Kifo cha RPC Mwanza: Maswali ya Bei Mbaya...

Nashkuru kuwa nanyi wana JF wenzangu, kimsingi tumepoteza another JEMBE alafu wanajamii tusipende kuhusisha kila jambo na siasa. Tujaribu kukosoa wapi serikali yetu inakosea na kuipa ushauri wa bure najua tupo maintelgensia wengi humu ndani ya mjengo wa JF!!
Una maana gani kuwa tumepoteza jembe?
Kwani marehemu alikuwa mwanaJF?
 
Waswahili usema ukiona mwenzio ananyolewa zako anza kutia maji!nasema haya kufatia tukio la mauaji ya ndugu yetu,malehemu Mwangosi!!!hawa wajamaa walidhani kafa paka!!!!!!!!!!?????hawakujua kuwa hatawao wawezeza kufa tena kwa risasi hizohizo wazitumiazo kwa nguruwe!!!!!!!!!!!!!!!!???????????:hatari:
 
Je kuuwawa bahati mbaya ni kwa raia tu? Je kitu kizito chenye ncha kali kilitokea upande gani? Je chago -njaa ameenda kuchunguza? Je RPC hakupigwa tokea alikotoka halafu akawakimbilia polisi jamii wamsaidie kwa sababu hata mwangosi tulidanganywa na chago-njaa kwamba alipigwa tokea kwenye mkutano akakimbilia kwa polisi kuomba msaada,mwisho kapumzike unapostahili kamanda,JEHANAM au PEPONI.

Aisee!
Hii inadhihirisha kwamba jamii imeshiba kabisa na chokochoko za polisi dhidi ya raia.
Kwa mtindo huu mbele giza...sioni kitu aisee!
 
kazi kweli kweli,eti dada! je mke wa marehem alikuwa anamfahamu huyo mama kuwa ni dada wa mumewe kweli? na hicho kikao cha harusi, ina maana mke wake alikuwa hahusiki? hapa kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia!
 
Duuuuuu ngoja jua lizame tuone kama Leo pia watakuwepo hao police jamii,nashauri nchimbi akafanye majaribio kuona kama hao watu wapi.ila jamani barlow Si mlevi?kama ni mlevi barnaids wafuatiliwe kutupa nyepesi.nina hofu Leo mwnza hakuna ulinzi Usiku wanaogopa kukamatwa.
 
Hili limetokea na majibu/dalili tosha kwamba mfumo wetu wa security umefeli and lazima tuchukue hatua za haraka.

.... ndio maana wameishia kuua raia badala kulinda raia na usalama wa taifa letu
.... ndio maana tunatenda makosa lakini ukiwa mlala hoi ndio sheria inafuata mkondo wake, ukiwa mtoto wa Kigogo mhhh

.... ndio maana wameshindwa kulinda raslimali zetu zinazoibwa kila kukicha

.... ndio maana wamelala kiasi kwamba intelligensia iko biased i.e. imekuwa tu ya kuwakosovo CHADEMA

.... ndio maana wameishia kufungua vikesi vya chap chap kutafuta Kinga ya kusema jambo hili liko mahakamani na lisijadiliwe

Hii ni hatari na yafaa uongozi mzima wa Police/Usalama kuchukua hatua... System failed and they should step down and let other Tanzanians to lead.

Matukio ya Mbagala, Iringa, Morogoro, Dr. Ulimboka, Kupigwa wabunge and yet no action taken, Morogoro, Arusha........
 
Ili kuufunga huu mjadala ningeseme kamanda alijiua baada ya kunyimwa penzi na dadaakeee! Be careful sijasema dada yake
 
Kwa kweli Mwanza inatisha. Nashauri IGP afanye uhamisho wa askari wengi sana waliopo Mwanza. Coz wengi hawaaminiki na wamekuwa kwenye siasa zaidi. Kama watataka ushirikiana wapangue askari waliopo wawapeleke Lindi na Mtwara na wa Mtwara na Lindi waende Mwanza..just my suggestion to IGP.

Hii mambo ya kuamisha hamisha ishapitwa na wakati --fukuza wote hata 4million FUKUZA
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza RPC Liberatus Ballow ameuwa usiku wa kuamkia leo na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu na Hotel ya Tai Five majira ya kati ya saa saba hadi nane.
Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Injinia Everest Ndikillo wakati akitoa taarifa za tukio la kuuawa kwa Kamanda Ballow.

Tukio hilo ambalo limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa jiji la Mwanza pamoja na familia yake huku watu wa kijiuliza kuhusiana aliyehusika na mauuaji hayo ya kikatili.

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa zinasema kuwa Kamanda Ballow alikiuwa anatoka katika kikao cha harusi na ndugu yake aitwaye Sembeli Maleto kilichokuwa kinafanyika katika Hotel y a Florida na kish akumpelek amwanamke aitwaye Dorcas Moses Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Nyamagana maeneo ya barabara ya Kona ya Bwiru kwenda Kitangiri.

Walipofika getini kwa Mama Dorcas mara waliwaona watu wawili wakiwa wamevaa makoti ya PolisiJamii, Mama Dorcas alimuuliza Kamanda Ballow kama anawafahamu Kamanda akasema kuwa hawa na watu wa ulinzi wa Jamii wako doria.

Mara wale watu waliongezeka na kuwa sita wakaanza kama kuzozana wao kwa wao na ndipo Kamanda alipowauuliza kuna nini, Mmoja wao akajibu hakuna kitu na ikapelekea Kamanda kutaka kutoka nje ila wale watu watatu wakaizingira gari ya Kamanda Ballow aina ya Rav 4.

Kamanda Ballow alipoona kama hali hewa inabadilika alichukua redio call ili aweze kuwa taarifu askari na ndipo wale jamaa walipompiga risasi kichwani nakupelekea kifo chake.

Taratibu za mazishi ya Kijeshi bado zinaendelea na nyumbani kwa marehemu ambapo mwandishi wa blogu hii amefika na kukuta watu mbalimbali wakiwa katika hali ya majonzi sana. Mke wa Kamanda Ballow yuko Dar es Salaam na anatarajia kufika Mwanza.

Mpaka sasa Polisi wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Dorcas kwa ajili ya Mahojiano huku uchunguzi mkali ukiendelea kuhusiana na kifo cha kamanda Liberetus Ballow.



 
je anayedaiwa kuwa dadake je ni dada kweli?
Je mke wake hausiki na mauaji haya kwa majibu ya upelelezi wa polisi kwamba mauaji yamesababishwa na wivu wa kimapenzi?
Je hawezi kuwa amejiua?...

Duuuh! ni utata tu huu
 
Back
Top Bottom