Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

Pole sana Kibanda.
Asante kwa taarifa comrade.

BTW pamoja na kwamba kwa sasa mnashughulikia afya ya Kibanda, ni kipi kama waandishi mnashughulika
nacho ili kuhakikisha usalama wenu lakini pia waliomdhuru wanakamatwa. Ukizingatia kadri muda unavyokwenda
ndivyo pengine wahusika wanahakikisha ushahidi unafutika.

Najua Polisi wanasema wanafanyia hili kazi lakini pia kama waandishi kuna nyakati huwa mnafanya uchunguzi na
kuibua mambo mazito pengine yaliyowashinda hata Polisi. Whats way foward
 
Duh, poleni sana jukwaa la wahariri, waandishi, wanafamilia ya Kibanda, wapenda habari wote ndani na nje ya Tanzania kwa mkasa huu mbaya.

Vyombo vya ulinzi na usalama vina wajibu wa kuhakisha wote waliohusika na walionyuma ya huu mkasa wanajulikana na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria.

Tunaenda wapi Tanzania
 
Dah...halafu eti Ridhiwan anasema "Na huyu ni Rama Ighondo"?...saizi anaamua kumtuma mchumia tumbo Cyprian Msiba eti account yake imekuwa hacked!Kweli hujafa hujaumbika...Pole sana Kibanda Mwalimu wangu
 
Dah....ahsante kwa taarifa
pole kibanda,poleni wazalendo! Kama aishivyo Mungu nayemwamini siku zote
natabiri mwisho wa haya mambo haya ya kishenzi.Mark my words! mwakani majira ya joto wazalendo wengi
wa nchi hii watapata raha
 
nafikiri wewe jamaa hujawahi kusikia kitu kinaitwa ORGANISED CRIME toka uzaliwe si ndio.
Haya mambo yanatokea hata katika nchi zilizoendelea tofauti ya hapa na huko ni kuwa huko yameanza miaka mingi nyuma ,wakati hapa bado ni kitu kipya.

Organised crime ya kuteka watu na kuwatoa macho? organised crime huwa inalenga faida sio kuua watu na kuteka..especially Monetary profit sio kungoa watu macho na kucha...inaonekana wewe ni mbumbumbu katika haya masuala...
 
pole kibanda,poleni wazalendo! Kama aishivyo Mungu nayemwamini siku zote
natabiri mwisho wa haya mambo haya ya kishenzi.Mark my words! mwakani majira ya joto wazalendo wengi
wa nchi hii watapata raha

Jaribu kuweka bayana hii sentesi! Sijaambua kitu! Nini kitatokea?
 
Waliomshambulia inasemekana walikua wakimwita kiongozi wao 'afande'. Kama sio dola tuseme labda ni wanausalama wa dola wamekodishwa na watu binafsi? Au mnasemaje wana jf!! Wananchi tunafahamu askari wetu kwa kubobea kula rushwa siku hizi wanaweza kukodishwa!

'copy cat'
 
Kumsababishia mtu kuwa na jicho moja kwa makusudi,inasikitisha sana.
 
Napenda kuwapa taarifa za nyongeza kuhusu tiba ya Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda ambaye leo amefanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini.

1. Nimepokea taarifa kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Hussein Bashe kwamba tayari Mwenyekiti wetu, Kibanda ametoka theater alikokuwa akifanyiwa upasuaji. Hata hivyo taarifa mbaya ni kwamba Madaktari wameshindwa kuokoa jicho lake la kushoto hivyo wameling’oa.

2. Wamechukua hatua hiyo ya kitatibu baada ya kuwa tayari jicho hilo lilikuwa limepondeka kwa ndani hivyo lisingeweza tena kuona. Atawekewa jicho la bandia la plastiki ambalo hata hivyo halitakuwa likiona.

3. Jambo la kumshuruku Mungu ni kwamba kwa ujumla upasuaji huo uliochukua saa 5 na dakika 30 umefanyika kwa ufanisi mkubwa na ulikuwa ukiongozwa na madaktari bingwa watatu. Wawili kati yao ni wataalamu wa kichwa na mmoja ni mtaalamu wa macho.

4. Katika upasuaji huo, hakukuwa na madhara ya ndani katika kichwa chake, hivyo kichwa kiko salama. Sura yake imejengwa upya kutokana na majeraha ambayo yalikuwa yametapakaa baada ya kupigwa na watu wasiojulikana.

5. Changamoto kubwa waliyokutana nayo madaktari walionfanyia upasuaji ni kurejesha katika sehemu yake baadhi mifuma midogo inayozunguka jicho pia kurejesha taya la kushoto ambalo lilikuwa limeathiriwa na tukio la kupigwa kwake. Hata hivyo hatimaye walifanikiwa.

6. Ripoti kamili kuhusu upasuaji huo inatarajiwa kutolewa kesho Jumapili na madaktari hao.

Tuendelee kumwombea Mwenyekiti wetu Kibanda ili Mungu amponye. Kwaniaba ya Bodi ya Wakurungezi ya Jukwaa la Wahariri, kwa mara nyingine tunampa pole Kibanda pamoja na familia yake na tunamtakia uponyaji wa haraka.


--
[FONT=tahoma,sans-serif]Neville C. Meena,[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif]Secretary General,[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif]Tanzania Editors Forum - TEF,[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif]Dar es Salaam - Tanzania.[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif]Cell: +255 - 787 - 675555[/FONT]
[FONT=tahoma,sans-serif] +255 - 753 - 555556[/FONT]
 
Kweli kila mtu ni kilema mtarajiwa.

Mungu amtangulie,na ampe unafuu ndugu yetu.
 
huyu jamaa hapa namnukuu "Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania." ni mnafiki sana.....kulikuwa na haja gani ya kuripoti upasuaji na kutuambia ya Jekey?.....ni heri wange kuumiza wewe Neville kwa kuwa ni mnafiki kuliko watu wote ninao wajua

Mzee wa usafi,nakuunga mkono.
sipendi watu wanafiki.
Huyu kijana alinikera sana siku ya ulimboka.
 
Back
Top Bottom