Kiingereza kilishawagomea ndugu zetu wa kusini, hata kwenye hafla za kitaifa

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,797
48,764
Yaani tu yaani...

screenshot_20220801-211019-png.2311408

img-20220523-wa0228-jpg.2236393
 
Hatunaga udugu na wapuuzi wa huko wanaoona wamefiiiika kwa kuongea kingereza kuliko hata kikamba au kikalenjin
Mbona mnajikanganya jombaa? Si nyinyi tu ndio huwa mnapenda kuwaponda sana wakenya, kwa kupenda kukuza na kuzungumza lugha zao asili? 'Vilugha' kama mnavopenda kuziita kwa dharau. Huku mkitunaga, kisa tuna hadi stesheni za redio na Tv, ambazo huwa zinatumia lugha zetu asili na waandishi maarufu pia. Ambao huwa wanaandika vitabu vyao kwa lugha zao za asili kwanza, kabla havijafsiriwa kwa lugha zingine za kigeni.

Kiingereza sio dili sana nchini Kenya jombaa, maanake hata vijitoto vya shule za chekechea huwa vinakizungumza, bila matatizo. Kujua na kuongea kingereza huwa haiwazuii wakenya kuzungumza na kujivunia lugha zao asili na kiswahili juu yake pia.

Tena zaidi ya yote, mashuleni wanafunzwa lugha zingine za kigeni, k.m. kifaransa, Kimandarin, Kijerumani n.k.

Sidhani kuna mtu yeyote yule ambaye angekuwa anawasema, kama mngekuwa mnakitumia kiswahili mwanzo mwisho, kwa asilimia mia. Ila kwasababu mnakitumia mashuleni na kwenye vyuo vikuu pia na bado kinawatoa kijasho hivi, basi bila shaka kutakuwa kuna tatizo kubwa sana sehemu fulani.
 
Mbona mnajikanganya jombaa? Si nyinyi tu ndio huwa mnapenda kuwaponda sana wakenya, kwa kupenda kukuza na kuzungumza lugha zao asili? 'Vilugha' kama mnavopenda kuziita kwa dharau. Huku mkitunaga, kisa tuna hadi stesheni za redio na Tv, ambazo huwa zinatumia lugha zetu asili na waandishi maarufu pia. Ambao huwa wanaandika vitabu vyao kwa lugha zao za asili kwanza, kabla havijafsiriwa kwa lugha zingine za kigeni.

Kiingereza sio dili sana nchini Kenya jombaa, maanake hata vijitoto vya shule za chekechea huwa vinakizungumza, bila matatizo. Kujua na kuongea kingereza huwa haiwazuii wakenya kuzungumza na kujivunia lugha zao asili na kiswahili juu yake pia. Tena zaidi ya yote, mashuleni wanafunzwa lugha zingine za kigeni, k.m. kifaransa, kimandarin, kijerumani n.k.

Pumba tupu
 
kiswahili gani mnafahamu zaidi ya kuongea ugoro.
 
Tuombe kuuliza kama Uingereza walishaanzisha ila course ya Kiingereza kufuatia manesi waliokuwa wanataka kufanya kazi Uingereza kufeli vibaya kwenye basics za Kiingereza.
 
Yeye mwenyewe alikua vizuri kingereza, nahisi ni uzembe wao tu, unajua walivyo.
Tena alikua vizuri kingereza hadi kufanya tafsiri ya plays za Shakespeare mbili- Bepari wa venisi na Juliazi kaizari(Merchant of Venice, Julius Caesar). Kizazi cha enzi ya mkoloni kilifaidi elimu bora/sound colonial education!
 
Tuombe kuuliza kama Uingereza walishaanzisha ila course ya Kiingereza kufuatia manesi waliokuwa wanataka kufanya kazi Uingereza kufeli vibaya kwenye basics za Kiingereza.
Hizo zilikuwa porojo tu, manesi 20,000 kutoka Kenya walipata ajira UK.
 
Hawa wanatia aibu na huruma. Makosa ni kwamba Nyerere alipowaambia wajifunze kiswahili waliichukulia kwamba anawaambia eti wakisahau kiingereza kabisa.

Wrong! Nyerere hakuleta Kiswahili Tanzania wala hakuwaambia Watanzania wajifunze Kiswahili, Mwalimu Nyerere amezaliwa amekuta Kiswahili kinatumika Tanzania kila mahali hata wakati wa Ukoloni wote Ujerumani na Uingereza Kiswahili kilikuwa kinatumika kila mahali, hivyo sababu ya Watanzania kuongea na kutumia Kiswahili siyo Mwalimu Nyerere.

Kiswahili ni Lugha yetu, ni Urithi wetu na ni sehemu ya Utamaduni wetu!
 
Nimeona videos za zamani za Nyerere akiwasihi Watanzania wakipende na kukitumia lugha ya Kiswahili na kukienzi na hio ndio ilifanya Watz wasahau lugha zao za asili na pia lugha ya Kiingereza.
 
Mwalimu Nyerere amezaliwa amekuta Kiswahili kinatumika Tanzania/Tanganyika/German East Afrika.
Biblia na Kanisa linatumia Kiswahili Tanzania sasa hiyo siyo sababu ya Mwalimu Nyerere, Tanzania kupata Kanisa linaloendesha misa kwa lugha ya Kiingereza siyo rahisi na hiyo siyo sababu ya Mwalimu Nyerere yeye mwenyewe alibatizwa kwa lugha ya Kiswahili na mafundisho kwa Kiswahili.

Hivyo Kiswahili kina Historia na mizizi mirefu Tanzania huwezi tu kukiondoa na ndio maana hata Wakoloni waliona ni bora wakikubali tu na kukitumia kama lugha ya mawasiliano badala ya kukifuta!
 
Back
Top Bottom