Kicheche(player),kuna dawa ya kuacha?

Nifafanue vipi mkuu?
Player maana yake nini? nilivo elewa mimi ni kwamba unapenda sana kuanzisha uhusiano na wanawake mbali mbali, sometimes uhusiano unawapeleka kushiriki tendo la ndoa, alafu mnaachana kwa uamuzi wako, bila kujali kama mwenzio bado anataka au hataki. Haikusumbui kichwa kabisa ikiwa kuna uhusiano kati yako na wanawake wengi kwa wakati mmoja.
Am I right?
Sasa unataka kuacha kua player na kua 'mwaminifu katika mapenzi' (nimekosa neno kamili hapa). Basi anza kwanza kwa kuheshimu mwili wako na nafsi yako, usiwe unatoa kwa kila mtu.

nimekuelewa....na nimekupata sawia .
hapo kwenye mstari kwani player anakuwa hauheshimugi mwili wake? kivipi?
 
Kuufanya moyo wako uweze kukinai...kuridhika na kile kilicho mbele ya macho yako. Mfano.. Una girlfriend wako then mheshimu,mlinde,mkinge na machafu mbalimbali yakiwemo magonjwa..sio tena una girlfriend humtimizii hata upendo wa kweli,na bado macho yako na nafsi yako inatamani wanawake unaowaona barabarani....#Mbaya sana.

Akija mwenyewe Mwali ataelezea vizuri zaidi....
 
Ngoja nikupe mfano:

Kuna mtu mroho, mlafi: huyu akipewa chakula hawezi kukataa, hata kama kashiba, na hajali ni chakula gani, kimetoka wapi, ni cha nani. Yaani akiona tu chakula udenda unamtoka, anakula hadi mwenyewe anaona aibu. anakafirisha kitendo cha kula.
Mi Mwali napenda sana kula. Ila napenda chakula kizuri, na ndio maana nimejifunza kupika. Napika chakula cha kawaida tu ila ukila unapata ladha ya kila kiungo, bila viungo hivyo kuharibu ladha ya mboga. Ni mara chache sana nile chakula kama simfaham mpishi, na hata nikila restaurent ni zile ambazo nimesha ulizia kwa rafiki wanapikaje, ikiwezekana nimeongea na mpishi mkuu na kutembelea jiko lake. Kuna chakula nimesha amua siwezi kula kamwe, na zingine natamani ila siwezi sababu ya imani.

Sasa jaribu kulinganisha chakula na tendo la ndoa. Huyo wa juu ndio player, mimi sio player.
Umenielewa?
 
kwanza asante kwa ushauri nimekupata sawia bila chenga
let say namtimizia kila kitu upendo na mapenzi motomoto nampa..lakini bado tu ninatoka nje kuna ubaya?
 
Ngoja nikupe mfano:

Kuna mtu mroho, mlafi: huyu akipewa chakula hawezi kukataa, hata kama kashiba, na hajali ni chakula gani, kimetoka wapi, ni cha nani. Yaani akiona tu chakula udenda unamtoka, anakula hadi mwenyewe anaona aibu. anakafirisha kitendo cha kula.
Mi Mwali napenda sana kula. Ila napenda chakula kizuri, na ndio maana nimejifunza kupika. Napika chakula cha kawaida tu ila ukila unapata ladha ya kila kiungo, bila viungo hivyo kuharibu ladha ya mboga. Ni mara chache sana nile chakula kama simfaham mpishi, na hata nikila restaurent ni zile ambazo nimesha ulizia kwa rafiki wanapikaje, ikiwezekana nimeongea na mpishi mkuu na kutembelea jiko lake. Kuna chakula nimesha amua siwezi kula kamwe, na zingine natamani ila siwezi sababu ya imani.

Sasa jaribu kulinganisha chakula na tendo la ndoa. Huyo wa juu ndio player, mimi sio player.
Umenielewa?

nimekupata sawia
 
jamani mimi nimewapata sawia ila hamjanielezea jinsi ya kuacha au ushauri kutokana na mawazo yenu hapa naona mmenieleza tu ubaya wa kuwa player na kuwa sio vizuri kufanya hivi na vitu kama hivyo. ninachoomba ni jinsi ya kuachana na hii kitu sasa au nibadilishe life style niache kwenda kwenye bar,cinema ,beach,tour etc na vitu kama hivyo.
 
Nimekupa ushahuri, sema hukuuelewa:
Kwanza kabisa kaa chini na ujiulize unataka nini. Unavutiwa na nini. Alafu jitahidi kuupa Mwili wako na nafsi yako hivyo vitu tu, usikubali kwenda kiwango cha chini. imagine useme unataka mwanamke awe mnene, mweusi, nywele za asili, asiwe malaya, na awe mcheshi, awe na akili ya kujadili hoja mbali mbali etc. Sasa usikubali matamanio ya mwili kukupeleka kumtongoza mwanamke ambae hana vigezo hivyo. Utakua hujajitendea haki.
Upo?
 
Mwali umegonga ikulu kabisaa..kama ni manati yaani umempiga ndege kichwani, mara mbili zote mtu wangu mimi naingiaga chaka na imebidi hadi nimesitisha kutangaza ndoa na kwenda kutambulisha kwetu ,mdada mzurii kumbe tabia ni F ,samahani kwa kukueleza haya ila naona kama umenigusa manake hili jambo labda ndio chanzo chenyewe cha kutoa toa macho(player) coz natafuta kwa udi na uvumba ,basi mdada mwenyewe mwanzoni mwanzoni mpole huyo nikasema basi malaika si ndio huyu ,lol,,baadae alivyoanza ku display rangi zake basi mimi ndio sina hata hamu kwa ni aibu tupu,and this is second time same things different girls na hawajuani hawajawahi kuonana,au ndio uhusiano wenyewe upo hivi? nivumilie (hayavumiliki lakini)
 
Hivi unajua huwezi kwenda sokoni kununua bidhaa bila kujua una ngapi mfukoni?
Vile vile huwezi kujua ni mwanamke gani anakufaa kama bado hujajua thamani yako mwenyewe, na kama hujajua wewe mwenyewe una nini ya kutoa. Kama wewe uko fake, unajifanya uko A wakati wewe ni B, basi na watu utakao wakpata watakua hivo hivo. Be yourself, love yourself, respect yourself, na wengine watakupenda. Nobody can do it for you. :)
 
jamani mimi nimewapata sawia ila hamjanielezea jinsi ya kuacha au ushauri kutokana na mawazo yenu hapa naona mmenieleza tu ubaya wa kuwa player na kuwa sio vizuri kufanya hivi na vitu kama hivyo. ninachoomba ni jinsi ya kuachana na hii kitu sasa au nibadilishe life style niache kwenda kwenye bar,cinema ,beach,tour etc na vitu kama hivyo.

Wewe unataka uache kwa sababu zipi? Nguvu zimeisha? Endelea kuwaning'iza mpaka wakome. Tumia ujana wako vizuri na wakati ndio sasa. Kama jogoo linapanda mtungi endelea kukamua baba!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom