Kifo cha Lowassa kuombolezwa kwa Siku 5 kuanzia leo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
1707590422985.png

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo kuanzia leo February 10,2024 kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) ambaye amefariki Dunia saa nane mchana leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa kiongozi huyo mstaafu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kujikunja utumbo, homa za mapafu na shinikizo la damu.

Katika kipindi cha siku tano zote za maombolezo bendera zitapepea nusu mlingoti Nchi nzima.

Soma:
- News Alert: - Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo kuanzia leo February 10,2024 kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) ambaye amefariki Dunia saa nane mchana leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa kiongozi huyo mstaafu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kujikunja utumbo, homa za mapafu na shinikizo la damu.

Katika kipindi cha siku tano zote za maombolezo bendera zitapepea nusu mlingoti Nchi nzima.
Pumzika kwa amani Mzee Lowasa
 
Mzee Lowassa alikua kichwa sana niliwahi kumsikiliza akisema Maji ya Ziwa Victoria tutayatumia iwe isiwe haiwezekani chanzo cha maji kiwe Tanzania harafu Geita hakuna maji akiwa PM baadae kweli mkataba wao wa kibepari wakakubali baada ya kwenda kuwaomba...
 
Hiki ni kipimo kwa wale wanaoandaa maandamano huko Mwanza ,ambao Wana viongozi wa Kanda wanaoishi marekani wanaongoza Kanda ya Victoria kwa remote. Je ! Wataomboleza mgombea uraisi wao au wataendelea na fujo za maandamano?
 
Mambo matatu Daima yatamfanya ENL akumbukwe daima.

1. Msimamo wake imara wa Maji ya Lake Victoria kuanza kusambazwa nchini;

2. 2015, Kuitikisa CCM, Kuupa nguvu Upinzani na kuupumbaza pale ilipoporwa ushindi.

3. Kuhamia kwake CHADEMA, kulipelekea kufa CUF, Kukua ACT, Watanzania kupoteza imani na Siasa za Tanzania, madhala ambayo yanaishi hadi leo.

Historia ya Siasa nchi hii haitolisahau jina lake.

Apumzike kwa amani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom