanzania.Acha chuki za kijinga kwa Mwalimu Nyerere, Mwalimu kwa asilimia kubwa ndie amechagiza kutumika kwa lugha ya kiswahili Tanganyika...mpaka sasa hivi ukiingia usukumani ndani huko kuna watu bado kiswahili kinawapiga chenga, je 1960 hali ilikuaje?...Juhudi zake kubwa za kuunganisha makabila, kuweka somo la kiswahili mashuleni na kufundisha elimu ya msingi mashuleni, kuweka redio na magazeti ya kiswahili na kutumia kiswahili kama lugha ya mawasiliano maofisini kulifanya Kiswahili kikue kwa haraka.