Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima bwana Kibanda ameandika makala kwenye gazeti la Tanzania Daima kumshutumu Zitto Kabwe kugombea uenyekiti Chadema.Kibanda anafanya kazi chini ya gazeti la Mbowe,swali Mwalimu Nyerere alipewa Uenyekiti wa Tanu akiwa chini ya miaka 30,
Chadema ni Chama cha demokrasia kwanini Kibanda aogope Chadema watimize kauli yao ya Demokrasia kwa Vitendo? kama Kigezo ni Umri Marekani wangempa John MC CAIN kwa vile ni mtu mzima ana mvi kichwa chote. Tanzania Daima la leo lina habari mbili zote za Zitto Kabwe.....
Umri hata siku moja hutakuwa mizani ya kuangalia kama mtu anauwezo wa kuongoza ama la. Hii article ni kama propaganda fulani na pengine Kabwe akisoma inaweza kumpa nguvu zaidi katika nia yake ya kugombea uenyekiti wa chama chake. Si haja kwa kweli ya kutoa mifano ya viongozi ambao hili swala la umri lilitolewa kama kisingizio cha kuwafanya "eti hawapo tayari kuongoza", hivi karibuni tu, Obama wa Marekani, Joseph Kabila wa Democatic Republic of Congo na wengine wengi. Wote hawa wanafanya kazi ya uongozi vema kabisa ....
Cha msingi tu ni yeye (Kabwe) kuwa na stratejia ya kupambana na wapinzani wake kwenye hicho kiti na kufanya kampeni maradufu, kama wananchi wa constituency ya Kigoma North walivyompa kura na kumchagua kuwa Mbunge, ndivyo atakavyoweza kuchaguliwa na wanaCHADEMA kuwa mwenyekiti. Godspeed!
Zitto ni mwanasiasa mzuri na mahili ila kuwa mwenyekiti wa CDM na kugombea uraisi kwa tiketi ya CDM bado sana mpaka atakapokuwa ana msimamo thabiti katika kupigania chama yuko kimaslahi yake zaidi anarubunika kirahisi mtu gani kuna wakati alitaka kuanzisha chama chake wakati anajua yeye ni tegemeo CHADEMA.