Khah, First Date iliyonitoa jasho. . .

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
35,999
24,175
basi kipindi hicho kabinti nachipukia
kabyuti byuti ila sio sana.

Nimeombwa kutolewa out na kijana wa haja
baada ya kukalkuleti nikawa nishafika bei, nikakubali kutoka naye.

As usual, kama kwenye avatar yangu kibinti cha half kijijini/half mjini.

Nikajipigilia kile nilichoona ni kizuri kuliko vyote, hata mwizi angeingia na kubeba sanduku siku hiyo sikuwa na hasara.

Huyoo, nikaenda dinner.
Nadhani nilikuwa over excited
na kama kawaida yangu, I keep it real
nikaona kweli huyu kuku akatupwe? Roho ikakataa kabisa.
Kijana akajichanganya, akaenda toilet
mie huku nikaruka kwa furaha
Nikamfunga kwenye tissue paper yule kuku nikamtumbukiza pochini

basi tumepiga stori weee, mara muda wa kuondoka ukafika
tukatoka nje, wote hatukuwa na magari
akaniambia nimsubiri pale afuate tax
kama dakika 5

siku ya kufa nyani ndo ilikuwa ile
ile kaondoka niko nje ya hotel namsubiri
patrol inapita, kulikuwa na wageni wazito kwenye hotel hiyo wa kiserikali sie hatuna habari
si polisi wakanibeba kuelekea central polisi, uzuri nikamcal fasta nikamwambia anifuate

kufika pale, pochi hukaguliwa na kuorodheshwa vilivyomo
wakati bado naandikisha mali zangu ili niingie lock up
huyu hapa naye kafika
anashangaa yule kuku wa dinner anatokea kwenye pochi.
Akauchuna tu, akaongea nao hapo akawaachia kidogo
tukaondoka.

Jamani yule kuku alini-embarass hadi uzeeni huwa ananitania sana.
Eti kuku nilimla akafufukia kwenye pochi.

Ulishawahi patwa mkasa kwenye first date?
Hebu tupe mistari yako. . . .
 
Konnie nakudai mbavu zanguuuuu... Hahahahhaahhahahahaaaaaa......

Kwamba umekula kuku akatokea pochini?!
 
Binti uka-take away kisela ha..ha..ha kazi kweli kweli sijui ulitaka ukanywee chai asubuhi? Kweli sisi wa uswahilini haturembi.Hii ni XXXL.
 
kiukweli kilichonisumbua nikashindwa kumla ni Uma na kisu.
Niliona ataruka juu kama ana mabawa lol

Binti uka-take away kisela ha..ha..ha kazi kweli kweli sijui ulitaka ukanywee chai asubuhi? Kweli sisi wa uswahilini haturembi.Hii ni XXXL.
 
kiukweli kilichonisumbua nikashindwa kumla ni Uma na kisu.
Niliona ataruka juu kama ana mabawa lol

Ha..ha..ha nakuelewa sana Kisu na Uma ni changamoto sana,ila siku ukialikwa kwa mchina utajua umuhimu wa kutovunga kuomba maji ya kunawa mikono...afadhali uma na kisu lakini kuna vile vijiti yaani sitaki kuvisikia kabisa vilishawahi kunilaza njaa mimi.Kisa na mimi nionekane hawavumi lakini wamo ilibidi asubuhi ninawe mikono mwenyewe ili kuziba mashimo.
 
Back
Top Bottom