Kibiti: Polisi yaua watu wanne(4) wanaodhaniwa kujihusisha na mauaji wilayani humo

.....Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.....Chanzo: ITV
Hapo tu, naona kuna watu walibanwa korodani na kutema siri zote kabla ya kumalizwa...Safi kabisa, wauaji kabisa wale hakuna huruma kabisa..
 
Kuuwawa kwa hao wanaosadikiwa kuwa wauwaji ni hatua kubwa Jesho la polisi na nawapongeza kwa hilo
Ila kwa upande mwingine mmewauwa waalifu wote bila hata kumkamata mmoja au wawili wa kuhoji hata akiwa majeruhi?
Question mark
Swali la pili mashambulio mengi ya jeshi la polisi na wanaoshukiwa kuwa ni majambazi hayana tofauti na vita vya jw na jeshi lingine ni kuuwa 2 no majeruhi tulowakamata wakuhoji na kutuwezesha kupatabtaarifa zaidi imefikia mahali hata mtuumiwa anashukiwa kutaka kutoroka mahakamano na alikuwa chini ya ulinzi kala risasi ya kichwa
Hows these things?
Kazi ya mahakama ni ipi?
 
Kuna video ya hao jamaa wakirusha risasi? Mbona unaamini tu moja kwa moja bila kufikitisha ubongo?

Jesus???!! Kwahiyo ulikuwa unataka wajiselfie kama bongo movie wakati wanarushiana risasi???? Did u seriously wanted to post this au imejipost kwa bahati mbaya mkuu??? ...
 
Picha za bunduki zilizokamatwa au hizo maiti kama ilivyo kawaida ya Jeshi la Polisi ZIKO WAPI?
 
Hapo tu, naona kuna watu walibanwa korodani na kutema siri zote kabla ya kumalizwa...Safi kabisa, wauaji kabisa wale hakuna huruma kabisa..

Mkuu, kuna ubongo wa mtu umehoji eti kwanini wafe wote baada ya kujeruhiwa...Yaani mnataka polisi waseme kabisa kwamba baada ya kuwahoji fastafasta tukawandamiza kizenji..
 
Hongera sana polisi. Ni kazi nzuri, lakini tusiishie hapo kwani ni dhahiri kuwa bado hatujajua sababu ya hao wauaji huko kibiti. Pia japo sio rahisi ila tunaomba tuongeze bidii zaidi kuwakamata na sio kuua tuu kwani tunakosa ushahidi, ni kweli, kama tungefanikiwa kumpata hata mmoja akiwa hai angesaidia sana kujua mipango yao na idadi yao pamoja na mtu anayefadhili kundi hilo. Aluta continue
 
Kweli sisi watanzania tuna matatizo mmeambiwa baada ya kukimbia vichakani walianza kuwalushia risasi polisi ndipo mapambano yakaendelea mpaka polisi kufanikiwa kuwajerui kwa risasi ambapo badae wakawa wamefariki dunia then MTU anacomment et majambazi waliouawa kwa kudhaniwa! Watu waivo inatakiwa mkamtwe pia ilimtoe maelezo.
 
Wana uhakika? Isije ikiwa ni raia wema. Vinginevyo Good work
wew ni mjinga, watu wana silaha,wanawashambulia polisi alafu unauliza wana uhakika, mitanzania mijinga mijinga hii heri ungezaliwa burundi au africa ya kati huko
 
na kwanini kila kunapotokea shambulio la askari lazima waje na report inayosema "wanaohisiwa" neno "isiwa" linakujaje inamaana wanakuwa hawana uhakika na wanaowashambulia au ndo kujihami katika utoaji wa maelezo?
 
Umesoma bandiko langu nililomjibu ''Kolijojo''

Nimeeleza wazi kuwa katika mapambano ya kutafuta majambazi ya Pwani, hakuna namna Polisi wanaweza kufanya kila kitu kwa usahihi. Ni hali ngumu sana na ya hatari. Kuua ni sehemu ya mapambano

Hoja yangu ni kauli ya ''kusadiki'' kuwa 'wahalifu hao wana uhusiano na mauaji ya Pwani' bila kuwa na link
Hao wanaweza kuwa majambazi yanayaofanya ujambazi na siyo mauaji ya Pwani au yanaweza kuwa ndio majambazi yanayoua watu Pwani.

Forensic examination ya ushahidi wa silaha zilizopatikana na matukio ya nyuma ungeweza kutueleza vema. Je kwa muda mfupi wa masaa forensic imefanyika?

Kusema 'inasaidikiwa' bila kuwa na link yenye ushahidi kunaweza kutotupa picha halisi ya tatizo
Wamesema inasadikika au kudhaniwa kwa sab hawana uhakika kwa sab hawezi kusema wamefariki lkn cha msingi ni wahalifu.
 
Kama wamerusha risasi ni wahalifu hakuna tatizo.

Tatizo ni ''kusadikiwa' wanahusika na mauji ya Pwani'' bila kuwa na ushahidi wa ku link mauaji na wahalifu hao. Inaweza kuwa inaweza isiwe. Kinahoweza kutueleza ni utaalam
Hivyo ni mapema mno kusadiki tu bila kuwa na ''forensic exam''

Inafahamika vema kabisa kwamba maeneo mengi tu polisi wamekua wakipambana na halifu mbalimbali.

Kwa mfano kariakoo polisi walipambana Na majambazi yakiiba Kwa kutumia siraha, mbeya polisi waliwafukuzia majambazi walioiba pesa benki nk

Sasa inawezekana mkoa wa pwani kuna makundi hayo pia. Kutokana na mauaji yanayoendele Kwa Sasa ni dhahiri sasa kuna kundi jipya la uharifu linalowaua viongozi wa mitaa,vijiji,kata Na polisi.

Ndio maana taarifa inasema WANAOSADIKIWA, maana haijajulikana Kama ni majambazi wa kawaida tuliowazoea kila siku ama ndio wale wa mauaji ya kibiti.
 
Vikindu walisema waliwaua halafu yule msemaji wa wauwaji akawajibu hakuna waliyemuua..
hii vita ikipiganwa kwa maneno matokeo yataonekana mtaani..
vikindu tuliambiwa waliwauawa wote kasoro mmoja aliyetoroka.

Sasa kama unaamini maneno ya wauwaji ambao hata huwaoni badala ya polisi ambao unawaona sisi tukusaidiaje mkuu?
 
Back
Top Bottom