Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
- Thread starter
- #21
Napenda kutofautiana na mtoa hoja. Umeshindwa kutofautisha mambo mawili, WAJIBU na MAMLAKA. Siamini kuwa Waziri Membe ana nguvu na sifa ya kimungu ambayo mtoa mada anataka kumpa. Kwamba Membe anaweza kushitaki, kufunga na hata kuumba na kuhitimisha kila jambo. Membe ni Waziri wa Mambo ya Nje, Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Mtama tu. Hana mamlaka ya kushitaki, kuteua wala kufukuza.
Membe ni mmoja kati ya Mawaziri 13 waliowahi kuwa Mawaziri wa Mambo ya Nje toka tupate uhuru. Hakuna Waziri hata mmoja huko nyuma ambaye amewahi kuwa na mamlaka ya kushitaki, kufukuza wala kuteua. Hivyo, Waziri Membe si Waziri Mraba ni Waziri kama Waziri mwingine.
Waziri Membe kama kiongozi anao WAJIBU wa kukemea maovu katika jamii ikiwemo ubadhirifu na ufisadi. Membe kwa bahati mbaya MAMLAKA aliyonayo inamdhibiti kushughulikia maovu na ubadhirifu ndani ya Wzara aliyokabidhiwa pekee, na MAMLAKA hiyo imeainishwa katika 'Instruments' alizokabidhiwa alipoapa.
Kwa upande wa WAJIBU, Membe ndiye Waziri pekee katika Serikali ya Awamu ya Nne ambaye amethubutu kusema wazi kuwa wapo Watuhumiwa wa Rada nchini na wanapaswa kufikishwa mbele ya Sheria. Alilisema hili wakati akiwasilisha hotuba yake ya Bajeti mwaka huu( Rejea Hansard). Mawaziri wengine wote wamekuwa wakikwepa kulitamka hilo na wamekuwa wakidai kupatiwa ushahidi. Membe ametekeleza WAJIBU wake mkubwa zaidi wa kutetea maslahi ya taifa kwa kuvalia njuga fedha za Radar hadi Serkali ya Uingereza na BAE wakasalimu amri. Aidha, katika hili ameshirikisha hadi Bunge.
Sasa Membe amekamilisha WAJIBU wake na ametumia vyema MAMLAKA yake kama Waziri wa Mambo ya Nje kusimama kidete na kuongoza mapambano hadi fedha zmepatikana. Hata kama angependa kwenda mbele zaidi kuwashitaki watuhumiwa, MAMLAKA yake haimruhusu. Hata pale palipokuwa na Kesi ya Mahalu ambayo ilianzia katika Ubalozi wa Tanzania Rome, MAMLAKA iliyoshitaki ilikuwa ni PCCP,DPP na Mwanasheria Mkuu.
Nahitimisha hoja yangu kuwa Membe hana mamlaka ya Kimungu. Amekamilisha vyema WAJIBU wake na ndani ya MAMLAKA yake. Hata angekuwa na mabaya kiasi gani, anapaswa kupongezwa kwa hili. Swala la RADAR linapaswa kuulizwa kwa wenye MAMLAKA ya kuchukua hatua kuanzia pale alipomalizia Membe.
pole sana umetumia muda mwingi kujibu hoja ambazo zipo nje ya mada........mimi sijazungumzia mamlaka au umunugu wowote humu.............kwa hiyo hizo ni hoja mpya.............................kufhusu radar ningependa ni kujibu kama ifuatavyo:-
Membe hajawahi kututajia ni akina nani ambao walihusika na udhalimu wa hiyo rada kwa hiyo kuzungumzia kuwashtaki wasiojulikana ni unafiki mkubwa usio na kifani..........................................alipaswa awatambue kwanza halafu mengineyo yangelifuata...................
kuhusu kesi ya mahalu...............huu ni ushahidi wa ya kuwa Membe yupo pale kulinda mkate wake..................................hebu nieleze yuko JK na Luhanjo? Mbona hawajashtakiwa wakati wao ndiyo waliokuwa wasimamizi wa hiyo wizara? membe mbona hatujamsikia akilalama ya kuwa ni dagaa tu ndiyo wanashughulikia kama kule majengo pacha ya BOT?
anza kutafakari..........................membe ana walakinmi mkubwa na hafai kuwa kiongozi hata wa shina popote hapa nchini..............