...."Weep not my child,Looh, OMG!
Jicho la plastic? The enemy is wining ... we must do smthing ...!!
Maana ya Breaking news imeshakosa maana kwa baadhi ya watu humu.Kibanda amefanyiwa upasuaji chini ya madaktari bibwa watatu, kati ya maktari hao wawili wakiwa ni wataalam wa kichwa na mmoja ni mtaalamu wa macho,
katika upasuaji huo madaktari hao wamegundua kuharibika vibaya kwa jicho la mwanahabari kibanda kiasi cha kulazimika kuliondoa nahivyo wanaangalia namna ya kumwekea la plastiki.
eatv
...."Weep not my child,
Weep not my darling,
the ravening clouds shall not be victorious,
They shall no longer posses the sky"...by Ngugi.
...."Weep not my child,
Weep not my darling,
the ravening clouds shall not be victorious,
They shall no longer posses the sky"...by Ngugi.
I love Manyerere Jackton, he is a reall son-of-a-gun. Manyerere Jackton is a Dedicted Journalist who wants right on every side, his and mine too. Lakini Manyerere Jacton is a New-Generation young man who does not know and cannot truely comprehend why (for example) Mwalimu Nyerere was known to have 'kionambali". Ukimwambia Mtemi Fundikira kuhusu kionambali atakwambia anataka wenye nacho ndiyo wamwongoze. Manyerere anataka kiongozi mwenye bashasha, mcheshi, mbunifu n.k. Lakini Manyerere, hii ni Dunia ya Mungu na inaongozwa na Mungu Mwenyewe. Matakwa ya Mungu katika wabadamu hujulikana kwa wenye hivyo unavyoita vionambali. Hao huambiwa kesho kutakuwa na dhoruba, na keshokutwa ukame. Usidanywe na Idd Amini mwenye ndoto za mwendawazimu, waulize wazee wako kama kuna mwenye kionambali katika nchi. Mkimficha wote mnajitafutia majanga, wewe na wazee wako na hili wazee wengi sana huwa hawalitaki kwa sabau ni majanga ya kujitakia. Msimamo wa Manyerere Jackton kama kijana na mwana habari ni kutuingiza vichochoro vya kutoelewa nini maana ya kionambali kwa sababu tu vijana wamepata kusema bila kusahihishwa na wazee.Uhuru wa kuongea hata Masai aliukataa kwa Morani, siyo ujinga, ndiyo ujanja wenyewe wa kujua makubwa ya Mungu. Manyerere, tumwombee ndungu yetu Kibanda apone na arudi salama lakini meno matatu na jicho moja hana. Usidhani nafurahia hali hii ya Kibanda, nasikitikia sana pia na hali ya Dr. Ulimboka ambao sasa hivi nina hakika wataishia kuwa "Siri ya Taifa" kama mnavyowaita. Kinachonikera ni kuwepo akina Manyerere Jackton na kalamu zao wakitamba kila mahali bila kuona hatari wanazoziparamia. Sasa hivi Watz tumegeuka waganga majeraha baada ya kuangukia mikenge badala ya kuikwepa tukaenda salama. Mara mitihani, mara Padri kauwawa, mara Ulimboka katekwa. Tume za kuchunguza haya ni kipofu kusaka sindano gizani ambapo hata Kikwete mwenye macho haioni. Manyerere amka kutoka ujingani, tutakwisha huku tukionana wakati tunahudhuria misiba ya waliotutangulia.
Hivi wewe ni pacha na Mzee wa Kwembe kati?Jogoo la shamba, nimesoma waraka wako. Umetoa changamoto kubwa, si kwangu tu, bali kwetu sote tunaopenda kuiona Tanzania ile iliyodhamiriwa kujengwa na wazee wetu. Kuna makala nimendika kuhusu Kibanda. Nisingependa isomwe kabla ya Jumanne-siku ambayo JAMHURI linakuwa mikononi mwa wasomaji. Kwa ufupi ni kwamba Watanzania wote, bila kujali rika, jinsi, hali, imani au aina yoyote ya tofauti zetu kama binadamu, tunapaswa kuungana kuifanya Tanzania kuwa mahali pazuri pa kila mmoja wetu kuweza kuishi. Miaka kadhaa iliyopita Tanzania ya aina hiyo ilionekana kupatikana, lakini kadri siku zinavyokwenda, sifa hiyo ya uungwana inapotea. Wajibu huu wa kuifanya Tanzania kuwa mahali pazuri ni wa wanahabari, madaktari, madereva, wachuuzi, walimu, wanasiasa, wafanyabiashara, waliooa na wasiooa, vilema na wazima, wazee, vijana na kila mmoja miongoni mwetu. Matukio ya kuvamiwa kwa KIbanda na wanahabari wengine, aidha, tukio la kuawa kwa Mwangosi na Watanzania wengine, ni mengi. Kama Taifa tunapaswa kusema "IMETOSHA". Naamini kabisa, kwa umoja wetu, na kwa mapenzi ya Mungu, tunaweza kurejea kwenye umoja, mshikamano na udugu wetu.
Du.!! Kabla hujafa hujaumbika..walaaniwe wote walio fanya unyama huu.
bilashaka kuchapisha makala ndefu iliyohusika na kuwepo chuo cha ugaidi huko ukerewe ndiko kumekuletea huu msiba. Pole sana bwana kibanda, hii ndio gharama ya kulinda na kutetea mstakabali wa nchi yako na watu wake.